Baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za mawasiliano Tanzania laipongeza Serikali kwa kuondoa tozo ya kutuma miamala ya fedha kidijitali

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Tanzania (TCRA CCC) linaishukuru na kuipongeza Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya ongozi wa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa uamuzi na hatua za kundoa tozo kwenye huduma ya kutuma miamala ya fedha kidijitali.

Kuondolewa kwa too hil kunaendelea kuchochea ukuaji wa matumizi ya fedha kidigitali na kuimarisha usalama wa fedha za watumiaji hususani kupitia simu za mkononi na kuongeza ushiriki wa watanzania katika mfumo jumuishi wa fedha.

Serikali imeondoa too za miamala ya kutuma pesa kwa simu za mkononi, na watumiaji wanatozwa tu pale wanapotoa pesa kwa lengo la kuhamasisha malipo mbalimball kufanvika kwa nia ya kidijitali badala ya fedha taslimu. Matumizi ya fedha kidijitali hurahisisha malipo mbalimbali, kuongeza uwazi, kuweka Kumbukumbu za malipo na salama wa fedha za watumiaji.

Baraza linatambua kwamba mfumo imara a salama wa malipo a miundombinu ya kidijitali ni mojawapo ya nguzo kuu za uchumi wa kidijitali Tanzania ambavyo ni vipaumbele vya serikali katika sekta ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) a katika kuimarisha ustawi wa Watanzania.

Aidha; Baraza linaipongeza Serikali kwa uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa minara mipya 758 katika kata 713 Tanzania Bara na 48 katika shehia 38 Zanzibar na kuongeza wezo na nguvu ya minara 304 katika maeneo mbalimbali nchini. Hatua hii itawezesha watumiaji wa simu za mkononi maeneo ya vijijini kupata huduma za intaneti ya kasi na kuongeza wigo wa watumiaji wa huduma za mawasiliano kunufaika na kushiriki katika mapinduzi ya uchumi wa kidijitali.
Ujenzi na uimarishaji wa mindombinu ya mawasiliano vijijini ni mojawapo ya mikakati ya Serikali kueneza matumizi ya mawasiliano ya kasi kwa wananchi ili kufikia lengo la kuwezesha asilimia 80 ya Watanzania kutumia intaneti ifikapo 2025.

Baraza linatoa wito kwa watumiaji wa huduma za mawasiliano, hasa za fedha kupitia simu za mkononi na mifumo ya kidijitali, kutumia fursa hi ya kuondolewa kwa baadhi ya tozo kufanva miamala kwa uhakika na ufanisi zaidi kwa shughuli zao za kiuchumi, kijamii na kibinafsi.

Baraza linarudia wito wake kwa watumiaji kuwa makini wanapotumia mitandao ya mawasiliano kwa miamala ya kifedha au huduma nyingine kulinda namba zao za siri na kujihadhari na wahalifu. Baraza linapenda kuwakumbusha watumiaji, kutoa taarifa kupitia namba 15040 pindi wanapopata ujumbe wowote wenye kiashiria cha utapeli ili hatua stahiki zichukuliwe dhidi ya wahalifu.

Aidha, linawaomba Watanzania kulinda miundombinu ya mawasiliano a kunga mkono jitihada za Serikall kuifanya Tanzania kuwa ya kidijitali.

Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano lilianzishwa kwa Sheria Na. 12 ya mwaka 2003 ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, kama ilivyorekebishwa mwaka 2017 kama chombo cha kuwakilisha masahi ya Watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano kwa kushauriana na Serikali, Mamlaka ya Mawasiliano, watoa huduma na wadau.

IMG_5762.jpg

IMG_5763.jpg
 
Back
Top Bottom