DOKEZO Kuna Walimu wa Shule ya Sekondari wanaharibu maisha ya Wanafunzi wa kike Kilwa (Lindi)

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Asee kuna hili jambo linanikera sana na lina Waharibia Wanafunzi future yao.

Nikiwa Mdau muhimu wa Elimu naumia sana kuona Waalimu wa kiume kukatisha ndoto za mabinti kwa kukuanzisha uhusiano nao na kisha kuwapa ujauzito na wengine ndoto zao kuisha kabisa.

Wapo Wanafunzi kadhaa walifaulu kwenda kidato cha tano na chuo ila wameshindwa kuendelea kisa Waalimu wamewapatia ujauzito.

Waalimu wakike wamepaza sauti sana ila imekuwa kama nyimbo tu sasa, mbaya zaidi jamii inashindwa kuwashtaki wakihofia vijana wao kukosa matunzo.

Wapo Waalimu Watatu wa kiume kazi yao kubwa ni hiyo katika Shule ya Sekondari ambayo ipo Kata ya Kivinje, Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi

Kuweka rekodi sawa, aliwahi kupita Godfrey Zambi alipokuwa Mkuu wa Mkoa, akasema miongoni mwa hao Waalimu watolewe ila hawakutolewa baada ya yeye kuondoka.

Hilo limekuwa tatizo na ajira imekuwa kama kuwatia jeuri kwao, naomba jamii isaidie kupaza sauti, Watoto hawa huwenda wakanusurika na kinachoendelea.

Hakika jambo linaumiza ingawa wanasema Watoto wa Kusini hawapendi shule ila Waalimu nasi tunachangia Wanafunzi hao kutokupenda shule na kuzima ndoto zao.
 
Unashindwaje kutaja majina yao hapa? Yataje, uko salama, usipoyataja unabakia kuwa Umbea, we taja (kama ni kweli wanafanya hayo) week haitaisha utasikia.
 
Serikali lazima ijipambanue juu ya kuwawajibisha watumishi wanaoenda kinyume na matakwa na watumishi kama hawa walimu wanaoanzisha mahusiano na wanafunzi wao wawajibishwe na kukemewa vikali sana pia maonyo makali yatolewe kwa watumishi wanaovunja taratibu za serikali.
 
Mtoa uzi nawewe ni wale wale ulipaswa uwataje kwa majina yao matatu hao waalimu ikiambana na location wanapoishi ili wakafirimbiwe kizarendo Zaidi. wazazi tuna hasira sana
 
Walimu tuna shida sehemu,chuki ,wivu husuda,utakuta mtoa hoja anapambania vyeo shuleni na hao anaowatuhumu
Nimekaa Kilwa Kivinje na Kilwa Masoko, anachosema mdau ni kweli kabisa. Miaka hiyo ilikuwa walimu wazee wakikukanya ukaendelea kujifanya kidume hawakawiii kukushusha bonge la busha. Kuna kisa cha Mwalimu mmoja alikuwa anajifanya kijogoo mpaka kwa wake za watu, maana huko wazee wanaoa vibinti vibichiii, basi huyo mwalimu siku moja kaamka asubuhi mdomoni hakuna jino hata moja, kawa kibogoyo, ilikuwa kijiji cha Mchakama kama sikosei maana ni muda mrefu kidogo.
 
Dogo acha ukuda..... Wamebanduana wenyewe wewe inakuhusu Nini?

Wazaz hawalakamiki na agizo la mkuu wa mkoa likionekana halina uhalali.

Utaolewa, punguza shobo
Acha kudinya wanafunzi wewe, kuna siku binti yako naye yatamkuta ndiyo akili itakurudi..
 
Huu ni umbea, mtoa madam angetaja shule, walimu, na mifano ya wanafunzi walioachishwa masono.
Asa wenye mamlaka watashughulikaje na hii stori ya kilabuni.
 
Mkumbuke walimu nao ni binadamu wana hisia kama binadamu wa kiume vitoto vya sasa akili zao ni za porn yani kujilengesha na vitabia vya ukahaba na kuvaa vinguo vya ajabu hasa wakati wa mazoezi na kazi za ziada.

Siwatetei waalimu kwa tabia za kishenzi ila siwahukumu kwa kupambania hisia zao
 
Huna hoja zaidi unaleta speculation kitu ambacho sio sawa. Kama unania njema taja Mwl. Kampa mimba mwanafunzi jina na kidato.
Hoja yako ni mfu mambo ya siasa tena miaka kadhaa unayaleta leo acha umaamuma. Hiyo kata inazo shule tatu za sekondari ni ipi miongoni mwao lete na majina ya wahusika turuke na wewe.
 
Back
Top Bottom