Zimwi la 'Udini' na utangamano wa Tanzania yetu

Apr 8, 2023
26
17
Ni maoni yangu kwamba mazimwi matatu yanayouzinga utawala wa awamu ya sita ni (Ukabila) Uzanzibari na Utanganyika, Udini na Jinsia kuliko ilivyo maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Kama ilivyo kwa "mazimwi" ni aghalabu kuzungumzwa kwa sababu ya hofu ya mazimwi yenyewe kujitokeza hadharani na kusababisha sintofahamu, kwa hiyo mara nyingi jamii hujifanya ama kutoamini juu ya uwapo wa mazimwi yenyewe, ama hujifanya kudharau habari za uwapo wake kwa kuita wazo hilo kuwa "hadithi za kizee", hata hivyo mazimwi haya matatu ni hai na kuyazungumzia ni njia pekee ya kuyakabili na hivyo, wacha walau niseme mojawapo kwenye makala haya.

Udini! Jeshi la Polisi huko Zanzibar limewakamata watu kadhaa kwa kosa la "kula adharani" wakati wa Ramadhani na vyombo vya habari zimeandika juu ya hili, na sijaona popote wanaharaka, wanazuoni na wasomi wetu wakisema chochote, hasa katika zama zinazojitanabaisha na "Demokrasia na Utawala wa Sheria".

Hii ni aibu, tena ni aibu kubwa siyo tu kwa Wasomi wa Sheria nchini, Watendaji ndani ya Jeshi la Polisi, Wanazuoni na Wanaharakati wote wa kijamii, Wanachama na mashabiki wa chama kinachotawala, na wasifiaji wa Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi yetu, bali ni aibu kwa Rais wetu ambaye alionekana mbele ya vyombo vya habari akipana mkono na Mkuu wa Kanisa Katoliki Ulimwenguni kwenye ziara maalumu huko Vatican kumaanisha Rais huyu Muislamu, anasimamia misingi ya katiba na sheria inayotambua Tanzania kuwa taifa lisilo na dini ya taifa, ingawa watu wake wanazo dini zao, yeye ni mlinzi wa haki za watu wa dini zote katika taifa letu. Hii ni aibu kubwa.

Kukamatwa kwa kula adharani!!? Hili linakumbusha miaka kadha nyuma wakati watu walipojichukulia sheria mkononi na kuwatandika bakora mabinti na wanawake walioonekana kutembea mitaa ya Zanzibar wakiwa wamevalia "nguo fupi" a.k.a "Nusu uchi" na linaibua hoja mbili kubwa:- Je Zanzibar ni Sehemu ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na hivyo inatawaliwa Kidemokrasia na siyo Kitheoklasia!!? Je Zanzibar (nje ya Muungano) ni nchi ya Kitheoklasia!!? Je kwa Jeshi la Polisi kuwakamata watu kwa kosa la "kula adharani" wakati wa Ramadhani" linatekeleza sheria za Taifa lipi!!?

Sasa tunajua kwamba mahusiano ya Kanisa (hasa kanisa Katoliki) na Serikali ya awamu ya sita baada ya mkataba wa DP World (kati ya mambo mengine)yaliingia mushkeri baada ya kanisa kutangaza rasmi kutotaka kuunga mkono mkataba huo, na hata kujitokeza hadharani na kusema Askofu aliyeonekana kwenye utiaji saini mkataba huo "aliingizwa mkenge" kwa kualikwa Ikulu pasina kujua alikuwa akialikwa kufanya nini, hivyo haikushangaza pale ambapo kwa maneno ya Waziri wa mambo ya nje "ilichukua muda mfupi "kukamilisha utaratibu wa mwaliko" wa Rais wetu huko Vatican na wataalamu wa PR tukalisifu (wengine wazi na wengine kimyakimya) jambo hili kama moja ya PR muhimu kujaribu kujenga mahusiano mema kati ya Serikali na Kanisa Katoliki. Kwa hiyo wakati moja ya vyombo vya dola (government instruments of power) vinaposigina haki za watu kwa misingi ya imani za dini na kuwataka ama wafunge au wale kwa siri kwa vile tu ni Ramadhani, na kisha kila mtu akajifanya hajaona kasoro kwenye hili ni aibu kubwa.

Mimi ni moja ya watu wanajivunia kuwa Mtanzania, na Mzanzibari mkaazi walau kwa vile nimetumia Sehemu ya maisha yangu Zanzibar. Miaka ya tisini nikiwa mwanafunzi pale Nyuki Sekondari niliingia mara mbili kwenye ugomvi na rafiki zangu pale Michenzani tulipokuwa tukiishi wakati huo. Moja ni pale alipopigwa mdogo wangu na wanafunzi wenzake pale Skuli Kisiwandui baada ya "kula adharani" wakati wa Ramadhani. Baba yetu alikuwa amesafiri kwenda bara lakini aliporudi nyumbani mdogo wangu akilia kwamba kapigwa na mwalimu kaona, nilikwenda shuleni na kudai haki ya mdogo wangu na busara ya mwalimu ikamuongoza kuwaadhibu waliompiga ingawa alitushauri pia mimi na mdogo wangu kujifunza "ustahimilivu wa kidini" ili kuishi kwa amani kati ya ndugu zetu wazanzibari. Mara ya pili ni pale nilipofikishwa kituo cha polisi Madema kwa kumtwanga ndoo mmoja wa Rafiki yangu aliyenipokonya mkate na kuutupia jalalani huku akiusindikiza na "Istighfar" (nadhani akiniombea miye ) kwa ati mimi kutembea na chakula adharani wakati wa ramadhani, mimi nilichoona siyo dini, bali kufuru na dharau kwa mwanaume kukidharau chakula changu, na mbaya zaidi alikuwa rafiki na mwanafunzi mwenzangu, nikamtwanga ndoo akazimia, (nadhani mchanganyiko wa ndoo ya kondoo na njaa ya mfungo). Aliyeumaliza ugomvi ule alikuwa mzee Marini Hassan(Marehemu sasa) aliyekuwa amekuja Michenzani kumuona mtangazaji mwenzie "Uncle Saleh" aliyekuwa akiishi hapo. Najiuliza, baada ya miaka mingi yote hii, bado ubaguzi wa kidini unaendelea Zanzibar!!? Najiuliza, ubaguzi huu unafanywa dhidi ya Wakristo tu, tena weusi maana sina hakika kama yumo mzungu kati ya waliokamatwa.

Kwa makala haya, nashauri CCM kupitia msemaji wake iwe na kauli kwa watanzania kuhusu uheshimu wa katiba na sheria zetu, na pia Serikali iwawajibishe watendaji wa jeshi lake kwa kukosa busara ya kuheshimu hisia za waliofunga huku wakilinda haki za walao maana ndiyo hasa tafsiri ya 'weledi'. Kama Polisi inakamata watu kwa makosa yasiyo jinai (najua watajitetea na "disorderly misconduct" lakini bado hili haliswihi hata katika sheria hiyo), watafanya nini ikiwa watakwaza wazanzibari na mtu anayebeba Biblia akapita mitaani kwenda Kanisani, tena akiimba Tenzi za rohoni!!? Uvumilivu wa kidini ni uvumilivu na uvumilivu hauhitajiki kama hakuna kero ama maumivu kama ambavyo dawa haihitajiki kama hakuna maladhi, tustahamiliane, tusilazimishane kwa mabavu ya kisheria.
 
Rais wa Zanzibar aliwahi kusema kuwa atashauriana na mwenzake rais wa Tanzania waanzishe mfuko wa hija ambao utawawezesha waisilamu kwenda Maka.
 
Kwanza niongee jambo moja tu la msingi hili suala halina umuhimu kwa watanganyika kabisa kwa sababu ile ni jamii ina sheria zake kama mgeni fuata wanachotaka .

Mimi binafsi nilipangiwa vituo vya kazi mikoa miwili yenye wakristo wengi ,plus tetesi wa washkaji nikaomba nihamishwe maana jamaa yangu alishawahi kuishi huko anasema na akivaa kanzu anaitwa mchawi .

Nimeona kuhamishwa mara mbili ,kwa vile naamini kila mtu na tamaduni zake ,ni mambo ya kupita tu.

Zanzibar wanafanya hivyo pia ni kisiwa kilichopokwa na Nyerere kwa sababu za kiusalama ila haikuwa sawa kabisa..Ni bora kukubali wale ni watu wengine kuliko kutafuta haki kweny nchi ya mtu ,kama polisi wanafanya basi serikali yao imeridhia .

kitu kibaya👉 Sio Zanzibar bali ni chuki ambazo wamefanya zenji tena kiongozi anasambaza video ya miaka 6 nyuma ,hata mkipigana vita kama Kenya mwaka 2007 mwishoe mtahesabu hasata na casualties halafu mtajiona wajinga ,maana kila mtu ataendelea kuwa na msimamo wake.

Inakuwaje mtu anatweet kututkana waislamu wotu ,matusi ya nguoni kule "X" ebu chukulia kipigo cha pale kina shida gani ? Mpaka watu kuja juu na ni miaka 6 sita nyuma hata videoa ilisambaa sana !?

Tumieni akili hakuna mtu anaweza kubadili tamaduni za mwingine ,bora mkadili na mambo mengine.

Ukiachana na zenji hapa bongo bado tunabaguana kwa makabila , mpaka watu wanaona wenzao hamnazo na majina mabya ,ukiwa na akili utajua utengano ni asilia tangu mtu anazaliwa na hautoisha ... Jaribu kwenda kenya wale wengi ni wakristo ila kaangalie ukabila upo kiwango gani ,jaribu kuendana na jamii ya watu wengi wanaofuata sheria zao ningekemea kama ingetokea bongo ila huko hata wao wamebariki.
 
Back
Top Bottom