Imagine ZITTO anahama CHADEMA

Imagine ZITTO anahama CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Swala si migogoro ndani ya CHADEMA. Zitto alitumwa na mafisadi kuuwa CHADEMA. Ndio maana alianza kufagilia ununuzi wa DOWANS.

Sasa tujiulize, je huyo ndie Zitto alietaka kuwa mwenyekiti? Angeupata huyo uenyekiti, si angeuwa chama?

Zitto si CHADEMA, CHADEMA itaendelea kuwepo bila Zitto au Dr. Slaa.

Kumbukeni CHADEMA na Dr. Dlaa ndie walitufundisha kuhusu mafisadi, EPA, Kagoda etc.

Mimi nawaambieni mnaojifanya mnamtetea Zitto endeleeni kumtetea tu. Kwa mfano, Dk Slaa ambaye kiitifaki yuko juu yake na alitumia mamlaka yake kwa mujibu wa utaratibu wao ambao yeye Zitto anaufahamu na anaujua vizuri kuwatimua kina Juju naMpuuzi mwingine anaitwa Kafulia, mwenyewe Zitto asivyo na adabu akakurupuka kujibu uamuzi huo kupitia Mwananchi!

Ningekuwa Slaa on the spot ningemtimua. He is not deserving to be a leader. What kind of a Leader Chadema is having? Indiscipline leader is also need to be chased away!

ZITTO TOOOOOOOOOOOOOKA WAACHIE WANACHADEMA CHADEMA YAO
 
  1. Inasikitisha kuona jinsi Dr. Slaa anavyoendelea kulaghai umma kwa kukataa the obvious. Kama hakuna mgogoro, anafafanua nini kila siku kwenye vyombo vya habari?
  2. Huku kumuandama Zitto as if hawezi kumpata kwenye simu na kujadili hayo anayojadili kwenye wanahabari sijui nako kuna nia gani.
Dr. Slaa wa leo sio yule tuliyekuwa tunamjua miezi michache iliyopita. Wa sasa anaonekana shallow na mnafiki.

Nafuu ya Mbowe ambaye yeye kakaa kimyaa kimya kabisaa kama vile sio kiongozi wa CHADEMA. Kamuachia Mzee wa wa watu wa kimbulu amfanyie madudu yake na wakati huo huo kujimaliza mwenyewe.

Dr. Slaa yupo sahihi kabisa kwa hili, na kama zitto aligawa password yake basi ni Uzembe ambao hauwezi kabisa kufikirika. Password maana yake ni nini?

Mbowe yeye ni mwenyekiti ana majukumu mengine ya kichama, katibu mkuu lazima awe ndiyo mfafanuzi ya masuala ya kichama kama haya.

Chadema ni taasisi si mali ya Mtu sasa kama Zitto na wenzake walijidanganya wanaweza kuiteka wamekwisha, Aliondoka Kaburu itakuwa yeye aamue haraka hata aitume hiyo kwa barua pepe itamfikia boss wake atutangazie tujipange tujue moja

Hakuna haja ya kukaa na vijikundi ktk chama, bora uuwe mzizi wa fitna mapema.

Na kama alitumia email address ya CHADEMA kufanya hizo correspondances basi ni kosa kiasi kwamba chadema inaweza hata lumshitaki sababu email address ya kampuni huwezi kutumia kwa mawasiliano ambayo hayahusu kampuni husika.

Si point Dr Slaa ampigie zitto simu, yeye zito anatakiwa ariport makao makuu yote haya sababu bado ni kiongozi wa chadema.

Nipo kipenzi sana na huyu jamaa ila baada ya tu ya kuiningia Kamati ya madini ndipo akaanza kupoteza uelekeo taratibu. Anadhani watu watamuamini kuwa mambo anayofanya?
 
Mimi nawaambieni mnaojifanya mnamtetea Zitto endeleeni kumtetea tu. Kwa mfano, Dk Slaa ambaye kiitifaki yuko juu yake na alitumia mamlaka yake kwa mujibu wa utaratibu wao ambao yeye Zitto anaufahamu na anaujua vizuri kuwatimua kina Juju naMpuuzi mwingine anaitwa Kafulia, mwenyewe Zitto asivyo na adabu akakurupuka kujibu uamuzi huo kupitia Mwananchi!

Ningekuwa Slaa on the spot ningemtimua. He is not deserving to be a leader. What kind of a Leader Chadema is having? Indiscipline leader is also need to be chased away!

ZITTO TOOOOOOOOOOOOOKA WAACHIE WANACHADEMA CHADEMA YAO

Ndiyo aondoke, alikikuta na atakiacha. chadema si mali ya mtu ni taasisi.
 
Niliwahi kuandika siku moja kuhusu siasa za Tanzania. Siaza za Tanzania ni kama ifuatavyo:

1) Ni mchezo wa kuigiza ambao hauna maandishi, kwa hiyo kila anayeigiza hakuna anayejua kitakachotamkwa kwenye "scene" ifuatayo jukwaani

2) Ni mchezo wa kuigiza ambao hauna "mwongozaji" ("director"), na kwa kuwa hakuna "director", anaweza akatokea "director" wa muda, wakati wowote ule, kushika hatamu, na kuachia ngazi anapojitokeza "mwongozaji" mwingine mahiri zaidi kuliko huyo aliyepo.

3) Ni mchezo wa kuigiza ambao hauna waigizaji rasmi, kwa hiyo yeyote yule atakaye anaingia na kutoka kadri apendavyo.

4) Ni mchezo wa kuigiza ambao hauna mandhari maalum wala maudhui maalum, kwa hiyo mada hubadilika kutokana na wakati uliopo.

Kazi kwenu!

./Mwana wa Haki
 
HUO ndio mwisho wa Chadema.

Mchawi wenu ni Dr Slaa. Kwani Elimu yake ni ubabaishaji mtupu na utata kibao sasa analeta kwenye chama.

Poleni sana Chadema. Akiondoka Zitto na chama kimekufa. maana yake majimbo ya Kigoma zero

wewe ndio bunguwani kabisa...Zitto sio CHADEMA!! aliondoka Kabouru itakuwa zitto..kama hujui undani wa mambo ni nora ukae uwani kwako ucheze drafti na wanao..Eti Dr.Slaa ana elimu ya kubabaisha...unajua unachoongea au unabwabwaja tu???hivi kwani lazima muwe wanachama au washabiki wa CHADEMA?? huyo Zitto aondoke hata leo hatumuhitaji na chama kitaendelea kuwepo..nyie vipi
 
1. Zitto nafikiri ameridhika haraka sana.

2. Hila mara zote ukiona mtu anaanza kujisifia mwenyewe ujue kuna kitu anaficha.

3. Baadala ya kukaa anatishia nyau ni bora tu achomoke Chadema na kutafuta Chama mbadala kitakachomsaidia (either NCCR au CCM).

4. Chama Chochote cha siasa lazima kiwe na nidhamu. Bila nidhamu siyo chama, kwamfano CCM ya sasa siyo Chama.

5. Zitto inawezekana amekosa experience ya kukaa na watendaji, aangalieni maana amepanda haraka na anaweza kushuka haraka.

6. Huyu jamaa anatuchanganya wakati tunaelekea katika uchaguzi.
 
Msitake kuleta ushabiki wa kivyama, kwa mtu mwenye akili timamu atakuwa na jibu kuwa Chedema kuna mgogoro na sasa ni dhahiri kabisa.

Chadema wameingia kwenye tabia ya CCM kuanza kulumbana kupitia vyombo vya habari. Hii ni hatari sana kuna mambo yanatakiwa kuzungumzwa na wanachama kwa siri. Inasikitisha kuona chama ambacho tulikuwa tunakipa nafasi ya kuleta mageuzi nchini kinaingia kwenye migogoro ya kijinga.
 
HUO ndio mwisho wa Chadema.

Mchawi wenu ni Dr Slaa. Kwani Elimu yake ni ubabaishaji mtupu na utata kibao sasa analeta kwenye chama.

Poleni sana Chadema. Akiondoka Zitto na chama kimekufa. maana yake majimbo ya Kigoma zero

Nilifikiri ukitoka Hijja utakuja umebadilika kumbe ni yule yule!
 
Hizo ni mbinu tu za kuanza kudhoofisha vyama vinavyoonekana vina nguvu, hadi uchaguzi unafika vimesambaratika.
Hoja ya HM Haffif ni haffifu na ya mawazo yaliyolala. Watu wa namna hii ndo wanatuharibia Maendeleo ya Taifa letu.
 
chadema wana mgogoro,na hawataki kuutambua huo mgogoro ili waweze kujua jinsi ya kuutatua na kuutuliza. tatizo ni kutokujitambua cc ni kina nani

Ndiyo. mgogoro uko Chadema, umepandikizwa na mafisadi wakiongozwa na RA na kumtumia Zitto na wenzake kufanya vurugu.

Na haihitaji PhD kujua kwa nini mafisadi wanataka Chadema ivurugike.

Zitto ni kaput -- na ilianzia wakati ule wa kutimuliwa Bungeni kwa suala la Buzwagi -- chati ilipanda sana hata magazeti na watu wakaanza kusema "Zitto for President" Akavimba kichwa na kujiona kuwa anaweza kummg'oa Mbowe, pamoja na kuwapo Bungeni kwa miaka 3 tu.

haraka yake -- au tuseme, kusukumwa kwake na mafisadi -- ndiyo kunamuangusha kisiasa. Angefanya subira. Angekaa Bungeni hata angalau vipindi 2 (kama angeweza kufanya hivyo -- lakini naona ingekuwa ngumu sana kwake kutokana na kutowajali wapiga kura wake) na angeweza tu kumrithi Mbowe. lakin tamaa daima ndiyo inawaponza watu.

Mimi naona asifanye makosa ya kwenda NCCR -- ni bora aende CCM kama vile Lamwai alivtofanya ambaye sasa wala hajulikani yuko wapi.
 
Miezi michache iliyopita tulimshambulia Kibanda hapa kwa makala yake kuhusu misimamo ya huyu Zitto na vision yake, now it gets clear that the guy was right!! This is so frustrating.
Hatuhitaji kuwekeza kwenye watu ambao wanaweza kununuliwa au chochote kutokea, tuwekeze kwenye ukweli na misingi sahihi ya kuokoa nchi hii kutoka kwenye mikono ya wanyang'anyi. forget about Zitto and co.[/QUOTE

Mimi nawashangaa sana! Mnapokuwa busy kujadili kama Zitto anahama au ahami ni sawa na kuunyanyua Mkia wa Mbwa halafu unauliza anatolea wapi Haja kubwa! Ni upuzi! Zitto ni SISIMIZI. Aondoke tu, full stop. No need of compromising. Hakutuma application letter alipotaka uanachama so awe free kutimua, na mimi nitakuwa mmoja wa watakao ogelea Bierre siku nitakayosikia ameondoka.
 
Umepigilia msumari mahala pake ndugu yangu. Zitto kamalizwa na akina RA na mafisadi wenzake. Kusema kweli Chadema imewaumbua sana sana jamaa hawa wanaoututia umasikini, kiasi kwamba sasa hivi wanaona bora Chadema ikafilia mbali -- eti ndiyo wanaona salama yao. Wamebakia wanabwbwaja tu -- mafisadi hawatakiwi popote duniani, na nakubaliana na Slaa kwamba waendeleze mapambano ya kuwafichua wote.

Watajaribu, kama wanavyofanya, na wao (akina Slaa na wenzake) kupakwa matope lakini potelea mbali -- hii ni kawaida katika mapambano yoyote ya haki. Matope ya akina Slaa hayawezi kufikia EPA, Kagoda ettc.
 
Miezi michache iliyopita tulimshambulia Kibanda hapa kwa makala yake kuhusu misimamo ya huyu Zitto na vision yake, now it gets clear that the guy was right!! This is so frustrating.
Hatuhitaji kuwekeza kwenye watu ambao wanaweza kununuliwa au chochote kutokea, tuwekeze kwenye ukweli na misingi sahihi ya kuokoa nchi hii kutoka kwenye mikono ya wanyang'anyi. forget about Zitto and co.[/QUOTE

Mimi nawashangaa sana! Mnapokuwa busy kujadili kama Zitto anahama au ahami ni sawa na kuunyanyua Mkia wa Mbwa halafu unauliza anatolea wapi Haja kubwa! Ni upuzi! Zitto ni SISIMIZI. Aondoke tu, full stop. No need of compromising. Hakutuma application letter alipotaka uanachama so awe free kutimua, na mimi nitakuwa mmoja wa watakao ogelea Bierre siku nitakayosikia ameondoka.

Mkuu jaribu kutushawishi kwa hoja si kwa maneno yanayotufanya wote kwenye hili jamvi tuonekane wehu!
 
Mpendwa Mheshimiwa Zitto,
Hivi karibuni katika moja ya thread humu JF, nilisema kuwa Rostam Aziz amenunua viongozi wetu wengi wa kisiasa, nikasema kuwa huyo bwana anamwagilia miche yote maana hajui upi utakao chipua. Nikawasema kwa majina watu ambao wamekuwa wakifadhiliwa na RA hata nikaandika kuwa Rostam alichangia kwenye kampeni za ODM ya Kenya.

Nilsema kuwa sijui nani anafadhili masomo yako huko ughaibuni lakini nikasema bayana kuwa Rostam ndiye aliyegharimia masomo ya Mbatia huko huko ughaibuni. Sasa mambo yanayoendelea kwenye chama chenu yanatia wasiwasi mpaka sisi wapiganaji tunaona kama kamanda wetu umenunuliwa na huyo huyo Rostam. Tuna wasi wasi mkubwa kwa sababu tunajua jinsi mbinu chafu za fisadi huyo. ninakuomba usije ukatumbukia katika mtego huu wa kifisadi na kujitoa CHADEMA ukaenda NCCR,

NCCR Mageuzi ni chama chenye historia ya kukumbatia mamluki, wapo wengi na wengi wamepitia hapo. Lakini kitendo chako cha hivi karibuni kufadhili swahiba wako aliyefulia na kuanza kutukana chama chako unachokiongoza, kimeleta wasiwasi mkubwa kwetu, sisi tunaokuamini na kukuheshimu.

Hatujui mbinu hiyo ya kuibomoa chadema ni ajenda ya nani!!! kamwe sitaki kuamini kuwa wewe Zitto Kabwe tunayekujua waweza kusaliti vuguvugu la kukomboa nchi hii na kujiunga na mafisadi wachumia tumbo! Hatutaki kukubalia na hoja zozote za kututenga wewe na sisi, maana bado tunakuhitaji mstari wa mbele wa mapambano.

Mpendwa Zitto, mbona umebadilika hivi kwa siku za karibuni? Kwanza ulianza kutetea kununuliwa kwa Dowans, baadaye ukaona vema kupimana nguvu na ikiwezekana umwondoe Freeman kwenye uenyekiti wa chama. Kukaa kidogo ukaanza kumsifia Idrisa Rashid, Fisadi na tapeli wa kutupwa aliyesababisha NBC kufilisika na kuuzwa kwa bei chee ambaye pia amehusika kwa tuhuma za ufisadi mkubwa mkubwa wote hapa nchini. Zitto mdogo wangu, bado hayo yalipokwisha ukaanza kuwakumbatia watu wanaovuruga chama unachoongoza na bado unawakumbatia!! kwani ungetegemea katibu wa chama awafanye nini wafanyakazi wa chama wanao kiuka utaratibu??

Zitto, kwa kweli sikubaliani na wewe kumtetea kafulia kwa vyovyote na kama ulishiriki kumshauri ajiondoe kwenye chama, ulifanya makosa makubwa na umejiunga na wahaini wengine wowote. Kwani Kafulila ilikuwa ni lazima awe Ofisa wa Chama? kwa nini hakukubaliana kuacha hiyo ofisi akajiimarisha na kisha kuwa kugombea na kuwa kiongozi?

CHADEMA ni kubwa kuliko mtu yeyote. Si Mtei, Mbowe, Slaa au wewe ambaye ni mkubwa kuliko Chadema, kwa hiyo ilikuwa ni vyema kama kuna hoja ambazo tumezisikia kwa Kafulia akupatie wewe au ampe mtu mwingine ziwasilishwe kwenye vikao vya chama. Kafulila alikuwa anahoji utiaji wa saini kama nani? Je mnataka sisi watu wa mitaani ndiyo tujadili na kuwashauri nyinyi kamati kuu ya CHADEMA nani atie saini na nani asitie? hilo si ni jambo la ki utendaji tu? au Freeman ndie amekuwa mwenyekiti wa kwanza kutia saini zake kwenye hundi?

Mpendwa Zitto kama umesukumwa na mafisadi kubadilika hivi, ujue umma wa watanzania tuliokuwa nyuma yako tutakuacha na utakuwa mwenyewe wewe na mbatia na Rostam. Hakika utapotea kama alivyopotea Marando, Lamwai na Kabouru. Fikiria sana kabla hujaamua chochote. Nyota yako inawaka kwenye CHADEMA na itazimika wakati wowote. Ebu Muheshimiwa, mtafute DK Slaa, mjadili a way forward kabla mambo hayajakuharibikia, najua thamani yako kwenye CHADEMA haitapungua hasa baada ya kuwa mkomavu na kuondoa jina lako kwenye uchaguzi ule.
Wasalaam
 
watu wamejitoa ANC na bado inaendelea iweje watu wajitoe CHADEMA ife? Mnao lipwa na mafisadi ili muisambaratishe hizo njaa zitawamaliza.
 
HM Hafif katoka hijja .....basi ni udini mpaka afe mwe!!!
 
Kubwajinga said:
Alisema alielezwa na mama huyo kuwa wapo watu wanaomtumia Zitto kwa maslahi wanayoyajua wenyewe na kwamba mtu mmoja (jina linahifadhiwa) anayo password ya anuani ya barua pepe ya Zitto ambayo anaitumia kuandika taarifa mbalimbali alizoeleza zinaonyesha kama vile zinatoka kwa Zitto.
Wapi Mwita Maranya?
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom