Gharama za michango ya harusi na sintofahamu ya chakula

Gharama za michango ya harusi na sintofahamu ya chakula

Hivi karibuni kwenye mijadala ya harusi, gumzo limekuwa kadi za mchango. Ukitazama kadi, single unachangia elfu 50, double elfu 90. Hapo mtu anajisikia kama amenunua Tiketi ya Mechi fulani, kumbe unakwenda kuwapiga tafu watu katika harusi yao. Lakini ukifika, unakutana na ujumbe kuwa: “Chakula hakipakuliwi kiholela, kuna catering service waliobobea katika kupakua chakula.”
View attachment 3471398
Sasa mtu anabaki kushangaa, hivi hela yangu niliyoitoa kwa moyo mmoja ni mchango au ni tiketi ya chakula cha kupimwa? Kwanini kwenye harusi watu wanajiona kama wameingia kwenye mgahawa wa five star hotel ya Dubai? Na mbaya zaidi, ukitamka kidogo tu, “mimi leo nataka nyama tu,” unachunguliwa kana kwamba umetukana bibi harusi mbele ya maharusi wote, na wakati mwingine kupewa mifupa.
View attachment 3471397
Jamani, kama mtu hajui, nyama ndiyo kiburudisho kikuu wa sahani. Wali, ndizi na chapati ni wachezaji wa akiba tu. Mchango wangu ni kama mzazi wa mjukuu, siwezi kupewa kipimo cha kijiko kimoja cha nyama eti kwa sababu kuna “uwiano.”
View attachment 3471399
Lakini, tuseme ukweli, hizi harusi zetu zinatufundisha kitu: mchango si bei ya chakula, ni kuunga mkono. Ila basi, wenyeji wakumbuke, ukimpa mtu kadi ya mchango, usimfanye ajisikie kama ameingia kwenye jaribio la kidiplomasia la kula kwa mizani.
View attachment 3471400
Weka ucheshi, acha watu wale mchele, nyama ipate wadau, na watu wabaki na kumbukumbu tamu badala ya kumbukumbu za kuhesabiwa idadi ya nyama.
hahaha
 
Uongoooo!!
Ungejua mimi sio mlaji sana na ni mwembamba. Mama yangu na gf wangu wanagombana nami suala la kula, watu wasio wanene hatuna uroho na kuku wa harusini.
Na sinywi pombe hivyo siwezi lilia bia za michango.
 
Kuchanga siyo lazima ,kama unayo support kama hauna unatulia tu hakuna MBAYA ,maelekezo.
 
Kuna hizi sherehe za kidini wanaita mahafali za kidini ni ushuzi mtupu....55k mchango na chakula kilikuwa cha hovyo nyama zimeisha watu hawajala bado baada ya watu kukaza ndio vipaja walivyojifichia viongozi wa dini vikaletwa ......waliniuzi had cheti nimewaachia

Hii nchi kila mtu tapeli imagine hadi Viongozi wa dini ni matapeli.
 
Mbinu za kutokukosa msosi harusini au kwenye semina ni kuwahi mbelembele, wa mbelembele hufaidi mapande makubwa ya nyama. Utasikia wagawaji chakula wakiambiana punguzeni migao watu bado wengi. Hawa wanaokuwa wa mwishomwisho hupata kidogo kwa kuwa mgao umepunguzwa. Mi huwa nawafuata wazazi wa maharusi nyuma yao, kuwa wa mwisho ni kujitakia kukosa chakula
Miaka ya 2018-2019 tulikuwa tunakaa geto na mwanangu mmoja master sana, ghero lilikuwa karibu Sana na ukumbi yahn MC akiwa anafanywa mbwembwe zake unamsikia na ukumbi ulikuwa kishua sana aisee so harusi za pale hazikuwa za njaaa ....tulikuwa tunazamia harusi mpaka walinzi wa ukumbi wakatusanukia maana kila alhamis na jumamos ilikuwa uhakika.....kigezo vaa vizuri fika mapema kabla maharusi hawajaingia.
 
Back
Top Bottom