Hili suala la wanafunzi kubaki shule lina umuhimu mkubwa kwa maisha ya baadaye ya mtoto wako

DR HAYA LAND

JF-Expert Member
Dec 26, 2017
18,132
45,932
Wazazi mwanao kama yupo form four, aendelee kusoma na kujisomea, haya matamko ya wanasiasa ni matamko ya kisiasa.

Wewe mwanao yupo shule ya kata, na unajua kuwa ili aweze kupata nafasi ya kwenda hata VETA au kuongeza ujuzi wowote basi cheti cha Form four lazima.

So akili kichwani, yaani mzazi unakaa na kusubiri future ya mwanao ambaye yupo shule ya kata iliandaliwe na waziri!

Mwanao akipata zero hata upolisi hawamchukui na huko mtaani ndio kizazi cha singeli hiki, pathetic.

Nimeandika maana nipo uswahilini De es Salaam, nimeona watoto wa kike na kiume wakikaa mtaani wanaishia kupoteza mwelekeo huku mtaani, hakuna mzazi makini wakumpa malezi bora mwanae.
 
Kuna Watanzania wanapenda sana kulalamika. Wakati walimu wanapambana kuhakikisha watoto wao wanafaulu kwa kuwabakisha wakati wa likizo ili wajisomee! Wao wanalalamika warudi nyumbani.

Halafu wakirudi nyumbani kwenyewe, hawasimamii nidhamu na mienendo yao ya kila siku, likiwemo zoezi la kujisomea, na baada ya likizo, watoto hao hurejea shuleni huku kichwani wakiwa ni empty heads na wakifeli mitihani yao ya mwisho, utawakuta hao wazazi wanaanza tena kuwalalamikia walimu walewale tena, eti kwa kufelisha watoto wao!

Hovyo kabisa. Binafsi naunga mkono shule mbalimbali nchini kubakiza madarasa ya mitihani, ili kujisomea na kujiandaa kwa mitihani yao.
 
Ahsante mkuu kwa kuleta hii mada. Isitoshe hao watu watoto wao wanasomea shule zenya kutoa au kua na mazingira bora ya kujisomea na kujifunzia.

Wanawadanganya wananchi walio hoi katika ili. Kwanza huyu Waziri na Kamishna ilibidi watumbuliwe
 
Watoto waende nyumbani kupumzika na kuwasaidia kazi wazazi wao. Muda wa kupumzika uheshimiwe.
Mashamba yenyewe Serekali mmesha tunyanganya na kuwapa wawekezaji, Sasa vijana watakuja Nyumbani kutusaidia kazi gani tena!? Au mnataka watusaidie kuendesha Bodaboda zetu!!? Mi naona bora wabaki tu huko huko shule!!
 
kama Mimi nilisoma saint kayumba na nikafaulu vizuri na Kila likizo nilikua naludi nyumbani sihitaji mtoto wangu abaki shule likizo. Hawa watoto wanaoshinda boarding tutajenga nao bond lini sisi wazazi. tumeweka ufaulu mbele sana. Kuna maisha baada ya A za darasani.
 
Mpaka sasa wapo majumbani hao watoto kwa wazazi wanaotoka asubuhi kurudi usiku, mtoto anashinda na beki 3, sijui mtawasimamia muda gani hao watoto. Wakati tunasoma vidato vya mitihani tulibaki shule lakini sasa mnawasikikiza wanasiasa na kuwapangia elimu ya watoto wenu. MUDA UTAONGEA
 
Wazazi Mwanao Kama yupo form four , Aendelee kusoma na kujisomea haya matamko ya wana-siasa ni matamko ya kisiasa.


We Mwanao yupo shule ya kata, na unajua kuwa ili aweze Kupata nafasi ya kwenda hata VETA au kuongeza ujuzi wowote Basi cheti Cha Form four lazima .


So akili kichwani yaani Mzazi unakaa na kusubiri future ya Mwanao ambaye yupo shule ya kata waziri amuandalie future kid.


Mwanao akipata zero hata upolisi hawamchukui na huko mtaani kizazi Cha singeli hiki , pathetic

Nimeandika maana nipo uswahilini dsm nimeona watoto wa kike na kiume wakikaa mtaani wanaishia kupoteza mwelekeo huku mtaani hakuna Mzazi makini wakumpa malezi Bora mwanae.
Mapumziko pia ni muhimu
 
Mpaka sasa wapo majumbani hao watoto kwa wazazi wanaotoka asubuhi kurudi usiku, mtoto anashinda na beki 3, sijui mtawasimamia muda gani hao watoto. Wakati tunasoma vidato vya mitihani tulibaki shule lakini sasa mnawasikikiza wanasiasa na kuwapangia elimu ya watoto wenu. MUDA UTAONGEA
Mkuu sisi enzi zetu ikifika lilizo tulikuwa tunaruhusiwa kwenda nyumbani lakini tulifaulu masomo vizuri. Walimu hakikisheni mnakwenda na syllubus vizuri na kwa wakati! Lakini kwa habari ya Afya watoto waruhusiwe kupumuzika.
 
Mpaka sasa wapo majumbani hao watoto kwa wazazi wanaotoka asubuhi kurudi usiku, mtoto anashinda na beki 3, sijui mtawasimamia muda gani hao watoto. Wakati tunasoma vidato vya mitihani tulibaki shule lakini sasa mnawasikikiza wanasiasa na kuwapangia elimu ya watoto wenu. MUDA UTAONGEA
Mapumziko ni muhimu acheni complications nyingi kama toto lako ni jinga ni jinga tu

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom