Vontec
JF-Expert Member
- Nov 26, 2020
- 232
- 363
Enyi Mitandao ya simu Tz ebu kueni basi na huruma, hata kama ni shinikizo kutoka serikalini kunyonya tozo vilivyo, Onyesheni basi kutujali sisi wateja wenu
Sio nanyie kuendelea kutubana kwa kuondoa baadhi ya bando, kuongeza bei za bando nk.
Haswa tukiwa tunakimbizana na dunia, kwenda sambamba na spidi ya ukuaji wa sayansi na teknolojia, kuwepo mtandaoni ni muhimu mno kwa ajili ya kuchota maarifa na ujuzi mpya.
Hichi nyie na serikali mnachokifanya mnawapa wakati mgumu sana watanzania aswa wenye nia njema ya kujiinua na kuinua nchi yetu kusogelea level za teknolojia ambazo mataifa makubwa yapo.
Kilichonifanya niandike uzi:
Ni baada ya kusaka vifurushi vya usiku kwa ajili ya ku-update PC yangu jambo ambalo watu wengi uwa tunalikwepa.
ku-update mashine (au Software) zetu ni muhimu mno kwa sababu mara nyingi hujumuisha critical patches to security holes. (kudumisha usalama wa vifaa vyetu), pia kujumuisha vipengee vipya au vilivyoboreshwa, au utangamano bora na vifaa au programu tofauti (enhanced features, or better compatibility with different devices or applications).
Sasa mnapotuondolea na vifurushi vya usiku tuwaeleweje ndugu zetu, mbona mnatufanyia hivyo watanzania wenzenu!?
Nimesaka night bundles za Airtel na Tigo bila mafanikio sijui na mitandao mingine kama bado wana izi bando?