Mchungaji Shayo: Michango ya harusi ni ushamba; usitoe mchango wowote

Mchungaji Shayo: Michango ya harusi ni ushamba; usitoe mchango wowote

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
27,566
Reaction score
28,729
Naingia kwenye mada moja kwa moja bila kuwachosha wala kuwachelewesha. Watanzania tumezoea kuchangiana wakati wa shida na raha na utamaduni huu tumedumu nao tangu enzi za mababu zetu hadi sasa.

Pamoja na ukarimu uliopo miongoni mwa watanzania, eti mchungaji huyu hapa chini anapinga kabisa mambo ya kuchangiana kwenye harusi! Anasema harusi sio dharura; kwamba kila mtu aandae sherehe yake kwa gharama zake mwenyewe.

MAONI YANGU
Huyu mchungaji bila shaka ameshiba sadaka anazovuna kutoka kwa wafuasi wake. Ikiwa hataki watu wachangiane kwenye harusi na sherehe mbona yeye anachangiwa sadaka? Ningemuona wa maana zaidi kama naye angekataa kupokea sadaka kutoka kwa waumini. La sivyo, apuuzwe tu.
​
 
Naingia kwenye mada moja kwa moja bila kuwachosha wala kuwachelewesha. Watanzania tumezoea kuchangiana wakati wa shida na raha na utamaduni huu tumedumu nao hadi enzi ya mababu zetu.

Pamoja na ukarimu uliopo miongoni mwa watanzania, eti mchungaji huyu hapa chini anapinga kabisa mambo ya kuchangiana kwenye harusi! Anasema harusi sio dharura; kwamba kila mtu aandae sherehe yake kwa gharama zake mwenyewe.

View attachment 3674943
MAONI YANGU
Huyu mchungaji bila shaka ameshiba sadaka anazovuna kutoka kwa wafuasi wake. Ikiwa hataki watu wachangiane kwenye harusi na sherehe mbona yeye anachangiwa sadaka? Ningemuona wa maana zaidi kama angekataa kupokea sadaka kutoka kwa waumini. La sivyo, apuuzwe tu.
​
Hajijui kuwa mshamba ni yeye, maana inaelekea hana wazazi wala wajomba(si ajabu mtoto haramu)
Mtu akijiita mchungaji kwanza awe na hekima pili awe na akili.
 
Mimi binafsi huwa nachangia misiba, maradhi na dharula zingine za kibinadamu ambazo zinahitaji utatuzi wa haraka!!!

Nilishaachana na kuchangia harusi miaka zaidi ya kumi iliyopita..... zingine za watu wangu wa karibu.....lakini huo ndo umekuwa msimamo wangu.....
 
Wewe wale watu waliokuchangia utawalipaje michango yao mkuu?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom