Imagine ZITTO anahama CHADEMA

Imagine ZITTO anahama CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Hatuna uhakika wa kujitoa Zitto ila inaonekana yuko over ambious na kwa umri wake angetulia na kuijenga Chadema Uenyekiti ungekuwa wake katika muda si mrefu ujao.
Vijana wanatuvunja moyo watu wote tunaopenda mageuzi na wakati mwingine unapata kichefuchefu.
Nilikutana na Tambwe Hiza akiwa CUF katika vijiji vya Kusini mwa Tanzania akiwaeleza wananchi kuhusu ununuzu wa rada na ndege ya Rais akilinganisha gharama zitazotumika na umaskini wa wanavijiji wale;leo yuko kwingine na anaponda alikotoka na kusifia alipo.Naamini dhamira zitawasuta wengi na hawatakuwa na amani ya moyoni kwa maisha yao yaliyobaki.
 
Hii habari imekaa ki "ujinga ujinga". Eti Zitto anatembea na barua ya kujiuzulu! Kwani inachukua dakika ngapi kuandika km mtu ameamua? Haya ndiyo mambo ya kipuuzi na uzishi. Hivi unaweza kutembeaje na barua ya kujiuzulu???? Na unatakiwa uembee nayo siku ngapi? Ukiandika si ndio kumaanisha???
 
Mh. Zitto tuweke sawa Wafuasi wako.

Wewe unayetaka kuwekwa sawa kwani uko tenge!!!!!!
Habari yoyote ya udaku majibu yake yanategemea akili yako wewe msomaji, hivyo majibu mnayo.
kwani Zitto kujiondoa CHADEMA ni kitu gani cha ajabu cha kukunyima kufikiria mambo mengine ya maana? Kama anajiondoa ni juu yake yeye na itafahamika tu, sasa aweke sawa nini.
 
Ha, mwananchi hawajipendi? Litabadilika kuwa rai mda si mrefu

Ninachojua mimi (ambacho nimewahi kuambiwa na mmoja wa waandishi waandamizi Mwananchi) Reading Story kubwa za mwananchi zimekuwa haziwekwi kwenye webu kwa vile watu wengi wamekuwa wakiziiba na kama mtakumbuka kuna wakati story zao zilikuwa zikifanana sana na zile za Nipashe.
Na mara nyingi story ambazo ni scoop kwa magazeti mengine wamekuwa hawaziweki.
 
Kwenye hili mtalaumu watu wengine lakini ukweli unabaki pale pale kwamba hii yote ni vita ndani ya CHADEMA. Kuna watu wanatafuta mchawi wa kumsingizia ili kutatua matatizo yao binafsi.

Picha inarudia ile ile kama ilivyokuwa kabla ya kifo cha Wangwe. Watanzania tutajifunza lini kwamba kutofautiana kisiasa au kimsimamo si uadui?

Kama kuna mtu anategemea Zitto ajiondoe CHADEMA kipindi hiki, huyo hajui siasa za Tanzania. Ni Mrema peke yake alishawahi kuachia ubunge na kupoteza marupurupu yote. Wengine wote wanasubiri mpaka bunge limalize muda wake.

Mkimuandama sana Zitto basi ataamua asigombee 2010 ili aende kuchuma mapesa mengi kwenye private sector na kurudi tena 2015.

Msije mkampa pressure kubwa Zitto na yeye akaishia kupata ajali. mwacheni asome shule yake kwa faida yake na chama chake na nchi yake.
 
Jamani nimeona article inayosema Zitto yuko mbioni kujiuzulu Chadema katika Mwananchi! Cha kushangazwa article hiyo wameitoa ghafla! Sasa najiuliza kulikoni?

Unajiuliza nini kwani Chadema mlimnunua Zito? Kama mlimnunua mlitoa bei gani?
 
Mambo CHADEMA yalianza kuharibika wakati wa Wangwe...Mlitakiwa m salve wakati ule, sasa its too little too late.
 
Hawa ndio waandishi wa wetu...!!! kila mtu anataka ajenge au awe na gari nzuri....ili uyapate hayo kanuni nyepesi ni kuchafuana ktk habari...!!!
 
Tuangalieni sana kwa makini juu ya tarifa hizi. Kwenye gazeti la mwanachi la leo kuna tarifa hizo za zito kujiuzuru. Lakini ukienda kwenye mtandao wao www.mwananchi.co.tz hakuna kitu kama hicho. Hii inaonyesha kuwa ni habari ya kupika. Halafu ukiisoma vizuri utaona kwamba Zitto aliwasiliana na mwananchi kwa barua pepe, lakini mwishoni wanasema zitto aliwapigia simu? Kipi kati ya hivyo ni sahihi? Na kwanini hiyo habari iliondolewa online kama inaukweli wowote?

Nadhani Mafisadi wameshajua kuwa Gazeti la Mtanzania halina soko tena na wala halina mashiko kwa WaTz. Bila shaka nyote mnakumbuka kabla ya uchaguzi wa CHADEMA, GAzeti la Mtanzania lilimuandama sana Dk Slaa kwa habari za ajabu na hata kumnukuu kuwa "Dk Slaa kutogombea Ukatibu Mkuu!" na hata kuweka kwenye MAoni yao ya Mhariri "Dk Slaa kwa Kutogombea Ukatibu Mkuu CHADEMA ni jambo la kuigwa!" HAbari za Slaa 'kutogombea' Ukatibu Mkuu ziliripotiwa mara kadhaa. Jambo la Ajabu ni kuwa KAtibu Mkuu wa CHADEMA ni nafasi ya kuteuliwa!

Kwa MAfisadi kugundua kuwa habari za kudhoofisha Upinzani kupitia Mgazeti yao wanayomilimki ya Mtanzania sasa wamehamishia nguvu hizo Mwananchi. Naweza kuona kuwa kwa habari hizo za MWananchi, gazeti hilo litapoteza credibility yake kwa Watanzania kama MAgazeti ya New Habari Corporation (Mtanzania, Rai, Dimba, The African)

Labda Mwananchi nao wameshauza baadhi ya Hisa kwa Mafisadi au Mafisadi wamemkabidhi Ali Mufuruki rungu la kupamabana na Wapinzani. Pia inawezekana lengo la Mafisadi ni kujaribu kutusahaulisha WaTz habari za Mafisadi na Ufisadi hapa TZ.
 
Watu ninyi mliowekeza kwa watu wengine mtakuwa mnakerwa sana kwa kila habari.

Jisimamieni, na mjiamini na sio kuwekeza kwa watu.
 
Watu ninyi mliowekeza kwa watu wengine mtakuwa mnakerwa sana kwa kila habari.

Jisimamieni, na mjiamini na sio kuwekeza kwa watu.

Mkama, ninajisimamia na najiamini. Ukisoma ile thread ya CHADEMA mambo mdundo nimechangia pale na kusema kuwa kuna tatizo katika Uongozi wa CHADEMA Taifa kwa kutoa marejeo tangu enzi ya Chacha Wangwe hadi kwa Kafulila. LAkini katika habari hii ya MWananchi naona kabisa ina walakini kubwa na ina mission yake kwa Wapinzani wa CCM. Hivi wewe Mkama unaamini kabisa kuwa hiyo habari ni kweli? Huyo MWandishi ameiona hiyo barua au ameona bahasha tu akaambiwa kuwa ndani kuna barua ya Zitto kujiuzulu CHADEMA?

Hata kama Zitto ataondoka CHADEMA bado hainifanyi niisaidiki hiyo habari ya MWananchi maana habari imekaa kiumbeya na hata wao Mwananchi hawajiamini kwa habari hiyo.
 
Hao ni wafanya biashara. pamoja wanatuhabarisha lakini pia ni wafanya biashara
 
I’m sensing a fascinating trajectory in this, it possibly correlates with what he had to say as an interviewee to Mohamend Dewji.
Retrieved at; http://www.mohammeddewji.com/blog/2009_11_01_archive.html

Dewji: Je safari yako kisiasa itaishia kwa ubunge tu, wapo vijana wengi na wadau wanasema una uwezo wa kuwa Rais, umefikiria kuhusu nafasi hiyo?

Zitto: Urais? watch my steps........

Dewji: Wewe ni mmoja wa wabunge waliolifanya bunge la kuanzia mwaka 2005 kuwa la kusisimua zaidi na lenye meno, je una mpango wa kutetea kiti chako cha Kigoma Kaskazini mwaka ujao?

Zitto: Mpango wangu ni kutogombea tena ubunge ili niweze kusoma na kupata PHD na niweze kuwa mhadhiri wa chuo kikuu. Ninapenda zaidi kufundisha kuliko siasa. Kuna shinikizo kubwa kuwa nigombee tena. Lakini nafsi yangu ni nzito sana kurudi Bungeni Bunge la 10. Nadhani nitarufahi zaidi nikiongoza chama changu kupata wabunge wengi zaidi na mimi nikae nje ya siasa kwa muda kidogo. Niliweka nia yangu hii toka mwezi septemba mwaka 2006. Lakini watu hawataki kabisa kuelewa hili. Nadhani sitagombea............

If he has to walk his talk then it won't necessarily be an outcome of political frictions,instead it can be what Maslow calls a self-actualizing mission.
 
Mimi pia niliiona article hiyo na ni kweli ipo kwenye gazeti la mwananci la leo ila naona webmaster wa mwananchi aliiweka na huenda alipigiwa simu na watu fulani na wakaitoa kwenye website yao lakini ukisoma hard copy ya gazeti la mwananchi jumapili la leo article hiyo ipo.

Naomba wadau article hiyo iwe scanned na tuisome.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom