Biteko: TANESCO inanunua umeme wa Megawati 31 kutoka Uganda na Zambia

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,914
4,856
1713968575402.png
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko bungeni jijini Dodoma, wakati akisoma hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Nishati kwa mwaka wa fedha 2024/2025 amesema:

Katika mwaka 2023/24 Serikali iliendelea kuchukua hatua za kuimarisha uzalishaji na upatikanaji wa umeme nchini ambapo hadi kufikia Machi 2024, uwezo wa mitambo ya kufua umeme iliyounganishwa katika mfumo wa Gridi ya Taifa ulifikia jumla ya megawati 2,138 ikiwa ni ongezeko la asilimia 14.2 ikilinganishwa na megawati 1,872.1 za Mei 2023. Katika kiasi hicho megawati 836.3 sawa na asilimia 39.1 ni umeme unaotokana na nguvu ya maji, megawati 1,198.8 sawa na asilimia 56.1 ni gesi asilia, megawati 92.4 sawa na asilimia 4.3 ni mafuta mazito na megawati 10.5 sawa na asilimia 0.5 ni umeme wa tungamotaka (biomass)”- Dkt. Biteko.

Ongezeko la uwezo wa uzalishaji wa umeme limetokana na kuanza kwa uzalishaji wa umeme katika Mradi wa Kuzalisha Umeme wa Julius Nyerere (megawati 2,115) ambapo megawati 235 zimeanza kuzalishwa kupitia mtambo namba 9 pamoja na kukamilika kwa mradi wa kuzalisha umeme wa Rusumo ambao unachangia megawati 26.7 katika Gridi ya Taifa.

Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Machi 2024, uwezo wa mitambo ya kuzalisha umeme ambayo haijaungwa katika Gridi ya Taifa ni megawati 33.4 ambazo zinajumuisha mitambo inayomilikiwa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) yenye uwezo wa kufua megawati 28.4 na megawati 5 zitokanazo na nguvu ya jua kutoka kwa mzalishaji binafsi.

TANESCO na kununua Umeme
Wizara kupitia TANESCO inanunua umeme wa megawati 31 kati ya hizo megawati 21 kutoka Uganda kwa ajili ya Mkoa wa Kagera na megawati 10 kutoka Zambia kwa ajili ya Mkoa wa Rukwa.

PIA SOMA
- TANESCO: Umeme tunaozalisha ni mwingi mahitaji ni madogo nchi nzima, hakuna mgawo kwa sasa

- Waziri Mkuu Majaliwa: TANESCO imezalisha umeme zaidi ya mahitaji
 
megawati 31 kati ya hizo megawati 21 kutoka Uganda kwa ajili ya Mkoa wa Kagera na megawati 10 kutoka Zambia kwa ajili ya Mkoa wa Rukwa.

Kwa mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Mara, Mwanza na Shinyanga pia wangenunua kutoka Kenya ili umeme wa uhakika usiokatika upatikane, hadi hapo uzalishaji na usambazaji wa umeme wa uhakika toka vyanzo vya ndani na miundombinu mipya ya usambazaji itapokamilika.
 
22.04.2024 Tumezima mitambo 4 umeme umezidi.
24.04.2024 Tunaazima umeme Uganda na Zambia.


Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo - Bado Sana Nchi Inahitaji umeme zaidi ya 5,000 Megawatts na ili Tujitosheleze kabisa ni 10,000 megawatts hapo tutakuwa hatuna uhaba wa mahitaji ya umeme kwa shughuli za Kiuchumi na Kijamii


View: https://m.youtube.com/watch?v=fEGzgp3BnBI
 
Hii Nchi Siku raia wake wakijielewa ndiyo Siku ambayo Viongozi wetu wataanza kuwa serious kutuhudumia.

Haiwezekani Nchi hiyo hiyo Moja, Kunatolewa taarifa mbili tofauti na Viongozi tofauti.

Wanakwambia Umeme tunaozalisha ni ziada hivyo tunaanza kuwauzia Nchi jirani za Zambia/Msumbiji n.k

Leo wanakwambia Umeme wetu hautoshi hivyo kama Nchi tunapaswa kununua Nchi za Jirani za Uganda na Zambia

Hii Nchi aliyeturoga amekufa haki ya nani 🙌
 
Huyu Rais Samia ki ukweli, anakazi ngumu sana!

Mawaziri wake wanapotangaza umeme umekuwa mwingi kuliko mahitaji, huku tukishuhudia mgao wa umeme nchi nzima, Makonda ananza bipi kuitwa kwenye maadili huko ccm?

Kwa nini wasiitwe hawa mawaziri wanaotoa maelezo yasiyoeleweka?

Umeme tunanunua kutoka nje, halafu mgao wa umeme uko palepale, hii ni nini..!?
 
Siku ya kwanza mtu kujiunga na wizi, au siku hiyo hiyo ndo ameiba then akadakwa, hakuhitaji akili kubwa kumhoji ili upate ukweli

Kwa maelezo hayo tu, inatosha kusema, kuna watu wageni wamekaribishwa kwenye makundi ya upigaji na bahati mbaya hawajapewa semina ya kuelezea ili kuondoa wasiwasi kwa wananchi kugundua kuwa wanatupiga!

Hapo kumeelezwa nini na nani kaelewa anyoshe mkono juu??
 
Hii Nchi viongozi utadhani hawana exposure,Wananchi nao sisi ni matahira tu.

Yani Nchi iliyozungukwa na maji,makaa ya mawe,upepo,gas kila eneo inakosa umeme megawati 3000 tu huku kuna kampuni moja tu huko Europe wanatumia megawat 2000.

Yani umeme umekuwa umeme toka kipindi cha Nyerere hadi leo.huu ni ujinga wa hali ya juu.
 
Back
Top Bottom