Hii Mitandao ya simu inatutakia nini wanateknolojia Tanzania?

Vontec

JF-Expert Member
Nov 26, 2020
232
363
Enyi Mitandao ya simu Tz ebu kueni basi na huruma, hata kama ni shinikizo kutoka serikalini kunyonya tozo vilivyo, Onyesheni basi kutujali sisi wateja wenu

Sio nanyie kuendelea kutubana kwa kuondoa baadhi ya bando, kuongeza bei za bando nk.

Haswa tukiwa tunakimbizana na dunia, kwenda sambamba na spidi ya ukuaji wa sayansi na teknolojia, kuwepo mtandaoni ni muhimu mno kwa ajili ya kuchota maarifa na ujuzi mpya.

Hichi nyie na serikali mnachokifanya mnawapa wakati mgumu sana watanzania aswa wenye nia njema ya kujiinua na kuinua nchi yetu kusogelea level za teknolojia ambazo mataifa makubwa yapo.

Kilichonifanya niandike uzi:

Ni baada ya kusaka vifurushi vya usiku kwa ajili ya ku-update PC yangu jambo ambalo watu wengi uwa tunalikwepa.

ku-update mashine (au Software) zetu ni muhimu mno kwa sababu mara nyingi hujumuisha critical patches to security holes. (kudumisha usalama wa vifaa vyetu), pia kujumuisha vipengee vipya au vilivyoboreshwa, au utangamano bora na vifaa au programu tofauti (enhanced features, or better compatibility with different devices or applications).

Sasa mnapotuondolea na vifurushi vya usiku tuwaeleweje ndugu zetu, mbona mnatufanyia hivyo watanzania wenzenu!?

Nimesaka night bundles za Airtel na Tigo bila mafanikio sijui na mitandao mingine kama bado wana izi bando?
 
Naona kuna link kati ya kufunga site zetu zile, na kuondoa bundle za usiku. Mawazo yangu tuu.

Lakini, nimeanza kuona katika maeneo mengi (husasan ninapoishi) nyaya za TTCL wanaanza kuziunga na Fibre; hivyo naamini muda sio muda mitaa mingi ya Dar es Salaam kutakuwa na Fibre to home, na tutaachana na haya maswala ya bundles.
 
Kuna bundles pia mtu alizileta za Ttcl ambazo ni nafuu, walete Fiber mitaani, 25,000 sidhani kama kuna Familia zitashindwa ku Afford ukizingatia Fiber mnaweza kushare familia zaidi ya moja.

Sasa hivi kkoo kuna muitikio mkubwa sana wa zuku, frame kibao watu wanaweka, wanachanga hela wanaweka speed kubwa na kushare internet.
 
Zinaonekana nafuu hizo bei japo naamini wanaweza kuja na package za Fibre zinazolingana na zile za Zuku.

Mwanzo nilikuwa napanga kuweka hawa jamaa: Konnect high-speed satellite Internet | Konnect Africa

Lakini kutokana na habari hii Tanzania: Broadband Connectivity to Reach All Tanzanians nikaona kabla kuingia gharama zote hizo, nisubiri kwanza miezi kadhaa kucheki mipango ya makampuni ya ndani itakuwaje. Huenda chagua nafuu lipo kwenye kona
 
S
Dawa ni kusambaza home internet na kutoa elimu ya faida zake. Mobile data haijakusudiwa kudownload file kubwa kubwa. Hiyo ni kazi ya home wi-fi. Lakini sijui tumekwama wapi.
Tatizo home internet hata dar tu bado haijasambaa kote.
Mfano maeneo ya pembezoni kidogo kama kigamboni.
 
Zinaonekana nafuu hizo bei japo naamini wanaweza kuja na package za Fibre zinazolingana na zile za Zuku.

Mwanzo nilikuwa napanga kuweka hawa jamaa: Konnect high-speed satellite Internet | Konnect Africa

Lakini kutokana na habari hii Tanzania: Broadband Connectivity to Reach All Tanzanians nikaona kabla kuingia gharama zote hizo, nisubiri kwanza miezi kadhaa kucheki mipango ya makampuni ya ndani itakuwaje. Huenda chagua nafuu lipo kwenye kona
Hii konnect kuna mtu anatumia unaemjua? Bei ni rafiki sana kusema kweli, ila information za ping ni muhimu.
 
Hii konnect kuna mtu anatumia unaemjua? Bei ni rafiki sana kusema kweli, ila information za ping ni muhimu.
Ping itakuwa sio nzuri since kwenye YouTube wanakwambia haipo suitable for Video conferences Au online gaming hiyo ndio hasara yake.

Lakini kwenye upande wa mazuri, according kwa nilivyoambiwa - kwanzia saa 4 usiku hadi saa 12 asubuhi data utayotumia haipimwi.
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom