Uncle bright
JF-Expert Member
- Feb 9, 2023
- 1,040
- 4,081
Bei ya vifaa vyote na kuwekewa ni shilingi laki 9.
kifurushi kinadumu kwa mwezi, nadhani anapanga bei kwa kuangalia uchumi wa nchi, Marekani ni 230,000/= , Nigeria ni 98,000, Hapa Kwetu si ajabu ikawa 70,000.
Ni internet ya kisasa, Speed yake ni kubwa sana, unaweza kushusha file la gb 1 speed ikiwa chini dakika 3 na speed ikiwa poa ni sekunde 50 tu, kwenye kuperuzi ni kugusa tu hakuna kusubiri, kucheki video ama video call hakuna mambo ya kuganda ganda.
Haina kikomo, ukitumia hata gb 20 kwa siku ni wewe.
Inaweza kupatikana mpaka mbugani, milimani, kwenye makorongo na sehemu remote ambazo mitandao ya simu haijaweza kufikia, Ni kama vile dstv.
.....................................................................................
ujio wake unaweza kupora wateja wengi wenye matumizi makubwa, hii ni hatari kwa makampuni ya simu na kama mjuavyo kuna watu wana hisa zao huko. Mbaya zaidi kifaa kimoja kinaweza kutumika hata kwa watu 50 kwa mpigo maana speed ni kubwa hata ikigawanywa, ni hatari ukizaliwa utamaduni wa watu kujichanga huku wakiacha kununua mabando,
Kwa kuwa internet ni ya Satelite hapa itaweza kufika hadi maporini na vijijini ambako maeneo hayo mengi internet huwa ni changamoto, hii itakuwa changamoto kwa mitandao ya simu hasa katika miji inayokuwa wakitaka kuweka minara watakuta tayari watu wameshazoea starlink.
..............................................................................
HITIMISHO
Kwa hali hii nadhani naanza kuelewa kwanini vibali vinacheleweshwa, sitashangaa njia ya kumuondosha ikiwa ni tozo nzito sana zitazofanya hata kifurushi kuwa bei sawa na mitandao ya simu, dana dana za kusaini documents kila uchwao au tukaja sikia kisingizio kwamba huduma inaharibu mazingira, ni hatari kwa usalama, n.k.