Shule ambazo mtoto anashinda siku nzima shuleni kama watu wazima kazini ni hatari kwa future ya mtoto zama hizi

FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
8,822
33,527
Shule ambazo mtoto anaenda asubuhi na anarudi jioni saa 11 ama saa 12 jioni sio nzuri kwa future ya mtoto.

Mtoto anapaswa atoke shuleni mapema. Ili awe na muda wa kujifunza skills za mtaani

Siku ya mtoto haipaswi kuishia kujifunza ya shuleni tu, anapaswa apate muda wa kujifunza extracurricular skills Mtoto acheze mpira na watoto wenzake mtaani nje ya shuleni .,

mtoto apate muda wa kujifunza kuimba iwe kwaya kanisani ya watoto ama kujifunza kupiga vyombo vya muziki kama kinanda, saxophone, drums etc, mtoto apate muda wa kujifunza kuigiza mtaani,

kama kuna waigizaji unaishi nao jirani waombe ama walipe wawafundishe wanao kuigiza mapema.

Mtoto ajifunze kupika, kupamba, kuongea mbele za watu wengi. Hivi vitu vitamsaidia kuliko masomo ya shuleni .

Jiulize why International school of Tanganyika watoto wanatoka saa saba tu mchana?

Jiulize why nchi zilizoendelea shule zao watoto wanatoka shuleni mapema?

UKWELI MCHUNGU ZAMA HIZI MAISHA YAMEBADILIKA SANA. ELIMU HAITAMSAIDIA MTOTO WAKO KWENYE FURSA ZA KIMAISHA KAMA HAJUI VITU KAMA NILIVYOVITAJA NA VINGINE VINGI
 
Nchi hizo akitoka mapema ni kama mzazi wake kamaliza kazi mapema kamfata.
Mbinde iko palepale wanatoka sa 11 jioni,kumi na moja kama Africa.
Baba anatafuta hela mama pia,,
Na ukimtia mimba mwanamke ,mwanaume una martenity leave na mke yakwake.
Mwanamke atakaa nyumbani 6 month ananyonyesha.
Badae mwanaume 6 month pia ulee mwanao
 
Huu ujinga nishaukataa na nikamwambia mpaka mkuu wa shule mwanangu atafutwa shule saa nane kamili, likizo ni mda wa mtoto kupumzika, siitaji sijui batch za maswali sijui nini likizo nikucheza na wenzie kusafiri ni, siitaji ssijui tuition mtoto siitaji

Mda wakussoma ukifika atadoma na tamkazia kweli kweli ajue baba yupo seriously siyo hizi drama za ajabu ajabu
 
Na yale Mambo ya sijui kubariki au kuyatakatifuza, mwende mkayaangalie kuhusu watoto wenu wa kushinda sana boarding school.

Hasa hizo boarding za wamishenari.
 
Shule ambazo mtoto anaenda asubuhi na anarudi jioni saa 11 ama saa 12 jioni sio nzuri kwa future ya mtoto.

Mtoto anapaswa atoke shuleni mapema. Ili awe na muda wa kujifunza skills za mtaani

Siku ya mtoto haipaswi kuishia kujifunza ya shuleni tu, anapaswa apate muda wa kujifunza extracurricular skills Mtoto acheze mpira na watoto wenzake mtaani nje ya shuleni .,

mtoto apate muda wa kujifunza kuimba iwe kwaya kanisani ya watoto ama kujifunza kupiga vyombo vya muziki kama kinanda, saxophone, drums etc, mtoto apate muda wa kujifunza kuigiza mtaani,

kama kuna waigizaji unaishi nao jirani waombe ama walipe wawafundishe wanao kuigiza mapema.

Mtoto ajifunze kupika, kupamba, kuongea mbele za watu wengi. Hivi vitu vitamsaidia kuliko masomo ya shuleni .

Jiulize why International school of Tanganyika watoto wanatoka saa saba tu mchana?

Jiulize why nchi zilizoendelea shule zao watoto wanatoka shuleni mapema?

UKWELI MCHUNGU ZAMA HIZI MAISHA YAMEBADILIKA SANA. ELIMU HAITAMSAIDIA MTOTO WAKO KWENYE FURSA ZA KIMAISHA KAMA HAJUI VITU KAMA NILIVYOVITAJA NA VINGINE VINGI
Yaani huwa kila siku nasema , ningekuwa na mtoto anasoma ningegombana sana na walimu kuhusu tuition za jioni na weekend za hapa DSM.

Haiwezekani mwanafunzi wa primary awe busy kuliko hata wanachuo
 
Mtoto anaamshwa saa 11 alfajiri kujiandaa kwenda shule. Kurudi saa 12:30 jioni n ujinga sana kwa wazazi.
Kuna baadhi ya shule mtoto jtatu hadi jmosi shule.
Wanachoka mno kwa kweli....maana hata likizo ndefu kama hii bado wapo tuition siku nzima.
 
Back
Top Bottom