Gridi ya Taifa yapata hitilafu na kusababisha baadhi ya maeneo kukosa umeme, TANESCO watoa taarifa

Hitilafu ina tafsiri pana, inaweza kutokana na uzembe wa schedule maintance, poor upkeep of infrastructure or unforeseen environmental factors.

Kwa TANESCO hitilafu ni uzembe wa kutunza infrastructure.
 
Enzi za Mkapa na Magu, Gridi ikizima ni sawa na jaribio la kupindua nchi, wahusika wanaenda kujieleza mjengoni!

2024 pekee tu, gridi imechomoka mara ngapi? Wako serious kweli?
  • Hitilafu maana yake ni nini?
  • Nguzo zikianguka, inasemwa, wandhani hatuna akili ya kujua watachosema? Na itokee sasa hata kama wanajua tatizo ni nini!

Ninachojaribu kusema, upumbavu umezidi kukithiri! Kucheza na hatima ya maisha ya watu ndio dili la panya wachache walioko chamani na serikalini!

Huhitaji vyombo vya habari kujua nchi iko gizani, hatukuwa na hii mambo kipindi fulani....mtasema ilikuwa inatokea ila waliogopa kusema?
Huyu wa sasa watu wanamdharau sana. Zile kauli za "kila mmoja ale kwa urefu wa kamba yake" na " najua mnapatapata kwenye maeneo yenu" lakini mnavimbiwa " ziliwapa watu fursa ya kumdharau na tiketi ya hujuma at one's capacity!
 
Kuna mgao sasa wa siku tatu mkoa wa Tanga kila eneo tajwa kwa siku nzima kutoka saa 12 asubuhi mpaka 2 usiku kwa maeneo fulani fulani Mkoa wa Tanga na mengine toka saa 2 usiku mpaka saa 2 asubuhi ..kuanzia tarehe 3 -5 may/2024
 
Kwani mgao uliisha maana? Wengine tumezoa kukatiwa umeme siku nzima. Alhamisi, Jumamosi, Jumapili, Jana tulishinda bila umeme, ukarudi saa mbili usiku. Hatupewi taarifa wala ratiba. Leo tena tunajua tunashinda bila umeme hili la gridi wamesema tu kwa kuwa wanajua umekatika maeneo mengi labda
 
photo_2024-05-04_06-46-40.jpg
HITILAFU KWENYE MFUMO WA GRIDI YA TAIFA

Jumamosi, 04 Mei 2024
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake kuwa kumetokea hitilafu kwenye mfumo wa njia ya kusafirisha umeme ya Gridi ya Taifa kuanzia majira ya saa 8:40 usiku hivyo kusababisha baadhi ya maeneo nchini kukosa huduma ya umeme.

Mpaka sasa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Dodoma na Iringa huduma imeanza kurejea na wataalamu wetu wanaendelea na jitihada za kuhakikisha wanarejesha huduma ya umeme kwenye maeneo yote yaliyobaki nchini.

Shirika linawaomba uvumilivu wateja wake katika kipindi hiki ambacho huduma ya umeme inakosekana

Imetolewa Na;
KURUGENZI YA MAWASILIANO NA UHUSIANO KWA UMMA
TANESCO - MAKAO MAKUU
DODOMA
 
Tayari umerudi alfajiri hii, muwe mnasema nini chanzo cha hitilafu za kukatika kwa umeme. Tulidhani ni kimbunga HIDAYA kimeangusha nguzo!
 
Changamoto kubwa kuliko yote ni kukosa wataalam wa vitendo (maarifa). Tupo vizuri kwenye maneno na maombi (ambayo pia Mungu hasikilizi watu waliokosa maarifa).
Tunazalisha na kuajiri watu wa maneno zaidi.

Ukweli kwamba kwenye taasisi nyingi za Serikali tuna watu wenye maarifa duni.
 
Unazimika unawakaaaaa,,unguzen tu bulb yangu ya tsh 2000
 
Back
Top Bottom