Ngoja mtoto wako afike adolescent age (foolish age) ndio utaukumbuka umuhimu wa shule za Kayumba

LIKUD

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
15,118
27,122
Biblia inasema Mungu aliwapenda sana wana Isachar ( sio Isaka ni ISACHAR: Huyu Isachar alikuwa ni kati ya watoto 12 wa Yakobo. Sasa huyu Isachar alikuwa na watoto wa kiume 200 ndio hao ambao ninawazungumzia.

Biblia inasema Mungu alipendezwa sana na wana wa Isachar.

Sababu kuu iliyo mfanya Mungu apendezwe na wana Isachar utaikuta kwenye kitabu cha 1 Chronicles 12:32.

They knew what Israel had to do and at what time and how to do it.

Kwa ufupi hawa wana wa Isachar walikuwa ni majasusi.

JASUSI ni mtu anae jua kitu gani kinatakiwa kufanywa na wakati gani na kwa namna gani.

JASUSI anajua yote hayo sio kwa kupitia uchawi bali ni kupitia sanaa ya kutafuta na kuku sanya taarifa (the art of intelligence gathering) kuchakata taarifa (the art of intelligence processing) kuandika ripoti ya kitaalamu kupitia taarifa zilizo kusanywa na kuchakatwa ( the art of intelligence report) na kuifanyia kazi ripoti hiyo (the art of intelligence execution) .

Kikubwa zaidi ni kujua wakati gani muafaka wa ku -execute hizo taarifa.

Wana wa Isachar walikuwa ndio the brain behind King David's victory in all wars and battles which he fought.


Kwa wasio jua, His Majesty King David, the King of the United Kingdoms of Israel and Judah, ndio mfalme ambae hajawahi kushindwa vita yoyote ile katika utawala wake. Huduma ya ujasusi kutoka kwa wana wa Isachar ilikuwa ni sababu kuu mfalme Daud alishinda vita zake zote.

Mfalme Daudi alikuwa na intelligence madhubuti sana. (Nenda kasome kitabu " Rise and Kill First: The secret history of Israel's Targetted Assasinations " kilicho andikwa na Investigative Journalist na JASUSI wa kiyahudi aitwae Ronen Bergman ili uweze kujua wana wa Isachar ni watu wa namna gani katika dunia ya sasa)


The reason why King David acted strangely during Absalom Rebellion was because of the advice he was given by the children of Isachar. At the end of the day King David secured the victory without even putting a fight. All this ni kwa sababu ya kuzungukwa na wabobezi wa ujasusi.

Binafsi tangu nifahamu kuhusu siri hii ya wana wa Isachar nimekuwa nikiitumia hadi kwenye vitu vya kawaida kabisa kwenye maisha yangu.

Hata michepuko wangu huwa nawafanyia ujasusi kabla ya kuwapa " zawadi" ya kuwa nao kimapenzi. Kila mwanamke ana file na dawati lake. Mfano " Fatuma's desk" ( Dawati la Fatuma: dawati maalumu la ku dili na masuala yote yanayo muhusu Fatuma. Humo kuna mafaili yenye taarifa zote kuhusu Fatuma plus what when and how to act when dealing with Fatuma). The same to my children. Kila mtoto ana dawati lake.


BACK to my topic . Wazazi wengi wa miaka hii ya elfu 2 ambao ndio kina sisi tulio zaliwa miaka ya themanini katikati na mwishoni ( themanini mwanzoni na 70 mwishoni) plus miaka ya tisini mwanzoni, kwenye mindset zetu hatunaga image ya mtoto ambae yupo kwenye adolescent age ( teen age / foolish age) When it comes to children, wengi wetu huwaga tuna picha ya yule mtoto wa mwaka 0 mpaka 9 au 12 n.a. 13 hapo. Mtoto ambae bado ni mtiifu kwa almost kila kitu. Mtoto anaeweza kudhibitiwa hata kwa fimbo etc.

Wengi wetu huwaga hatujiandai kisaikojia kukabiliana na changamoto za mtoto alie balehe. Huwaga tunadhani mtoto ataendelea kuwa " Mtoto " hivyo hivyo maisha yake yote..

Utamsikia mtu anasema " namlipia mamilioni mtoto wangu shule hii ya English Medium kwa sababu hapa wanafaulisha vizuri. So nataka afaulu vizuri hapa then aende O level then A level then Chuo the apate kazi yake nzuri"

Mawazo kama hayo 👆 anasema Robert Kiyosaki kwenye kitabu " Poor Dad Rich Dad " yalikuwa valid kuanzia mwaka 1985 kushuka chini and not after that. Sasa hivi dunia imebadilika ( kumbuka hiyo ilikuwa mwaka 97 mzee ) Sasa hivi ni 2023 dunia imebadilika zaidi. Mfumo wa maisha ya dunia ya sasa umebadilika juu chini kama ulivyo badilika pale Eden baada ya Adam na Hawa Kula tunda la mti ule ulio katazwa...

Wakati wewe mzazi unahangaika kulipa mamilioni ili mtoto wako awe injinia, mwanasheria au daktari kumbe mwenzako anawaza kufanya kitu tofauti kabisa na wewe. Anataka kuwa kama Mzize, Zuchu au Gigy Money

Ndo maana nasema no matter how much money u put on ur children when they are young, when they grow up they will branch out.

Kwa wewe mzazi ambae una watoto wadogo ambao ni watiifu kwako at this moment fanya yote unayo fanya lakini jua kwamba wakifika adolescent age wata branch out. Watakuwa tofauti kabisa na unavyo tarajia..


Mimi namshukuru Mungu nimeujua huu ukweli tangu nikiwa mdogo kwa sababu Nimepata watoto nikiwa mtoto.

Nimesex ( kikubwa kubwa achilia zile za utotoni za kufanya kinguo nguo au kichupi chupi) kwa mara ya kwanza tareje 18 November 2000 nikiwa kidato cha pili najiandaa kuingia form three. I was 15 years old and she was 15 years old too. Tuliendelea na kamchezo Ketu mpaka demu akapata ujauzito nikapata mtoto wa kwanza wa kike nikiwa nna miaka.16 ( 2001) ( kumbuka jambo hili ni kinyume kabisa na maadili ya familia yetu Nimetoka kwenye familia inayo swali)

Mwaka 2003 nikiwa nna miaka 18 nikapata mtoto mwingine wa kike kwa mwanamke mwingine.

Hawa wote walisoma Kayumba.

Mwaka 2007 nikapata mtoto mwingine wa kike kwa mwanamke mwingine. Huyu alinikuta tayari nna vihela hela nikampeleka English Medium kuanzia la kwanza hadi la saba. N.a. private school kuanzia form one hadi form four.

2015 n.a. 17 nikapata watoto wawili wa kiume kwa mwanamke mmoja.


Huyu wa 2001 now yupo chuo mwaka wa mwisho ( she is very smart and very disciplined. )

Huyu wa 2003 yupo Chuo mwaka wa kwanza. She is very smart and very disciplined ( wote hawa wamesoma kayumba kuanzia la kwanza hadi form six )

Huyu wa 2007 yupo form four. Amesoma private kuanzia chekechea hadi form four. She is very smart darasani but kuhusu discipline nisiseme uongo. Ana leta uzungu mwingi. ( anajionaga kama.yupo na kina Ticha Thomas muda wote ) Kwake yeye uzungu ndio ujanja. I was so much dis appointed with her nilipomuuliza anataka kuja kuwa nani akaniambia she want to be a soldier. Duh yani Mimi nahangaika kulipa mamilioni ya hela halafu unakuja kuniambia unataka kuwa mwanajeshi? Hiyo hela si bora ningeenda kutoa single kwa .master Jay nikakusomesha Kayumba? ( ningejua ange kuja kuwa na wazo kama.hili aisee Kayumba ingemfaa sana kuanzia std 1 . Ila nashukuru Mungu huyu dogo amenisanua)

Hawa wawili niliwarudisha Kayumba mmoja akiwa la tatu na mwenzake akiwa la kwanza now mmoja yupo la nne na mwenzake la pili ( I am so much pleased na namna walivyo na discipline )

Namshukuru Mungu nimestuka mapema.

Mimi Nina afadhali, kuna jamaa zangu ambao wamekuwa dis appointed big time.

1. Kuna huyu brother ( was born in early 80s) a very smart dude . Darasani alikuwa anafanya vizuri sana. Mtoto wake wa kwanza wa kiume kamlipia private kuanzia chekechea hadi form four. He was paying almost 4 million per year ( hiyo ada 2 ukijumlisha na makorokoro mengine inafika almost 7 million)( hiyo chekechea na Primary)
Secondary kampeleka Alpha. Dogo kamaliza form four kapata one Kali. Ila kagoma kwenda form six. Anataka kwenda chuo. Now anasoma CBE. Kozi anayo isoma sasa? Procurement ina nafuu.

Baba mtu amechanganyikiwa amekuwa dis appointed watoto wake wengine wote kawarudisha Kayumba ( mmoja class 5, mwingine glass 2) na.mwingine form 3. Hataki tena kusikia habari za kulipa mamilioni kusomesha mtoto.


Huyu ana ahueni kuna dada mmoja mlokole best yangu, ni single mother , kamsomesha mtoto wake wa kiume shule za private kuanzia chekechea hadi form four . Dogo kapata one form form four ila anataka kusoma chuo. Kozi anayoitaka sasa!!! Anataka driving.

Mama kamshauri Mwanae hadi kachoka kaita wachungaji na walimu wamshauri ila dogo msimamo wake uko palepale.

Mwisho wa siku kanitafuta nimpe ushauri Mwanae asome chuo gani nikashauri asome Veta akisha pata leseni ya udereva aende pale NIT asome Defensive Driving plus other driving courses. ( nilishauri hivi ili at least mama mtu apate faraja aone mwanae anasoma kitu cha kueleweka) Now dogo yupo Veta, mama.mtu anasema mtoto wake amerogwa...

Kama.uwezo wako ni mdogo usijibane kumsomesha mtoto wako English Medium kwa matarajio kwamba eti atakuja kuwa vile unavyo tarajia wewe nope. English Medium waachie wenye uwezo mkubwa wa kifedha ambao kwao hiyo milioni 7 kwa mwaka sio pesa ya mawazo.

Wewe mwenye pesa ya mawazo bora umsomeshe Kayumba mwanao halafu pesa itumike kufanya mambo mengine ya maana.

Zile zama za eti kulala chini ili mtoto asome hazipo tena.Gone are those days!!
Usije kuishia kumpa mwanao radhi bure. Wewe unataka awe injinia kama Hersi kumbe mwenzako anataka kuwa kama Konde Boy.


Ni Mimi Likud wa JF..

Rais wa,
BACK TO KAYUMBA SCHOOLS CAMPAIGN

motto : MAKING KAYUMBA SCHOOLS GREAT AGAIN CAMPAIGN
 
Biblia inasema Mungu aliwapenda sana wana Isachar ( sio Isaka ni ISACHAR: Huyu Isachar alikuwa ni kati ya watoto 12 wa Yakobo. Sasa huyu Isachar alikuwa na watoto wa kiume 200 ndio hao ambao ninawazungumzia. Biblia inasema Mungu alipendezwa sana na wana Isachar. Sababu kuu iliyo mfanya Mungu apendezwe na wana Isachar utaikuta kwenye kitabu
Kayumba ni shule za wale wasio kua na plan B, wenye abject povert,....... wanao toboa maisha kupitia elimu wengi hutokea shule za magari ya njano, kijiji chetu tulio maliza darasa la saba tulikua 105, tulio weza kufika dar es salam na kuendekea na elimu ya juu tuko wa wili tu, kijiji kizima kina tutetegemea sisi mwaka uliofuatia hamna alio toboa, mwenzangu alisoma dip in electronics, mimi ndo nilio toboa zaidi.........

Wengi ni boda boda, wakulima, vibarua, mama wanyumbani, wengine walisha kufa n.k.......elimu ya kayumba is harzadius au massacre kwa future za watoto wa kitanzania, mpaka pale ccm itakapo kua na utashi wa kuboresha elimu ya nchi hi, mimi sitakuja kumpeleka mwanangu shule hizo hiyo ni 'ecademic suicide'.
 
Kayumba ni shule za wale wasio kua na plan B, wanao toboa maisha kupitia elimu wengi hutokea shule za magari ya njano, kijiji chetu tulio maliza darasa la saba 105, ilio weza kufika dar es salam tuko wa wa wili tu, kijiji kuzima kina tutegemea mwenzangu alisoma dip in electronics, mimi ndo nilio toboa tu zaidi.........wengi ni boda boda wakulima vibarua mama wsnyumbani n.k.......elimu ya kayumba is harzadius au massacre kwa future ya watoto wa kitanzania, mpaka pale ccm itakapo kua na utashi kuboresha elimu ya nchi, mimi sitakuja kumpeleka mwanangu shuke hizo hiyo ni 'ecademic suicide'
Mkuu kwa hiyo kufika Dar ndio kutoboa kimaisha?
 
Biblia inasema Mungu aliwapenda sana wana Isachar ( sio Isaka ni ISACHAR: Huyu Isachar alikuwa ni kati ya watoto 12 wa Yakobo. Sasa huyu Isachar alikuwa na watoto wa kiume 200 ndio hao ambao ninawazungumzia. Biblia inasema Mungu

motto : MAKING KAYUMBA SCHOOLS GREAT AGAIN CAMPAIGN
Elimu ya Tanzania kwa ujumla ni mbovu acha kujidanganya.
 
Biblia inasema Mungu aliwapenda sana wana Isachar ( sio Isaka ni ISACHAR: Huyu Isachar alikuwa ni kati ya watoto 12 wa Yakobo. Sasa huyu Isachar alikuwa na watoto wa kiume 200 ndio hao ambao ninawazungumzia. Biblia inasema Mungu alipendezwa sana na wana Isachar. Sababu kuu iliyo mfanya Mungu apendezwe na wana Isachar utaikuta kwenye kitabu cha 1 Chronicles 12:32.

They knew what Israel had to do and at what time and how to do it.
]EAT AGAIN CAMPAIGN
Eti mama mtu anasema mtoto wake amerogwa.🤣🤣

Kiufupi inatakiwa kusomesha hizo shule Kwa tahadhari,Mimi nawasomesha hizo hizo.private ila sio zaidi ya mil.1 Kwa gharama zote,sitaki ujinga kabisa.
 
Kayumba ni shule za wale wasio kua na plan B, wenye abject povert,....... wanao toboa maisha kupitia elimu wengi hutokea shule za magari ya njano, kijiji chetu tulio maliza darasa la saba tulikua 105, tulio weza kufika dar es salam na kuendekea na elimu ya juu tuko wa wili tu, kijiji kizima kina tutetegemea sisi mwaka uliofuatia hamna alio toboa, mwenzangu alisoma dip in electronics, mimi ndo nilio toboa zaidi.........wengi ni boda boda, wakulima, vibarua, mama wanyumbani, wengine walisha kufa n.k.......elimu ya kayumba is harzadius au massacre kwa future za watoto wa kitanzania, mpaka pale ccm itakapo kua na utashi wa kuboresha elimu ya nchi hi, mimi sitakuja kumpeleka mwanangu shule hizo hiyo ni 'ecademic suicide'.
Kama hana akili ila kama anazo atafaulu vizuri maana tabia Kwa sehemu kubwa Watoto wanatoa Kwa wazazi
 
Wanafaulisha kisiasa ila wako empty kichwani asikudanganyi mtu, shule za kayumba zinazo jitahidi ni zile kwenye majiji makubwa kama Dar arusha mwanza moro dodoma tena sio zote.
Kayumba mtoto anajua vitu vingi kuhusu maisha ,,,kufagia uwanja ,kupanda maua ,kufanya usafi chooni na darasani ,usafi kuanzia kiatu mpaka mavazi ....maana yote hayo anayafanya mwenyewe Tena Kwa fimbo ....kuelekezwa kidogo na kujitafutia kingiii .......na haya ndio maisha halisi ya Duniani ...

Kutana sasa na Hao st Mary's sijui nin ,uzungu mwingi tu ...mtoto WA kike anajua U nooo ,bikozi ,ze boyifurendi.....kupika haijui ,kufua hajui ,usafi hajui ,hata kufagia uwanja hawezi ....anakuwa boyaaaa boyaaaa ti zobaaaa shittyt kabisa
 
Nimerudia kusoma na kupata utata kidogo hasa hapo ulipo andika kuwa, ulianza kupata watoto ukiwa kidato cha pili (sijui unafundisha nini?)

Nilichogundua ni kuwa ulicho andika ni mtazamo wako sawa na watu wengine wanavyolima kwa kutumia mbolea na wengine hawaamini kabisa kwenye kuweka mbolea....
Au pengine niseme;

Ukipanda basi kutoka Dar hadi kigoma na mwingine akapanda ndege kutoka dar ikapata tatizo kidogo Tabora; hiyo haimaanishi kwamba usafiri wa basi ni mzuri na salama kuliko ndege?

Kimsingi kila mtu ana uhuru wa kufuata mtazamo anao ona ni sahihi zaidi kwake; wewe panda basi na mwingine bajaji na mwingine ndege kwa uwezo wa Mungu wote mtafika wala huna haja ya kushawishi wanaopanda ndege wasafiri kwa basi......
 
Back
Top Bottom