Israeli: Demokrasia yenye dosari na ubaguzi uliozagaa

Hamid Rubawa

Member
May 23, 2018
72
202
Ahmed Rajab

Maelezo ya Picha. Aliyekuwa Kiongozi wa Wapalestina, Yasser Arafat (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa zamani wa Comoro, Ahmed Abdallah (kushoto) na aliyekuwa Mufti wa Comoro Sayyid Muhammad Abdulrahman (kulia), wakati alipotembelea taifa hilo kwenye miaka ya nyuma.

‘Je, Israeli ni dola la ubaguzi wa kikabila?’ Nilimuuliza mwandishi habari maarufu wa Israeli Gideon Spiro kwenye mkahawa wa Bookworm Café jijini Tel Aviv, Mei 2009. Bookworm ni duka la vitabu lakini lina mkahawa na ni mahali ambapo Waisraeli wa mrengo wa kushoto hukutana.

Sijui kwa nini nilimuuliza Spiro swali hilo kwani nikijua kwamba Israeli ni nchi ya kibaguzi yenye utawala wa kikaburu. Labda nikitaka kushangazwa. Labda nikitaka kumsikia Mwisraeli wa mrengo wa kushoto akikana, kama inavyokana serikali yao, kwamba nchi hiyo si ya kibaguzi.

Siku chache kabla nilimuuliza swali hilo hilo mwandishi mwengine Wakiisraeli mwenye mawazo ya wastani. Alinijibu, kinaga ubaga, kwamba Israel ni dola la kibaguzi.

Lakini Spiro, aliyekuwa na umri wa miaka 77, hakukurukupa. Niliiona tabasamu yake iliyokunjika ikichezacheza kwenye ndimi zake na macho yake yakimetameta. Alilipima jibu lake kabla ya kufungua mdomo wake na alipoufungua alisema haya: ‘Ni mfumo wa utawala wa kimbari (ethnocracy)’.

Baada ya kusema hayo alisita, akapiga fundo la kahawa aipendayo, iliyojaa povu la maziwa — aina ya Cappuccino — na akaendelea kunieleza hivi:

‘Kwa Wayahudi ni utawala wa demokrasia yenye mipaka, kwa Wapalestina walio kwenye maeneo yanayokaliwa na Israeli ni utawala wa udikteta wa kijeshi na kwa Waarabu wa Israeli ni utawala wa demokrasia yenye ubaguzi. Lakini kwa Wayahudi na Waarabu kwa pamoja utawala huo si wa demokrasia,’ alisema.

Ingawa Wapalestina wana utambulisho mmoja, kuna aina tano za Wapalestina. Kuna Wapalestina wa Gaza walio chini ya utawala wa Hamas, kuna wa Ufukwe wa Magharibi wa Mto Jordan walio chini ya Mamlaka ya Palestina, kuna wa Jerusalem ya Mashariki wenye ukaazi wa kudumu, kuna Waarabu wa Israeli wenye uraia wa Israeli na kuna Wapalestina walio uhamishoni, wasioruhusiwa kurudi kwao.

Wapalestina wa sampuli zote hizo hawasalimiki na makucha ya chuma ya Israeli. Walio Gaza, mara kwa mara, hutwangwa kwa mabomu ya Israeli.

Wa Ufukwe wa Magharibi wanaishi katika eneo linalokaliwa kijeshi na Israeli. Wanajeshi wa Israeli huingia katika eneo hilo saa yoyote waitakayo, huzivamia nyumba na kuzipekua juu chini. Huwakamata au kuwaua Wapalestina wa huko.

Maisha ya Wapalestina wa Ufukwe wa Magharibi ni magumu katika miji yake yote ikiwa pamoja na Ramallah, Nablus, Hebron, Bathlehem, Qalqilya, Jenin na Tulkarm. Wanashambuliwa na walowezi wa Kiyahudi wenye silaha na wanaolindwa na wanajeshi wa Israeli ili waweze kuiba ardhi za Wapalestina.

Wapalestina wa Jerusalem ya Mashariki wanatolewa kwa nguvu majumbani mwao na nyumba zao wanapewa Wayahudi kutoka Marekani. Na Waarabu wa Israeli daima hubaguliwa. Ni marufuku Waarabu wa Israeli kuoa wanawake wa Kiyahudi. Siku hizi ni nadra kuwaona Waarabu wa Israeli wakitoka nje saa za usiku; wanaogopa. Hofu yao ni magenge ya wahalifu wenye silaha wenye kuwashambulia.

Kuna sheria 65 zenye kuwabagua Waarabu wenye uraia wa Israeli. Waarabu hao hawaruhusiwi kununua ardhi katika maeneo mengi ya Israeli. Vijiji vingi vya Waarabu vimetengwa mbali na miji ya Wayahudi. Katika Israeli nzima kuna miji kama minane tu ambamo Waarabu na Wayahudi wanaruhusiwa kuishi pamoja. Kila mji wa Waarabu umezungukwa na makazi ya Wayahudi kuwazuia Waarabu wasijitanue.

Spiro aliongeza kwamba, hata wenyewe kwa wenyewe, Wayahudi wanabaguana. Wayahudi wenye asili za kizungu ndio walio tabaka la juu lenye kutawala na Wayahudi waliosalia, hasa walio weusi, wako chini, fungu la Mungu.

Ikiwa hivyo ndivyo watendewavyo Wayahudi Weusi, kefu Wapalestina Weusi wenye asili ya Kiafrika na walio Waislamu? Kama nilivyogusia wiki iliyopita nilikutana nao katika jangwa la Negev walikonialika chakula cha mchana.

Wapalestina hao wa Kiafrika wameshiriki katika harakati za ukombozi. Aliye maarufu na ambaye sikujaaliwa kukutana naye, alikuwa Fatima Mohamed Bernawi, aliyefariki Cairo, Misri, Novemba mwaka jana na kuzikwa Gaza.

Hayati Fatima Bernawi, Mwanamapinduzi wa Kipalestina mwenye asili ya Kiafrika
Fatima alizaliwa Jerusalem mwaka 1939. Baba yake, aliyetoka Nigeria, alishiriki katika mapigano ya Wapalestina ya 1936 dhidi ya Waingereza. Mama yake alikuwa Mpalestina. Alipokuwa na miaka tisa wakati wa ‘Nakba’ (Maafa) ya 1948 Wayahudi walipokuwa wakiwafukuza Wapalestina kutoka kwenye nyumba zao na kuyapora mashamba yao, Fatima alimfuata mama yake aliyekimbilia kambi ya wakimbizi karibu na Amman, mji mkuu wa Jordan. Baba yake alibakia Palestina. Baadaye, Fatima na mama yake walirudi Jerusalem kuishi naye.

Alipokuwa anakua, Fatima alijiunga na mvuvumko wa ukombozi wa Palestina. Alikuwa miongoni mwa Wapalestina waliopatiwa mafunzo ya kijeshi ili wapambane na Israeli. Yeye alikuwa mwanamke wa kwanza wa Kipalestina aliyeandaa shambulizi dhidi ya Israeli.

Oktoba 1967 alitega bomu ndani ya sinema katika Jerusalem ya Magharibi. Ingawa bomu hilo halikuripuka wanajeshi wa Israeli walimkamata, akiwa Mpalestina wa kwanza wa kike kutiwa nguvuni na vyombo vya ulinzi vya Israeli. Fatima alihukumiwa kifungo cha maisha. Alikaa jela kwa miaka kumi. Aliachiwa kwa maafikiano ya Israeli na Wapalestina ya kubadilishana wafungwa.

Yasser Arafat, aliyekuwa kiongozi wa Chama Kikuu cha Ukombozi wa Palestina (PLO), alikawia sana kuoa. Alioa akiwa na miaka 61. Kabla hajaoa akisema kwamba kama ataoa, atamuoa Fatima Bernawi. Fatima hakuwa riziki yake Arafat kwani aliolewa na Mpalestina mwengine aliyewahi kuwa mfungwa wa Waisraeli, Fawzi al-Nimr, aliyeachiwa huru Mei 1985.

Kufikia 1996 Fatima alikuwa mwanamke wa ngazi ya juu kabisa katika jeshi la mgambo la chama cha Fateh na mkuu wa polisi wa kike katika serikali ya Gaza na Jericho.

Wiki iliyopita nilieleza kwamba kabla ya kuingia Gaza nilikaa Israeli kwa siku kadhaa. Nilipata fursa ya kuingia Ufukwe wa Magharibi na kushinda, kwa siku nzima, Ramallah, makao ya Rais Mahmoud Abbas, mrithi wa Arafat.

Arafat akiipenda Afrika na alikuwa na mshauri wake muhtasi kuhusu Afrika, Salman al-Hirif. Kadhalika, alikuwa na usuhuba na viongozi kadhaa wa Kiafrika. Akisikilizana na Nelson Mandela, Mwalimu Julius Nyerere pamoja na mrithi wake Rais Ali Hassan Mwinyi na pia Ahmed Abdallah, aliyekuwa Rais wa Comoro.

Arafat aliwahi kuzizuru Afrika Kusini, Tanzania na Comoro, ingawa Comoro hakulala kwa sababu ya usalama wake. Wakati huo, Comoro ilikuwa ikidhibitiwa na mamluki wa Kizungu waliomrejesha madarakani Abdallah ambaye baadaye walimuua.

Nilipokuwa Ramallah nililizuru kaburi lake Arafat. Kuvuka Ufukwe wa Magharibi na kuingia Israel si rahisi kwa Wapalestina. Kuna vizuizi vingi vya barabarani na wanajeshi wa Israeli wanaovisimamia hawana huruma na Wapalestina. Kazi yao kubwa ni kuwanyanyasa.

Wanyanyasaji ni vitoto vidogo utafikiri vina umri wa miaka 16. Lakini wana silaha nzito na ndimi zao zimejaa kiburi na ufedhuli. Kwa hivyo, ‘vijanajeshi’ hivyo vinakuwa mabwana — ingawa wengine ni wasichana — na ukiwa Mpalestina hukuona kinyangarika tu.

Niliyaona mengi Israeli. Nilizifuata nyayo za Nabii Issa (Yesu Kristo), nikatembea kwenye Mji Mkongwe wa Quds (Jerusalem), nikasali Ijumaa mbili kwenye msikiti wa Al Aqsa. Kiguu na njia nikaizuru miji ya Tel Aviv, Jaffa, Sderot na Be’er Sheva ulio katika Jangwa la Negev.

Israeli ni nchi ya kuta, vizuizi, vikwazo, vipingamizi na vikaratasi vya ruhusa na vibali vya kila aina wanavyotakiwa Wapalestina wawe navyo. Daima wanadhalilishwa kwa kila namna ya idhilali. Nyumba zao zinabomolewa, wanafukuzwa makwao na lengo la Wazayoni jijini Jerusalem ni kuufanya mji mzima uwe na sura ya Kiyahudi.

Waarabu hawaruhusiwi kujenga katika Jerusalem ya Magharibi kwa Wayahudi lakini Wayahudi wanaruhusiwa kujenga Jerusalem ya Mashariki kwa Waarabu.

Siku moja nilialikwa kwenye Bunge la Israel, Knesset, na Dakta Dov Khenin, aliyekuwa Mbunge wa chama cha Hadash, chama pekee cha Wayahudi na Waarabu na ambacho ni cha mrengo wa kushoto. Khenin alikuwa pia mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha Israeli, Maki.

Ofisini mwake Khenin alitundika picha ya Che Guevara, mwanamapinduzi mzalia wa Argentina aliyeshiriki kwenye mapinduzi ya Cuba. Nilipomwambia kwamba tathmini yake ya mustakbali wa mgogoro wa Israeli na Wapalestina inakosa rajua, kwa vile inayaona mambo yote kuwa yasiyo na mbele wala nyuma, alinijibu kwa kumnukuu mwanafalsafa wa Kimarx wa Kitaliana, Antonio Gramsci.

Alinikumbusha kwamba Gramsci aliwahi kuandika kwamba alikuwa hana ‘rajua ya akili, lakini alikuwa na dhamira ya kutegemea mema’ (pessimist of the intellect, optimist of the will). Ukosefu wa rajua ni kichocheo cha kuchukuwa hatua, na msimamo wa kutarajia mazuri ni ukakamavu wa kuamini kwamba hatua hiyo italeta mageuzi ya maana hata pakiwa na nakama.

Khenin alinisikitikia kwamba ubovu wa Israeli ni kuwa Waarabu na Wayahudi hawalingani kwa lolote. Jamii zao zimegawika vibaya. Hajakusudia Wapalestina na Wayahudi lakini Waarabu wa Israel na Wayahudi wao.

Si tu kwamba Waarabu na Wayahudi wanazungumza lugha tofauti lakini hata misamiati yao ni tofauti na dhana (concepts) zao ni tofauti — katika siasa, utamaduni, na katika maingiliano yao ya kijamii ambayo ni madogo mno na kwa namna wanavyoangaliana, kwa kuchujana.

Jamii zote mbili zinaogopana. Wayahudi wana hofu na Waarabu; Waarabu nao wanawaogopa Wayahudi. Lakini alitaka nitambuwe kwamba ‘Israeli sio tu pahala ambapo matatizo hukutana lakini pia ni pahala penye uwezekano mwingi,’ yaani mengi yanaweza kufanywa.

Hamna shaka kwamba hii ni saa ya giza katika Israeli. Ni wakati ambapo mengi yanaweza kufanywa, na lazima yafanywe, ili eneo zima la Mashariki ya Kati liwe na amani. La kwanza ni kuufumua mfumo mzima wa kikabila na ubaguzi uliotamalaki katika taifa hilo.

Dhana kama ‘demokrasia’ na ‘uhuru’ au ‘ukombozi’ zimekuwa zikitumiwa vibaya na wanasiasa wa Kizayoni. Wanazitumia kwa maslahi ya kikabila — kabila la Wayahudi. Lakini kuna tatizo: Wayahudi wengi wanazidi kupaza sauti zao kuwapinga Wazayoni, wakihoji kwamba imani za Kizayoni, zikiwa pamoja na kuundwa kwa dola la Israeli na misingi yake ya kikaburu, zinakwenda kinyume na dini yao na ni ukoloni wa Kizayoni. Uzayoni wenyewe nao ni itikadi ya ubaguzi wa kikabila.

Sauti hizo za Wayahudi zinapazwa sambamba na zile zinazotaka Wapalestina warejeshewe haki zao na demokrasia halisi isimamishwe Israel.

Ahmed Rajab ni mwandishi wa kimataifa na mchambuzi. §§§§§§§§§London, Postgraduate Diploma (Urbanisation in Developing Countries) kutoka University College, London na shahada ya MA (African Political Economy na Modern African Literature) kutoka Chuo Kikuu cha Sussex.

Gazeti la Dunia ni Jukwaa Huru la Fikra kwa wasomaji wa lugha ya Kiswahili lenye lengo la kuchapa makala za kichambuzi kuhusu masuala mbalimbali muhimu kwa Tanzania, Afrika na Dunia kwa ujumla. Waandishi wa kwenye jukwaa hili ni maveterani na wabobezi kwenye maeneo watakayokuwa wanaandikia. Kama unajua unachokiandika, hili ni jukwaa lako.

Screenshot_20231025-102622_Chrome.jpg
 
IMG_0596.jpg
 
Haya mapicha hayaondoi uhalsia, maukatili ya hiyo dini yenu ndio yamesababisha tufike huku, mjifunze kuishi na binadamu wengine kwa amani, mnashambulia Wayahudi kwa rockets huku mkichekelea na kupiga makelele ya akbar akbar, wakijibu mnaanza kupachika mapicha ya kutafuta huruma, mbona akbar wenu huyo hawasaidii kwa sasa.
Dini iliyojaa chuki, yaani mumeagizwa kabisa kuwachinja Wayahudi wote....ila mumeshindwa na imeshindikana na nyie ndio mnauawa wengi...

sahih muslim 2921
Abdullah b. 'Umar reported Allah's Messenger (ﷺ) as saying:
You and the Jews would fight against one another until a stone would say: Muslim, here is a Jew behind me; come and kill him.
 
Suha Arafat

Yasser Arafat/Wife (m. 1990–2004)

Personal life. In 1990, Arafat married Suha Tawil, a Palestinian Christian, when he was 61 and Suha, 27. Her mother introduced her to him in France, after which she worked as his secretary in Tunis. Prior to their marriage, Arafat adopted fifty Palestinian war orphans.
 
Haya mapicha hayaondoi uhalsia, maukatili ya hiyo dini yenu ndio yamesababisha tufike huku, mjifunze kuishi na binadamu wengine kwa amani, mnashambulia Wayahudi kwa rockets huku mkichekelea na kupiga makelele ya akbar akbar, wakijibu mnaanza kupachika mapicha ya kutafuta huruma, mbona akbar wenu huyo hawasaidii kwa sasa.
Dini iliyojaa chuki, yaani mumeagizwa kabisa kuwachinja Wayahudi wote....ila mumeshindwa na imeshindikana na nyie ndio mnauawa wengi...

sahih muslim 2921
Abdullah b. 'Umar reported Allah's Messenger (ﷺ) as saying:
You and the Jews would fight against one another until a stone would say: Muslim, here is a Jew behind me; come and kill him.

Dalili za kujibu bila kusoma. Soma mada kujiridhisha kuwa unakuwa kwenye mada.
 
Ahmed Rajab

Maelezo ya Picha. Aliyekuwa Kiongozi wa Wapalestina, Yasser Arafat (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa zamani wa Comoro, Ahmed Abdallah (kushoto) na aliyekuwa Mufti wa Comoro Sayyid Muhammad Abdulrahman (kulia), wakati alipotembelea taifa hilo kwenye miaka ya nyuma.

‘Je, Israeli ni dola la ubaguzi wa kikabila?’ Nilimuuliza mwandishi habari maarufu wa Israeli Gideon Spiro kwenye mkahawa wa Bookworm Café jijini Tel Aviv, Mei 2009. Bookworm ni duka la vitabu lakini lina mkahawa na ni mahali ambapo Waisraeli wa mrengo wa kushoto hukutana.

Sijui kwa nini nilimuuliza Spiro swali hilo kwani nikijua kwamba Israeli ni nchi ya kibaguzi yenye utawala wa kikaburu. Labda nikitaka kushangazwa. Labda nikitaka kumsikia Mwisraeli wa mrengo wa kushoto akikana, kama inavyokana serikali yao, kwamba nchi hiyo si ya kibaguzi.

Siku chache kabla nilimuuliza swali hilo hilo mwandishi mwengine Wakiisraeli mwenye mawazo ya wastani. Alinijibu, kinaga ubaga, kwamba Israel ni dola la kibaguzi.

Lakini Spiro, aliyekuwa na umri wa miaka 77, hakukurukupa. Niliiona tabasamu yake iliyokunjika ikichezacheza kwenye ndimi zake na macho yake yakimetameta. Alilipima jibu lake kabla ya kufungua mdomo wake na alipoufungua alisema haya: ‘Ni mfumo wa utawala wa kimbari (ethnocracy)’.

Baada ya kusema hayo alisita, akapiga fundo la kahawa aipendayo, iliyojaa povu la maziwa — aina ya Cappuccino — na akaendelea kunieleza hivi:

‘Kwa Wayahudi ni utawala wa demokrasia yenye mipaka, kwa Wapalestina walio kwenye maeneo yanayokaliwa na Israeli ni utawala wa udikteta wa kijeshi na kwa Waarabu wa Israeli ni utawala wa demokrasia yenye ubaguzi. Lakini kwa Wayahudi na Waarabu kwa pamoja utawala huo si wa demokrasia,’ alisema.

Ingawa Wapalestina wana utambulisho mmoja, kuna aina tano za Wapalestina. Kuna Wapalestina wa Gaza walio chini ya utawala wa Hamas, kuna wa Ufukwe wa Magharibi wa Mto Jordan walio chini ya Mamlaka ya Palestina, kuna wa Jerusalem ya Mashariki wenye ukaazi wa kudumu, kuna Waarabu wa Israeli wenye uraia wa Israeli na kuna Wapalestina walio uhamishoni, wasioruhusiwa kurudi kwao.

Wapalestina wa sampuli zote hizo hawasalimiki na makucha ya chuma ya Israeli. Walio Gaza, mara kwa mara, hutwangwa kwa mabomu ya Israeli.

Wa Ufukwe wa Magharibi wanaishi katika eneo linalokaliwa kijeshi na Israeli. Wanajeshi wa Israeli huingia katika eneo hilo saa yoyote waitakayo, huzivamia nyumba na kuzipekua juu chini. Huwakamata au kuwaua Wapalestina wa huko.

Maisha ya Wapalestina wa Ufukwe wa Magharibi ni magumu katika miji yake yote ikiwa pamoja na Ramallah, Nablus, Hebron, Bathlehem, Qalqilya, Jenin na Tulkarm. Wanashambuliwa na walowezi wa Kiyahudi wenye silaha na wanaolindwa na wanajeshi wa Israeli ili waweze kuiba ardhi za Wapalestina.

Wapalestina wa Jerusalem ya Mashariki wanatolewa kwa nguvu majumbani mwao na nyumba zao wanapewa Wayahudi kutoka Marekani. Na Waarabu wa Israeli daima hubaguliwa. Ni marufuku Waarabu wa Israeli kuoa wanawake wa Kiyahudi. Siku hizi ni nadra kuwaona Waarabu wa Israeli wakitoka nje saa za usiku; wanaogopa. Hofu yao ni magenge ya wahalifu wenye silaha wenye kuwashambulia.

Kuna sheria 65 zenye kuwabagua Waarabu wenye uraia wa Israeli. Waarabu hao hawaruhusiwi kununua ardhi katika maeneo mengi ya Israeli. Vijiji vingi vya Waarabu vimetengwa mbali na miji ya Wayahudi. Katika Israeli nzima kuna miji kama minane tu ambamo Waarabu na Wayahudi wanaruhusiwa kuishi pamoja. Kila mji wa Waarabu umezungukwa na makazi ya Wayahudi kuwazuia Waarabu wasijitanue.

Spiro aliongeza kwamba, hata wenyewe kwa wenyewe, Wayahudi wanabaguana. Wayahudi wenye asili za kizungu ndio walio tabaka la juu lenye kutawala na Wayahudi waliosalia, hasa walio weusi, wako chini, fungu la Mungu.

Ikiwa hivyo ndivyo watendewavyo Wayahudi Weusi, kefu Wapalestina Weusi wenye asili ya Kiafrika na walio Waislamu? Kama nilivyogusia wiki iliyopita nilikutana nao katika jangwa la Negev walikonialika chakula cha mchana.

Wapalestina hao wa Kiafrika wameshiriki katika harakati za ukombozi. Aliye maarufu na ambaye sikujaaliwa kukutana naye, alikuwa Fatima Mohamed Bernawi, aliyefariki Cairo, Misri, Novemba mwaka jana na kuzikwa Gaza.

Hayati Fatima Bernawi, Mwanamapinduzi wa Kipalestina mwenye asili ya Kiafrika
Fatima alizaliwa Jerusalem mwaka 1939. Baba yake, aliyetoka Nigeria, alishiriki katika mapigano ya Wapalestina ya 1936 dhidi ya Waingereza. Mama yake alikuwa Mpalestina. Alipokuwa na miaka tisa wakati wa ‘Nakba’ (Maafa) ya 1948 Wayahudi walipokuwa wakiwafukuza Wapalestina kutoka kwenye nyumba zao na kuyapora mashamba yao, Fatima alimfuata mama yake aliyekimbilia kambi ya wakimbizi karibu na Amman, mji mkuu wa Jordan. Baba yake alibakia Palestina. Baadaye, Fatima na mama yake walirudi Jerusalem kuishi naye.

Alipokuwa anakua, Fatima alijiunga na mvuvumko wa ukombozi wa Palestina. Alikuwa miongoni mwa Wapalestina waliopatiwa mafunzo ya kijeshi ili wapambane na Israeli. Yeye alikuwa mwanamke wa kwanza wa Kipalestina aliyeandaa shambulizi dhidi ya Israeli.

Oktoba 1967 alitega bomu ndani ya sinema katika Jerusalem ya Magharibi. Ingawa bomu hilo halikuripuka wanajeshi wa Israeli walimkamata, akiwa Mpalestina wa kwanza wa kike kutiwa nguvuni na vyombo vya ulinzi vya Israeli. Fatima alihukumiwa kifungo cha maisha. Alikaa jela kwa miaka kumi. Aliachiwa kwa maafikiano ya Israeli na Wapalestina ya kubadilishana wafungwa.

Yasser Arafat, aliyekuwa kiongozi wa Chama Kikuu cha Ukombozi wa Palestina (PLO), alikawia sana kuoa. Alioa akiwa na miaka 61. Kabla hajaoa akisema kwamba kama ataoa, atamuoa Fatima Bernawi. Fatima hakuwa riziki yake Arafat kwani aliolewa na Mpalestina mwengine aliyewahi kuwa mfungwa wa Waisraeli, Fawzi al-Nimr, aliyeachiwa huru Mei 1985.

Kufikia 1996 Fatima alikuwa mwanamke wa ngazi ya juu kabisa katika jeshi la mgambo la chama cha Fateh na mkuu wa polisi wa kike katika serikali ya Gaza na Jericho.

Wiki iliyopita nilieleza kwamba kabla ya kuingia Gaza nilikaa Israeli kwa siku kadhaa. Nilipata fursa ya kuingia Ufukwe wa Magharibi na kushinda, kwa siku nzima, Ramallah, makao ya Rais Mahmoud Abbas, mrithi wa Arafat.

Arafat akiipenda Afrika na alikuwa na mshauri wake muhtasi kuhusu Afrika, Salman al-Hirif. Kadhalika, alikuwa na usuhuba na viongozi kadhaa wa Kiafrika. Akisikilizana na Nelson Mandela, Mwalimu Julius Nyerere pamoja na mrithi wake Rais Ali Hassan Mwinyi na pia Ahmed Abdallah, aliyekuwa Rais wa Comoro.

Arafat aliwahi kuzizuru Afrika Kusini, Tanzania na Comoro, ingawa Comoro hakulala kwa sababu ya usalama wake. Wakati huo, Comoro ilikuwa ikidhibitiwa na mamluki wa Kizungu waliomrejesha madarakani Abdallah ambaye baadaye walimuua.

Nilipokuwa Ramallah nililizuru kaburi lake Arafat. Kuvuka Ufukwe wa Magharibi na kuingia Israel si rahisi kwa Wapalestina. Kuna vizuizi vingi vya barabarani na wanajeshi wa Israeli wanaovisimamia hawana huruma na Wapalestina. Kazi yao kubwa ni kuwanyanyasa.

Wanyanyasaji ni vitoto vidogo utafikiri vina umri wa miaka 16. Lakini wana silaha nzito na ndimi zao zimejaa kiburi na ufedhuli. Kwa hivyo, ‘vijanajeshi’ hivyo vinakuwa mabwana — ingawa wengine ni wasichana — na ukiwa Mpalestina hukuona kinyangarika tu.

Niliyaona mengi Israeli. Nilizifuata nyayo za Nabii Issa (Yesu Kristo), nikatembea kwenye Mji Mkongwe wa Quds (Jerusalem), nikasali Ijumaa mbili kwenye msikiti wa Al Aqsa. Kiguu na njia nikaizuru miji ya Tel Aviv, Jaffa, Sderot na Be’er Sheva ulio katika Jangwa la Negev.

Israeli ni nchi ya kuta, vizuizi, vikwazo, vipingamizi na vikaratasi vya ruhusa na vibali vya kila aina wanavyotakiwa Wapalestina wawe navyo. Daima wanadhalilishwa kwa kila namna ya idhilali. Nyumba zao zinabomolewa, wanafukuzwa makwao na lengo la Wazayoni jijini Jerusalem ni kuufanya mji mzima uwe na sura ya Kiyahudi.

Waarabu hawaruhusiwi kujenga katika Jerusalem ya Magharibi kwa Wayahudi lakini Wayahudi wanaruhusiwa kujenga Jerusalem ya Mashariki kwa Waarabu.

Siku moja nilialikwa kwenye Bunge la Israel, Knesset, na Dakta Dov Khenin, aliyekuwa Mbunge wa chama cha Hadash, chama pekee cha Wayahudi na Waarabu na ambacho ni cha mrengo wa kushoto. Khenin alikuwa pia mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha Israeli, Maki.

Ofisini mwake Khenin alitundika picha ya Che Guevara, mwanamapinduzi mzalia wa Argentina aliyeshiriki kwenye mapinduzi ya Cuba. Nilipomwambia kwamba tathmini yake ya mustakbali wa mgogoro wa Israeli na Wapalestina inakosa rajua, kwa vile inayaona mambo yote kuwa yasiyo na mbele wala nyuma, alinijibu kwa kumnukuu mwanafalsafa wa Kimarx wa Kitaliana, Antonio Gramsci.

Alinikumbusha kwamba Gramsci aliwahi kuandika kwamba alikuwa hana ‘rajua ya akili, lakini alikuwa na dhamira ya kutegemea mema’ (pessimist of the intellect, optimist of the will). Ukosefu wa rajua ni kichocheo cha kuchukuwa hatua, na msimamo wa kutarajia mazuri ni ukakamavu wa kuamini kwamba hatua hiyo italeta mageuzi ya maana hata pakiwa na nakama.

Khenin alinisikitikia kwamba ubovu wa Israeli ni kuwa Waarabu na Wayahudi hawalingani kwa lolote. Jamii zao zimegawika vibaya. Hajakusudia Wapalestina na Wayahudi lakini Waarabu wa Israel na Wayahudi wao.

Si tu kwamba Waarabu na Wayahudi wanazungumza lugha tofauti lakini hata misamiati yao ni tofauti na dhana (concepts) zao ni tofauti — katika siasa, utamaduni, na katika maingiliano yao ya kijamii ambayo ni madogo mno na kwa namna wanavyoangaliana, kwa kuchujana.

Jamii zote mbili zinaogopana. Wayahudi wana hofu na Waarabu; Waarabu nao wanawaogopa Wayahudi. Lakini alitaka nitambuwe kwamba ‘Israeli sio tu pahala ambapo matatizo hukutana lakini pia ni pahala penye uwezekano mwingi,’ yaani mengi yanaweza kufanywa.

Hamna shaka kwamba hii ni saa ya giza katika Israeli. Ni wakati ambapo mengi yanaweza kufanywa, na lazima yafanywe, ili eneo zima la Mashariki ya Kati liwe na amani. La kwanza ni kuufumua mfumo mzima wa kikabila na ubaguzi uliotamalaki katika taifa hilo.

Dhana kama ‘demokrasia’ na ‘uhuru’ au ‘ukombozi’ zimekuwa zikitumiwa vibaya na wanasiasa wa Kizayoni. Wanazitumia kwa maslahi ya kikabila — kabila la Wayahudi. Lakini kuna tatizo: Wayahudi wengi wanazidi kupaza sauti zao kuwapinga Wazayoni, wakihoji kwamba imani za Kizayoni, zikiwa pamoja na kuundwa kwa dola la Israeli na misingi yake ya kikaburu, zinakwenda kinyume na dini yao na ni ukoloni wa Kizayoni. Uzayoni wenyewe nao ni itikadi ya ubaguzi wa kikabila.

Sauti hizo za Wayahudi zinapazwa sambamba na zile zinazotaka Wapalestina warejeshewe haki zao na demokrasia halisi isimamishwe Israel.

Ahmed Rajab ni mwandishi wa kimataifa na mchambuzi. §§§§§§§§§London, Postgraduate Diploma (Urbanisation in Developing Countries) kutoka University College, London na shahada ya MA (African Political Economy na Modern African Literature) kutoka Chuo Kikuu cha Sussex.

Gazeti la Dunia ni Jukwaa Huru la Fikra kwa wasomaji wa lugha ya Kiswahili lenye lengo la kuchapa makala za kichambuzi kuhusu masuala mbalimbali muhimu kwa Tanzania, Afrika na Dunia kwa ujumla. Waandishi wa kwenye jukwaa hili ni maveterani na wabobezi kwenye maeneo watakayokuwa wanaandikia. Kama unajua unachokiandika, hili ni jukwaa lako.

Makala hii inatia huruma sana kuona karne hii ktk uso wa dunia bado kuna kipande kinatawaliwa kikaburu. Lakini makala haikuelezea chanzo cha tatizo la ni kwanini Wayaudi walifikia hiyo hatua.

Pamoja na kwamba ndugu Hamid umekuwa mwangalifu sana kuonyesha uungwana wa Waarabu hadi Yasser Arafat kumuoa Mkiristo (ili kuonyesa kwa Muislam dini si tatizo) lakini haiondoi ukweli kwamba walioanza kuwabaguwa Wayaudi ni Waarabu wenyewe kwa misingi ya kidini (hapa sitajadili kilichotokea Wayaudi walivyo ondoka na kurejea tena ktk eneo hilo). Wapalestina kwa pamoja na Waarabu hawakutaka kabisa kuanzishwa kwa taifa la Israeli.

Mgogoro wa Mashariki ya kati haujaanza leo wala jana. Tutazunguka kwa makala ndefu, lakini ukweli mzima umeandikwa kwenye vitabu vya dini, kwenye Tora na biblia. Sijuhi kilichoandikwa kwenye msaafu lakini najua Jerusalem ni eneo la tatu takatifu kwa wale wenye Imani ya dini ya kiislam.

Palestina ya leo ndilo eneo lililokuwa likijulikana kama Yudea na lilikuwa eneo la Wayaudi enzi za utawala wa Warumi. Jerusalem yenyewe ndiyo kulikuwa na hekalu la Wayaudi miaka mingi kabla ya kuzaliwa mtume Mohamed (kumbukeni mtume Mohamed alikuja miaka 500 baada ya Yesu), na kipindi Yesu anazaliwa hekalu lilikuwepo. Eneo hili limepitia tawala mbalimbali basi tuache yaliyoandikwa kwenye vitabu vya dini, eneo limetawaliwa na Warumi, Ottoman na Waingereza kwa nyakati tofauti.

Kwa kifupi, kinachotokea Mashariki ya kati si haki kurushia lawama upande mmoja. Ni swala tu la nani mwenye nguvu na timing. Wayaudi hawako tayari kuachia taifa lao tena hasa wakikumbuka kilichowatokea kwa Hitler wakati wa vita ya 2 ya dunia. Wayaudi million 6 kwa uchache waliuwa.
 
Hata mimi ningebagua mamtu yenye Roho ya kinyama,limtu linaamka tu kwenda kuvamia,kuua,kuteka na kujeruhi,hayavumiliki
 
Ahmed Rajab yupo very biased. Nilimsikiliza BBC nikamvua maana.
 
Makala hii inatia huruma sana kuona karne hii ktk uso wa dunia bado kuna kipande kinatawaliwa kikaburu. Lakini makala haikuelezea chanzo cha tatizo la ni kwanini Wayaudi walifikia hiyo hatua.

Pamoja na kwamba ndugu Hamid umekuwa mwangalifu sana kuonyesha uungwana wa Waarabu hadi Yasser Arafat kumuoa Mkiristo (ili kuonyesa kwa Muislam dini si tatizo) lakini haiondoi ukweli kwamba walioanza kuwabaguwa Wayaudi ni Waarabu wenyewe kwa misingi ya kidini (hapa sitajadili kilichotokea Wayaudi walivyo ondoka na kurejea tena ktk eneo hilo). Wapalestina kwa pamoja na Waarabu hawakutaka kabisa kuanzishwa kwa taifa la Israeli.

Mgogoro wa Mashariki ya kati haujaanza leo wala jana. Tutazunguka kwa makala ndefu, lakini ukweli mzima umeandikwa kwenye vitabu vya dini, kwenye Tora na biblia. Sijuhi kilichoandikwa kwenye msaafu lakini najua Jerusalem ni eneo la tatu takatifu kwa wale wenye Imani ya dini ya kiislam.

Palestina ya leo ndilo eneo lililokuwa likijulikana kama Yudea na lilikuwa eneo la Wayaudi enzi za utawala wa Warumi. Jerusalem yenyewe ndiyo kulikuwa na hekalu la Wayaudi miaka mingi kabla ya kuzaliwa mtume Mohamed (kumbukeni mtume Mohamed alikuja miaka 500 baada ya Yesu), na kipindi Yesu anazaliwa hekalu lilikuwepo. Eneo hili limepitia tawala mbalimbali basi tuache yaliyoandikwa kwenye vitabu vya dini, eneo limetawaliwa na Warumi, Ottoman na Waingereza kwa nyakati tofauti.

Kwa kifupi, kinachotokea Mashariki ya kati si haki kurushia lawama upande mmoja. Ni swala tu la nani mwenye nguvu na timing. Wayaudi hawako tayari kuachia taifa lao tena hasa wakikumbuka kilichowatokea kwa Hitler wakati wa vita ya 2 ya dunia. Wayaudi million 6 kwa uchache waliuwa.
Bahati mbaya sana hakuna utashi wa dhati wa kutatua hili tatizo la Israel na Palestine. Ni suala tu la kuangalia mipaka ya 1948 ilikuwaje, then Israel ina-exist kivyake na Palestine kivyao. Suluhu hapa ni sheria za kimataifa na sio hizi habari za dini zinasemaje.
 
Back
Top Bottom