Wanafunzi wote waache shule na vyuo: Ushauri wa tahadhari

BICHWA KOMWE -

JF-Expert Member
Jul 21, 2022
4,696
10,225
Hii ni tahadhari nawapa, kwa wazazi na wanafunzi kwa ujumla.

Ewe mzazi, usipoteze mamilioni kusomesha mtoto wako kwa uchungu na kwa jasho halafu akarudi nyumbani kukaanga chips na kuendesha bajaji.

Ewe mzazi, usiuze ng'ombe zako, usiuze ardhi yako, usifilisi biashara zako kwa ajili ya kupeleka hela shuleni. Unapoteza muda na fedha nyingi, utashangazwa mwanao atarudi nyumbani na makaratasi matupu akaanze kuendesha bodaboda na kuuza mwili wake kwenye madanguro.

Ewe mwanafunzi, usipoteza muda wako wa miaka zaidi ya ishirini unahangaika kusoma kwa tabu na uchungu mkubwa, utashangazwa. Utarudi mtaani kuwa boda boda.

Ewe mwanafunzi, kama uko shule achana nayo, kimbia haraka kaanze kujihangaikia.

Ewe mwanachuo, achana na habari hizo, ondoka hapo unapoteza muda. Unapoteza fedha nyingi kwenye sifuri.

Changamka. Ubodaboda hauhitaji digrii au cheti cha form four.

Achana na hiyo shule, anza sasa hivi kujifunza bodaboda utanishukuru. Usisubiri mpaka miaka 10 ijayo ukiwa umechoka na umeshapoteza fedha nyingi kwenye hamna.

Wenye masikio na wasikie. Wazazi amkeni. Shule ni ujinga.
 
Uharo mtupu
 
Wengi hawawezi kukuelewa ila ulichokiandika hapa kina ukweli. Kwa hapa tz elimu inatupotezea muda tu, haituandai kukabiliana na maisha halisi. Kwa upande wangu naona elimu ya form 4 inatosha sana.

Kama mtu atasoma vizuri, ajifunze kiingereza cha kuongea na kuandika, ujanja wa technojia. Kisha aje mtaani aanze kujifunza life skills na namna watu wanavyojipatia rizki kwa njia mbali mbali.

Hapo akiongezea na elimu yake aliyopata basi atakuwa na asilimia kubwa ya kufanikiwa kimaisha.
 
Wote wakifuata mtazamo wako,miaka 30 baadaye nani atakuwa daktari,mhandisi,mwanasheria,mwalimu n.k ?
 
Mimi niliacha shule kutokana na matatizo ya nyumbani. Miaka 5 sasa nasema ilikuwa mpango wa Mungu mimi kuacha shule.

Nikiangalia niliowaacha shule baada ya kurudi mtaani hata kupanga chumba cha elf 30 hawezi wala kununua simu ya 150,000?

Nasema mimi haya maumivu yangeniuwa kwakweli, lakini nimegeuka msaada kwa jamaa zangu ambao wametoka chuo. Nakaa nao getto wakijipata wanasepa.

Kwenda chuo na Hizi shule sio kubaya kama mwandishi alivyoandika.

Mimi nasema hivi soma au nenda chuo kwa kujua au kuwa na uhakika wa investment yako.

Kama utasomea mambo ya Transportation na baadae uje uanzishe company ya usafiri itakuwa unyama sana.

Soma ukijua utafanyia nini hicho ulichosomea. Sio habari za mimi mshahara sitaki chini ya laki 5.

Utapata laki 7 na utakuwa masikini kuliko hata umasikini wenyewe.

Tatizo la kipindi ukiwa shule unakuwa huna uwezo wa kuelewa mambo.
Mfano shule zinakupa mwanga na matarajio mazuri sana baada ya elimu yako.

Jambo ambalo huenda kuangamia kwako kukasababishwa na elimu au vyeti ulivyopata.

Unamaliza chuo ukiwa na miaka 26 alaf nyumbani hakueleweki aisee hiyo miaka ni mingi sana kwenye kuanza kupambana.

Utakata tamaa tu! Labda Mungu awe upande wako.

Mtaani kuna kujifunza mengi sana kuliko shuleni.

Ndio maana wasio soma ndio wanarun business kubwa hapa Kkoo.

Sababu ni wao wanawekeza kwenye elimu ya mtaani na wewe kwenye elimu ya mikataba na Berlin
 
Wengi hawawezi kukuelewa ila ulichokiandika hapa kina ukweli. Kwa hapa tz elimu inatupotezea muda tu, haituandai kukabiliana na maisha halisi. Kwa upande wangu naona elimu ya form 4 inatosha sana.

Kama mtu atasoma vizuri, ajifunze kiingereza cha kuongea na kuandika, ujanja wa technojia. Kisha aje mtaani aanze kujifunza life skills na namna watu wanavyojipatia rizki kwa njia mbali mbali.

Hapo akiongezea na elimu yake aliyopata basi atakuwa na asilimia kubwa ya kufanikiwa kimaisha.
Mtu kama huyu unakuta kampeleka mtoto wake shule. Anmnunulia vitabu, na anamtolea hela ya tuition.

Za kuambiwa changanya na zako.
 
Haya mambo sio common inategemea.

Binafsi. Nimemaliza Chuo 2022.

Sijafanikiwa kivile. Ila sijawai piga simu nyumbani kuomba hela ya Kula, kodi wala Matibabu. Nahangaika kupitia elimu niliyo ipata nikiwa shule.

Kwangu mimi hii hatua ni bora zaidi kuliko miaka 5 iliopita nikiwa bado sijaenda chuo, na bado niko future ninayo ipambania.

Hivyo mtoa mada usipotoshe jamii. Mafanikio ni kitendawili kwa tulio kwenda shule na ambao hawakwenda shule.

Kuna classmate wangu walio ishia darasa la saba/Form 4 Wakaingia mtaani kutafuta maisha leo hii hawana wanacho nizidi zaidi ya mke na watoto, na nikiangalia 5 years kama mambo yataenda hivi hawawezi nikuta.

Ushauri wangu. Watu waende shule ila kwa uangalifu wa vitu vya kusomea. Soma vitu ambavyo ni tangible skills katika jamii mfano.

1.Kujenga nyumba/Kuchora ramani
2.Ufundi wa magari/Umeme/
3.Kushona nguo
4.Kutibu watu/Mifugo
5.N.k
 
Back
Top Bottom