#COVID19 Fatma Karume: Hakuna chanjo ya lazima. Haki za Binadamu zinataka faragha hususan wa mwili wako

Chanjo yenyewe ni maambukizi yaliyo control, so baada ya hapo hata ukipata maambukizi ambayo hayatojionesha, ambayo ndiyo majority, that is irrelevant.

Kwenye vifo kuwaelimisha, ukiwa na tabia ya kuvuka barabara huku umefumba macho, ukasema umevuka mara tatu na hivyo kuvuka hivyo ni salama, huku hujui kwamba umeweza kuvuka kwa bahati tu, hilo halimaanishi kwamba kuvuka barabara huku umefumba macho ni jambo salama.

Tanzania Covid bado haijachanganya, usichukulie kwamba ndiyo imeshafika peak sasa.
Kwanini unasema Tanzania corona haijachanganya?
 
Madereva wengi wa kitanzania wanaamini kuwa pombe haiathiri uendeshaji wake. Wengine wanadai kuwa wakinywa ndio wanakuwa makini zaidi. Lakini sheria inazuia madereva wote kuendesha magari wakiwa wamekunywa kiasi fulani cha pombe hata wale wanaosema kuwa pombe inawafanya madereva bora zaidi. Kinachozuiwa hapa ni uwezekano wa dereva aliye kunywa kusababisha ajali ambayo itaathiri uhai wa watu wengine hata kama yeye atatoka mzima. Ingekuwa ukinywa pombe na kuendesha gari utaathirika peke yako, pengine serikali zingeona hamna haja ya kuingilia uhuru wako wa kunywa pombe.

Chanjo ni hivyo hivyo. Unaweza ukawa hauamini kuwa kuna corona au/na hauogopi kufa kwa corona kitu ambacho ni haki yako. Shida ni uwezekano wa wewe kuwaambukiza wengine na kuwasababisha ama wapoteze maisha yao au waathirike kwa namna nyingine( kiuchumi, kiafya n.k.) baada ya wewe kuwaambukiza. Na mbaya zaidi ni kuwa wengi wao hautawajua. Ndio maana ili kuwaokoa hao utakaowaambukiza, chanjo ni muhimu kuwa ya lazima. Tusipofanya hivyo hatutafikia herd immunity ambapo wote tutakuwa salama.

Amandla...
Hizi chanjo zina usalama kiasi gani ? Maana Huyu Virus ana tabia ya kumutate na kutengeneza variants tofauti tofauti Kama Variant ya South Africa , Variant ya India , Variant ya Delta ,pengine akatengeneza variant nyingine. Sasa unakuta mtu anapewa chanjo against Variant ya Delta lakini haiwezi kumprotect against Variant ya South Africa . Chanjo iwe hiari na tumuombe Mwenyezi Mungu auondoe huu Ugonjwa .
 
"Hakuna CHANJO ya lazima. HAKI za Binadamu zinataka FARGHA hususan wa MWILI wako. Serikali haiwezi kukuingilia mwili wako isipokuwa pale Mahakama inatoa order Na kama kuna SHERIA lazim iwe proportionate to social needs etc…."- Fatma Karume
She said well, chanjo haiwezi kuwa lazima hata WHO walishasema.Mbowe alikose kidogo atizame matamshi yake upya
 
kinachonifurahisha ni kwamba walikuwa wanahubiri chanjo kumbe na wao hawako tayari kuchanjwa.

mh aikaeli baada ya kuona atakuwa miongoni mwa sample chache zilizopigwa kufanya majaribio ya chanjo sasa anataka awaingizs chaka watu wote.
 
Katika jambo linaloweza kumtoa Mbowe Kwenye reli ya kisiasa ni msimamo wake wa kuitaka serikali kuweka chanjo ni lazima

Mbowe asome nyakati kama anataka kuilibeba Hilo kisiasa
 
Madereva wengi wa kitanzania wanaamini kuwa pombe haiathiri uendeshaji wake. Wengine wanadai kuwa wakinywa ndio wanakuwa makini zaidi. Lakini sheria inazuia madereva wote kuendesha magari wakiwa wamekunywa kiasi fulani cha pombe hata wale wanaosema kuwa pombe inawafanya madereva bora zaidi. Kinachozuiwa hapa ni uwezekano wa dereva aliye kunywa kusababisha ajali ambayo itaathiri uhai wa watu wengine hata kama yeye atatoka mzima. Ingekuwa ukinywa pombe na kuendesha gari utaathirika peke yako, pengine serikali zingeona hamna haja ya kuingilia uhuru wako wa kunywa pombe.

Chanjo ni hivyo hivyo. Unaweza ukawa hauamini kuwa kuna corona au/na hauogopi kufa kwa corona kitu ambacho ni haki yako. Shida ni uwezekano wa wewe kuwaambukiza wengine na kuwasababisha ama wapoteze maisha yao au waathirike kwa namna nyingine( kiuchumi, kiafya n.k.) baada ya wewe kuwaambukiza. Na mbaya zaidi ni kuwa wengi wao hautawajua. Ndio maana ili kuwaokoa hao utakaowaambukiza, chanjo ni muhimu kuwa ya lazima. Tusipofanya hivyo hatutafikia herd immunity ambapo wote tutakuwa salama.

Amandla...
Unapolinganisha vitu, jaribu kutafuta vitu vinavyofanana.

Unalinganisha katazo la kutoingiza kitu mwilini (kunywa pombe) na katazo la uhuru wa kukataa kuingiza kitu mwilini (chanjo).

Hiyo hoja ya kuwaambukiza wengine haina mashiko, kwa sababu tushaona mfano wa Marekani zaidi ya 97% ya wagonjwa wanaopelekwa hospitali ni wale wasiochanjwa, na zaidi ya 99% ya wanaokufa kwa Covid ni wale wasiochanjwa.

Kwa hivyo, wanaotaka kuchanjwa wachanjwe, chanjo itawalinda, hawatapata symptomatic infections, na uwezekano wa kufa kwa Covid ni less than 1%, which is statistically negligible and within a margin of error.

Wasiotaka kuchanjwa, waachiwe uhuru wao, wasichanjwe, wana 97% or more ratio katika wanaopelekwa hospitali. Hawa na zaidi ya 99% ratio ya wanaokufa kwa Covid.

Kwa hiyo hapo utaona kwamba.

1. Wanaochanjwa chanjo inawalinda, tukiweza kumpa chanjo kila anayetaka chanjo, hakuna a realistic fear ya waliochanjwa kuambukizwa na kuwa symptomatic. Hospitalization comprises less than 3% of this group.Deaths comprises less than 1% of this group.

2. Wasiotaka kuchanjwa waelimishwe. Wakiona umuhimu wa chanjo watabadilika. Wale wabishi kabisa waachwe. Waachiwe uhuru wao. Kwa nini kumlazimisha mtu chanjo. Akifa kataka mwenyewe.Hawa ndio wanawapa Wamarekani kwa mfano zaidi ya 97% ya hospitalization na zaidi ya 99% ya vifo vya Covid.

3.Tatizo kubwa naona kuwa hata chanjo za kutosha hazipo. Wanaotaka chanjo hawapati. Which makes the entire discussion about mandatory vaccination for everybody ridiculous. Yani huna chanjo za kuchanja wanaotaka, unalazimisha wote wachanje. Wakija wote uwachanje utawachanja na nini? Kuna watu wanasubiri wengine waanze kuchanja wakiona wamechanja na wako salama watachanja, sasa kwa nini uanze na habari za kulazimisha chanjo hata kabla hujaelimisha watu na kuwaonesha chanjo hazina madhara?

3. Tatizo kubwa ninaloliona
 
Kwa sababu ingechanganya kungekuwa na vifo vingi sana zaidi ya sasa.
Wakati wewe unaeleza hivyo wengine wanaeleza kwamba huu ugonjwa ni wa kuja na kuondoka kwa maana kuna muda inachanganya halafu inakuja kushuka, na kwamba Tanzania imeshapitia hicho kipindi corona ilichanganya ndio kipindi watu walikuwa wanakufa sana na ikaja kushuka hiyo hali.
 
"Hakuna CHANJO ya lazima. HAKI za Binadamu zinataka FARGHA hususan wa MWILI wako. Serikali haiwezi kukuingilia mwili wako isipokuwa pale Mahakama inatoa order Na kama kuna SHERIA lazim iwe proportionate to social needs etc…."- Fatma Karume
Kule hospitali za serikali tunalazimishwa kupimwa voltage kisheria imekaaje
 
Wakati wewe unaeleza hivyo wengine wanaeleza kwamba huu ugonjwa ni wa kuja na kuondoka kwa maana kuna muda inachanganya halafu inakuja kushuka, na kwamba Tanzania imeshapitia hicho kipindi corona ilichanganya ndio kipindi watu walikuwa wanakufa sana na ikaja kushuka hiyo hali.
Hakuna contradiction hapo.Hakuna mutual exclusivity.

Inawezekana huu ugonjwa unachanganya na kushuka katika wimbi ambalo kiujumla lina muelekeo wa kupanda.

Yani ni wimbi lenye vilima na mabonde, linapanda na kushuka, lakini, muelekeo wa jumla ni kupanda.
 
Hizi chanjo zina usalama kiasi gani ? Maana Huyu Virus ana tabia ya kumutate na kutengeneza variants tofauti tofauti Kama Variant ya South Africa , Variant ya India , Variant ya Delta ,pengine akatengeneza variant nyingine. Sasa unakuta mtu anapewa chanjo against Variant ya Delta lakini haiwezi kumprotect against Variant ya South Africa . Chanjo iwe hiari na tumuombe Mwenyezi Mungu auondoe huu Ugonjwa .
Na ndio mnavyozidi kukaa bila kuchanja ndio variants mpya zinavyokitokeza. Hatimae mnaweza kukuta chanjo hazina uwezo wa kukabiliana na variants zitakazojitokeza. Hiyo Delta variant ndio ya India na sasa hivi ndio inafyeka watu sana Uganda. Chanjo zilizopo bado zinatoa kinga lakini hatujui Kama ikitokea variant nyingine kama bado itakuwa effective. Mtaomba sana lakini bila sayansi huu ugonjwa utatufyeka sana. Mimi naamini hapa kweli hizi chanjo zingekuja kwenye kibuyu na angekuwa mtaalam mmoja ndio anazitoa tungepigana vikumbo kuziwahi kama tulivyofanya kwenye kikombe cha babu. Ulokole wetu na imani zetu kwenye mambo ya kitamaduni utatuua.

Amandla...
 
Kwa sababu ingechanganya kungekuwa na vifo vingi sana zaidi ya sasa.
Unajuaje kuwa vifo ni vichache wakina hamna takwimu? Watanzania wengi hawafii hospitali, kitu ambacho kwa vyovyote hakitakuwa reflected kwenye takwimu. Watu wanakufa wakutosha tuu.

Amandla...
 
Hakuna contradiction hapo.Hakuna mutual exclusivity.

Inawezekana huu ugonjwa unachanganya na kushuka katika wimbi ambalo kiujumla lina muelekeo wa kupanda.

Yani ni wimbi lenye vilima na mabonde, linapanda na kushuka, lakini, muelekeo wa jumla ni kupanda.
Dalili ipi yenye kuonesha muelekeo wa jumla wa kupanda? ukizingatia huu ugonjwa ni toka mwaka jana na toka kipindi hicho kulikuwa na mitazamo ya kupanda sijui kuchangaya ila hadi sasa tunakaribia kumaliza na huu mwaka.
 
Vifo vya watu wa familia, vifo vya watu maarufu, taarifa za kuhitajika oxygen Mwanza Bugando na KCMC.

Kwa nini serikali haitoi data?
 
Kuna tatizo gani kusema SAMAHANI TAARIFA NILIO TOA HAIKUWAFURAHISHA?. Ungwana ni kusikilizana na ulio tofautiana kimawazo.
 
Kiukweli Freeman Mbowe amechemka sana ktk hili; nashauri arudi kuomboleza msiba wa kaka yake. Chanjo ya corona haiwez kuwa jambo la lazima. Anayetaka achanje asiyetaja asichanje
Mbowe ana hofu! Anataka kuriwadhika na "kifo cha wengi harusi"! Yeye alishaingizwa chaka akachanjwa"! Na madhara yanaripotiwa kila siku! Anaona asiangamie peke yake!! Nakupa pole "mwamba wa karatasi"
 
Back
Top Bottom