Ujasiri unaanzia shuleni (sekondari, vyuoni)

conductor

JF-Expert Member
May 29, 2013
718
570
Mchawi wa kwanza kumtafuta na kumuua ni yule aliyetufundisha WOGA, aliyefanikisha kuturubuni kuacha kugoma mashuleni na vyuoni kama njia ya kuonyesha isia zetu na nguvu ya kujenga HOJA.

Vyuo vyetu kufunikwa na wanasiasa katika kuweka viongoz wao kwenye vyeo vya hatua ya kichuo, lakini pia viongoz wenyewe kukubari kuwa Chini ya mwavuli wa chama flani kama Sehem yakujitengenezea Ajira ya kisiasa.

Vijana wa leo wamekuwa dhaifu kusimama kukwepa upuuzi na ujinga wa kuishi kwa matakwa ya wanasiasa na NGO badala ya kuwa na mtazamo kuisogeza nchi mbele, huwez pata mwanajeshi imara,polisi imara,mwalim imara atakayetengeneza kizaz imara leo kwa kuwatoa vyuoni,na ndo janga tunalioona leo mashoga na madawa ya kulevya na kuvaa sandose za kichina (openi shoez kwa lecture rooms afu huyo huyo umwambie avae buti la kivita mwezi mzima porini (KAZI Leo kuwapata)

Shule niliyosoma uko o _level mwizi asingekatiza kuiba Mali za shule, labda awe ni mwanfunzi mwenyewe,maana akitokea akatoka nje vijij vyote vya Karib vitavamiwa na tutahakikisha wao wanamtaja ALIYE na tabia ya kuiba, siku moja ilitokea majambazi waka iba tyre za gari la headmaster (pick up) ,saa nane usiku, walivyomaliza kuiba tu headmaster alipiga filimbi kuita wanafunzi ,siku hiyo SAA nane na nusu usiku (enzi za chupi zinaitwa TAJIRI na VIP)vijana kila mmoja aliamka kibabe wengine chupi zimechanika makalion hata hivyo tulivamia mapori yoote tulitembea kilometres 16 kutafuta wezi, karibu vijij 7 tulikatiza, ilipofika saa 12 ndo tunastuka wengine tuko vifua wazi,peku,na vyuoni chup vya kiume, yaan mwingine chupi ni lile kaptura la darasa la saba alilovaa kumaliza mtihan Ila limeishachoka, hata hivyo tulirudi na tyre la mkuu wa chuo, leo eti shule ina walinz wa FFU,NA POLICE kulinda gate entrance, (ujinga huu) wanafunzi ndo jeshi lenyewe.

Vyuoni leo kijana hata ukimwona hana moral courage ya kujenga nchi kalegea utadhan kalazimishwa, Leo udsm na kwingneko palikuwepo sehem maalum ya kuleta hoja (mdegree -pe UDSM) prison square kule nchini Norway, na vyuo vingine Raisi wa chuo akisema tukutane pale jua bila majibu hatutoki hapo, nakumbuka kipindi flan bodi ya mikopo ilikuwa MSASANI (TILDO), kabla hawajaleta hizo issue za percentage kwa wanafunz, licha ya engineering tulikuwa hatuna hizo conditions za kipuuzi ukipata chuo unapata full accomodation. wakati huo huo ndo enzi wanaanza kuleta utaratibu wa kutoa mkopo Kwa mashart ya lazma uwe yatima, umesoma kayumba, nk.

Vijana hususani waliokuwa wanapata full tuliongoza msafara kwenda bodi kutetea wanfunzi wenzetu wasio na mkopo wakati kabisa sis wenyewe tunajuana ugumu uliopo kuishi na njaa na tunatokea mikoa mmoja, pale TIRDO lilikuwepo gate na mlinzi nje ili usingie, vijana tuliruka ukuta kuingia ndani wote kuonana na mkurugenzi ,wale walinzi wasingeweza kuzuia ile mass ya wanfunz strong, na hii ilitokana na mashairi mabovu ya awakurugenzi wa mikopo kuleta siasa kwenye Elimu, alijikuta nyomi nzima iko mapokez si alitoka kutoa kauli ili wenzetu wapate pesa ya kujikimu,(na akizengua anajua kiti chake cha moto)

Mawaziri wa chuo walikula vyiapo vya kweli kwa wanafunzi ukizengua ukala nje ya mipaka yako au kuleta upuuzi, moto utaupata, yupo Wazir wa mkopo alianza kuleta upuuz kila mda anaongea na utawala, siku moja tukamwambia usipoleta majib ya kwel kesho utakuta CHUMBA chako kiko tupu, na kweli aliporejea na uswahili wake alikuta kila kitu nje na nguo zake zimelowa.

Ndoto ya mwanafunz ilikuwa kuwa bora kwenye carrier yake leo mwanfunz anasoma huku akitamani kuwa miss, sijuh msanii, sijuh, mhubir...(shit), kama ni law anajua soko linaitaji nini, wale waliosoma education walikuwa moto wa kuanzisha MIGOMO, huku engineering tukipanga siraha za kushinda wanasiasa wapuuz, hata waliokuwa wenyewe wa vyuo walijisikia fahari kuwa na vijana wa kutetea chuo,shule, nakumbuka mashindano ya michezo ukifungwa na chuo, shule flani basi nawe shinda Kwa kumtwanga mpinzani ngumi mnapigana kweli kweli, leo eti ili ushinde au ufanye KAZI Kwa bidii uwanjan eti zawadi ya 5m, (alafu wewe mchezaji unajioona mzalendo) sioni mantiki mantiki, tusi hilo, (mwanangu kula nitakupeleka Jim, nitakununulia simu ukishinda mtihani, (wazaz wanamna hii nikiwa kiongozi namfunga kwa kulawit mtoto kisaikolojia, mimi mzee wangu alikuwa akisema mwanangu sina pesa nauza mbuzi,mti ili uende shule ila uridh sahau tafuta vyako maana umenifili, unasema ndio Baba/mama.

Leo single maza ndo watoa kauli, afu unategemea taifa liwe na msimamo mmoja (national culture), Wale tuliosoma boys, tulikuwa tukienda michezo uko nje, hizi co school zikitushinda vita kubwa na ikibid hata wasichana wao huwez kuwatongoza,hivyo shule lazma ipambane usishindwe na shule za mchanganyiko (waweka blue kwenye shati), tuliishi kama BOB JUNIOR na BOB KILER huna kipaji tafuta kipaji leo hii vinaja wanavaa short pence kama fashion nakuonyesha ngoz ilivyo nyororo, hao ndo waende Shambani kulima (hii miradi ya SSH na bwana BASHE),wataweza au wataleta vingeleza vyao kwenye UCHAVUSHAJI, kilimo kinafindishwa? Au kukusanya data nakuziweka kwenye soft ware ulizotoa Kwa Mzee ITIRIMBI mwenye miaka 92, mwenye historia ya pamba na mahindi ndo unatuletea hapa?

Unaacha specialization unachukua mvuvi wa NYASA aende SINGIDA kulima vitunguu ataweza? kisa tu ni kada wa CHAMA flani na baba yake alifia chama kwakutoa ardhi kujenga ofisi alafu kesho unalalamikia nchi kuwa na mashoga?

USA wenyewe ukienda Sehem za viwanda kama TEXAS unakuta jamaa kutoka mexco anajua kuminyima batton ya on/off Tu kwenye komputa ila anajua kukunja NONDO, kutengeza injin na darasa hajawah kaa na analipwa mshahara mkubwa kuliko manager wa kampuni sasa mletee stor za mimi msomi anakulamba bis bis ya kichwa kwani anaamin yeye ndo anakuweka kitini pale cha kuzunguka, leo afisa mkopo bongo anayezunguka mji mzima akitafuta wateja analipwa laki 3, alafu huyo HR wa mchongo na mpuuzi Tu analipwa 1.5m analeta na majigambo kibao mtaani, (hii yote inatokana na udictator wa kisiasa (politics is just entity it belongs to certain groups of common interest and earnings) we leo unajivisha ukada usiokupa tija, TZ ni kati ya nchi inayomilik mazao yoote duniani, wakati nchi nyingine zina zao moja na limeawainua (Norway wavuvi) Japani wavuvi, china all weather kwasabab ya population, ndo maana wanakuja africa, Scandinavia countries wakulima na shule kichwan) leo sis huku eti mwamba mmoja anakuja kuangazia masuala ya kuongezeka kwa vijana AFRICA (why?)

Yaani sis ni kama MKE wa Bob junior ukishinda njoo unichukue (shit mind) eti mrusi anarud Africa, USA anakuja africa Sisi tumejipangaje (wajane wa matokeo mabovu ya misingi isiyo imara vyuoni na kozi za umagharib).

Ukimuuliza mwanafunz wa leo swali hili " Kama usingebatika kusoma ungekuwa Nani?" Jamani maj bu atakalo kupa kama ni mzazi na uhakika utajua unavyopoteza pesa, si ajabu aka kwambia diamond, au posh queen au Mayele, alafu anayesoma tourism anakwambia field zake zote ni kariakoo.

Ngoja nipumzike Kwanza kidogo nasikia kuna MTU anaongea vingeleza vyake huko nje si ajabu ni wale wakusanya TAKATAKA kutoka manispaa, ambapo ili ushinde deal hilo kuwa Kada wa chama.

Jipime wewe unaesoma article hii uko wapi katika nchi hii.

Unafaa wapi kama usingepelekwa shule hizi za mchongo (mwalim yule Yule kama asingesoma angekuwa mkulima mkubwa leo anafundisha political science).

IMG-20230327-WA0013.jpg
IMG-20230327-WA0011.jpg
image_01c14373-8537-4710-87d2-a2dce71ccce720230325_224255.jpg
 
Mchawi wa kwanza kumtafuta na kumuua ni yule aliyetufundisha WOGA,aliyefanikisha kuturubuni kuacha kugoma mashuleni...
Nimesoma juu kichwa cha habari pekee na maneno ya mwanzoni ila kwa bahati mbaya nimeshindwa kusoma zaidi andiko lako.

Tafadhali edit andiko lako kwa kuweka aya ili tupate urahisi wa kusoma 👏🏿👏🏿
 
Mkuu ungeacha aya kwenye kuandika sema ngoja nisome

Oook nimekupata mkuu upo sahihi walimu uoga wameanzia vyuoni huko
 
Umasikin unafanya watu kuwa waoga na wanyonge mkuu ...

Leo hii unatoka kijijin huko ndani ndani wazazi hawana mbele wala nyuma,hata nauli ya kwenda chuo wameuza mbuzi unafika chuo udsm unapata mkopo asilimia 60 unagoma unataka kuingia barabarani kutaka asilimia 100, hio nguvu unaitoa wapi ? .....kwanza unakuta hata hio asilimia 60 ukoo mzima hawana uwezo wa kuipata Kwa jembe lao la mkono , hata wakiuza mbuzi na mali zote ...

UMASIKIN NI KITU KIBAYA SANA ...!!
 
Umasikin unafanya watu kuwa waoga na wanyonge mkuu ...

Leo hii unatoka kijijin huko ndani ndani wazazi hawana mbele wala nyuma,hata nauli ya kwenda chuo wameuza mbuzi unafika chuo udsm unapata mkopo asilimia 60 unagoma unataka kuingia barabarani kutaka asilimia 100, hio nguvu unaitoa wapi ? .....kwanza unakuta hata hio asilimia 60 ukoo mzima hawana uwezo wa kuipata Kwa jembe lao la mkono , hata wakiuza mbuzi na mali zote ...

UMASIKIN NI KITU KIBAYA SANA ...!!
Hapo umeona tatizo lilipo mkuu.
 
Back
Top Bottom