Eswatini: Jeshi na Polisi wapelekwa shuleni kuzuia maandamano

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Makundi yanayotetea demokrasia katika taifa la kusini mwa Afrika, Eswatini, yanaeleza kwamba serikali imepeleka wanajeshi na polisi katika shule ambazo wanafunzi wamekuwa wakiendelea na maandamano kwa wiki kadhaa wakitaka mageuzi ya kisiasa.

Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari katika taifa ambalo zamani lilifahamika kwama Swaziland, na taifa pekee la Kiafrika lenye utawala kamili wa kifalme, wamesusia masomo na wamekuwa wakiandamana kwa amani.

Madai yao ya msingi ni kuachiliwa waandamanaji wawili wanaotetea demokrasia, ambao walikamatwa mwanzano mwa mwaka huu, pia wanahitaji mazingira bora ya kusomea, na elimu iwe bure.

Msemaji wa kundi moja la kutetea demokrasia la Swaziland Solidarity Network, Lucky Lukhele, amesema wanajeshi walipelekwa katika shule hizo ili kuwatisha wanafunzi lakini hawakudhuru wanafunzi hao.

Licha ya hayo, amedai wanafunzi 17 ikijumuisha wale wenye umri wa miaka 7 walikamatwa katika maandamano ya Jumatatu.

Msemaji wa jeshi Tengetile Khumalo, amethibitisha jeshi kupelekwa katika shule ambazo wanafunzi wanaandamana.

Chanzo: VOA Swahili
 
Yaani Eswatin hadI wanafunzi wa primary wanaandamana kudai haki zao.
Hapa Tanzania utasikia majinga yanasema Mbowe,Lissu na Lema watangulize familia zao mbele.

Ujinga hautaisha Tanzania.
Inawezekana huko hawajahamasishwa na wanasiasa, wameamua kuingia front kwa kuhamasishana wenyewe kwa wenyewe na hata kama wameshamasishwa na viongozi wao wapo frontline.

Sasa tuje huku kwetu hata tukihamasishwa je wanaotuhamasisha wanakuwepo front au ndio wanatutoa mbuzi wa kafara huku wao wakiandamania kwenye mitandao ya kijamii?

Unajua inatia moyo sana kwa mhasishwaji ktk maandamano akimuona kiongozi wake front, inaleta maana kwamba mpo pamoja kiukweli kwa shida na raha, mkikamamtwa mnakamatwa wote , mkichezea vichapo mnachezea wote, sasa je hao viongozi wetu wa upinzani hufanya hivyo?
 
Inawezekana huko hawajahamasishwa na wanasiasa,wameamua kuingia front kwa kuhamasishana wenyewe kwa wenyewe na hata kama wameshamasishwa na viongozi wao wapo frontline,

Sasa tuje huku kwetu hata tukihamasishwa je wanaotuhamasisha wanakuwepo front au ndio wanatutoa mbuzi wa kafara huku wao wakiandamania kwenye mitandao ya kijamii?

Unajua inatia moyo sana kwa mhasishwaji ktk maandamano akimuona kiongozi wake front,inaleta maana kwamba mpo pamoja kiukweli kwa shida na raha,mkikamamtwa mnakamatwa wote , mkichezea vichapo mnachezea wote,sasa je hao viongozi wetu wa upinzani hufanya hivyo???
Lissu anaandamaniaga Belgium!! ha ha ha!
 
Yaani Eswatin hadI wanafunzi wa primary wanaandamana kudai haki zao.
Hapa Tanzania utasikia majinga yanasema Mbowe,Lissu na Lema watangulize familia zao mbele.

Ujinga hautaisha Tanzania.
Basi watangulie watoto wa mbowe lissu na lema then sisi tufuate!
 
Lissu anaandamaniaga Belgium!! ha ,wakati yeye mwenyewe au familia yake ipo mbali,hio ndio shida,wenzetu wakianzisha mtiti wanaanzisha wote bila kujali kiongozi au mfuasi,kwetu hapa viongozi wa upinzani wapo kwa ajili ya matumno yao na sio wananchi

Lissu anaandamaniaga Belgium!! ha ha ha!
Bongo hakuna wapinzani,kuna wachumia tumbo tu mkuu,amini nakuambia
 
Inawezekana huko hawajahamasishwa na wanasiasa,wameamua kuingia front kwa kuhamasishana wenyewe kwa wenyewe na hata kama wameshamasishwa na viongozi wao wapo frontline,

Sasa tuje huku kwetu hata tukihamasishwa je wanaotuhamasisha wanakuwepo front au ndio wanatutoa mbuzi wa kafara huku wao wakiandamania kwenye mitandao ya kijamii?

Unajua inatia moyo sana kwa mhasishwaji ktk maandamano akimuona kiongozi wake front,inaleta maana kwamba mpo pamoja kiukweli kwa shida na raha,mkikamamtwa mnakamatwa wote , mkichezea vichapo mnachezea wote,sasa je hao viongozi wetu wa upinzani hufanya hivyo???
Tumia kichwa vizuri basi,unataka kusema huko Eswatin viongozi wameenda hadi shule kuhamasisha maandamano?
Kazi ya viongozi ni kuamsha hisia na hali,kukujulisha usichojua kama ni haki yako,kukujulisha kuwa unaonewa pale amabapo wewe hujui.
KAZI YA KUDAI NI YAKO SASA,SIYO YAO TENA.
Kwamba kwa mfano Tanzania ikipata katiba mpya itamfaidisha Mbowe au Lissu kwa miaka mingapi?
Akili za kijima hizi ndiyo zinarudisha hii nchi nyuma
 
Mbona viongozi wa upinzan alwaya huwa wapo front? Mbowe alikoswa risasi, mke wa doctor slaa alipasuliwa kichwani na lipumba alivunjwa mkono mbagala, hawa wote walikuwa we ulikuwa wapi au ulikuwa unaandamana JF
 
Tumia kichwa vizuri basi,unataka kusema huko Eswatin viongozi wameenda hadi shule kuhamasisha maandamano?
Kazi ya viongozi ni kuamsha hisia na hali,kukujulisha usichojua kama ni haki yako,kukujulisha kuwa unaonewa pale amabapo wewe hujui.
KAZI YA KUDAI NI YAKO SASA,SIYO YAO TENA.
Kwamba kwa mfano Tanzania ikipata katiba mpya itamfaidisha Mbowe au Lissu kwa miaka mingapi?
Akili za kijima hizi ndiyo zinarudisha hii nchi nyuma
Katiba kwa sasa sio takwa la wananchi,ni takwa la chadema,upo hapo?
 
Yaani Eswatin hadI wanafunzi wa primary wanaandamana kudai haki zao.
Hapa Tanzania utasikia majinga yanasema Mbowe,Lissu na Lema watangulize familia zao mbele.

Ujinga hautaisha Tanzania.
Wewe huwa unaandamana au nawe unamsubiri Mbowe na Lema waambiwe hivyo halafu unatoa comment tu huku jf?
 
Katiba kwa sasa sio takwa la wananchi,ni takwa la chadema,upo hapo?
CHADEMA ni polisi?
Au ni kina nani?
Usikariri kila anachosema Mwigulu.
Unabana pua katiba ni takwa la CHADEMA siyo la wananchi, kwani hao CHADEMA ni kina nani.
 
Basi watangulie watoto wa mbowe lissu na lema then sisi tufuate!
Akili za wapi hizo?Unataka haki yako au unawataka watoto wa Mbowe?Kajitolea kukusemea na kukutetea lakini huridhiki hadi uwaone watoto wake?Kama familia yake haina mtazamo wa baba yao utafanyaje?
 
Uliona au kusikia sehemu Nyerere alimtanguliza mbele mtoto wake Anna au Makongoro wakati wa kudai Uhuru?Mandela na Kenyatta je?Kama "weye" hautaki,utulie!
Nyerere na Mandela ndio usiwataje kabisaaa,kama hujui historia bora utoe upupu wako hapa,hujui kwamba Mandela alifungwa kwa sababu zipi??
 
Yaani Eswatin hadI wanafunzi wa primary wanaandamana kudai haki zao.
Hapa Tanzania utasikia majinga yanasema Mbowe,Lissu na Lema watangulize familia zao mbele.

Ujinga hautaisha Tanzania.

kamandaaa

unaongozaje maandamano bila kushusha mguu road!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom