Kilimanjaro: Baada ya Shule kuandikisha Wanafunzi Watatu tu, Serikali yaanzisha msako kutafuta Watoto waliopo mtaani

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Siku chache baada ya JamiiForums kuripoti juu ya Shule ya Msingi ya Mlembea Wilayani Rombo kuandikisha Wanafunzi Watatu pekee wa Darasa la Kwanza, baadhi ya Wananchi wamedai moja ya changamoto inayosababisha hali hiyo ni uongozi wa Shule.

Mwananchi mmoja amesema “Watoto wangu wawili wamesoma hapo, nimelipa hela ya chakula lakini unakuta wanakula miezi miwili tu, pia kuna matumizi mabaya ya fedha lakini kwa Mwaka huu hakuna Watoto wengi wameenda sehemu nyingine kusoma.”

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Raymond Stephen Mwangwala amesema “Tunatoa wito kwa Wazazi na walezi ambao hawajaleta Watoto shuleni wana siku chache za kufanya hivyo.

“Kwa sasa kazi inayoendelea ni viongozi wa Serikali kuanzia ngazi ya Vitongoji, Tarafa, Kata, Waratibu wa Elimu na Maafisa Tarafa kuhakikisha wanatembea vitongoji vyote kuhakikisha Watoto wote wanaostahili wanapelekwa shule.

“Endapo kutakuwa na yeyote anayezuia Mtoto kwenda shule kwa makusudi atambue kuwa kusoma ni haki ya msingi ya Mtoto.

“Nitoe wito kwa Wazazi na viongozi, yeyote atakayeona mtoto anazagaa mtaani wakati wa shule atoe taarifa kwa mamlaka.

Pia soma:
- Kilimanjaro: Shule ya Msingi ya Serikali yaandikisha Wanafunzi watatu (3) kuanza Darasa la Kwanza

- Mkurugenzi Rombo: Shule iliyoandikisha Wanafunzi Watatu hakuna imani za kishirikina ni maamuzi ya wazazi tu
 
Waacheni watoto hao
Hao wote wanataka kuwa
Wasanii kama wakina mondi misomisondo konde zuchu
Baba level mwijak ,wamewa inspire

Ova
 
Wanawaimiza watoto waende shule wasipopelekwa ndani vip wakimaliza kuosoma wanawandalia nin kama selikali Kwan kuwaimiza uko unamaliza shule vyeti kama vyote ya kuhitimu vyuo na bado unakosa kazi sas sibola wanyamaze
 
Back
Top Bottom