Huyu Johnthebaptist Yuko Wapi?

Siyo kweli. johnthebaptist alikuwa na energy kubwa sana kwenye uchangia hoja JF kwenye kila jukwaa. Nadhani alianza kupotea kwa sababu ya kufungiwa na Serikali mwaka jana mwezi Septemba. Ila baada ya JF kufunguliwa sijamuona kabisa akirudi. Yawezekana amefariki ngoja tuendelee kusubiri pengine atatokea kama alivyotokea denoo G na raraa reree ambao pia kwa muda mrefu hatukuwaona
 
Dahh nilipata rafiki mpya, TheSeer sijui yuko wapi tulipanga vzr tu kupambana na maaskari siku hiyo🥲
 
Usijekuta masisiemu walimchinja kama kawaida yao kutoa roho za wenye mawazo tofauti, au ndio alikuwa Polex2, ujue hizi aidii feki zinaficha mengi humu, hata mamaduro alisema anasoma sana hapa so obviously ana aidii feki coz hatuoni jina lake jamvini!
 
Kuna wakati watoto wake walimpeleka Soberhouse maana alizidisha pombe hadi mikono inatetemeka hawezi kushika hata simu, sasa sijui ameishia mazima huko maana kimya kimezidi .
 
Huyu MwanaJF yuko wapi ni muda sasa hajaonekana hapa jukwaani.

Nimeona reply yake ya mwisho ni mwezi wa tisa mwaka jana.
Kabla ya uchaguzi.



johnthebaptist
Isije kuwa kesha ingia kwenye orodha mpya ya watekwaji tu?Kwani vibakora bado tunatembeatembea!Jo popote ulipo fanya kama unajikuna tukuone tafadhali!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…