Hatma ya Dkt. Slaa, Wakili Mwabukusi na Mdude bado Giza Totoro

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
1692163131269.png

Wakati Jeshi la Polisi likiendelea kuwashilia wanasiasa Dk Willibrod Slaa na Mpaluka Nyangali maarufu ‘Mdude’ na mwanasheria Boniface Mwabukusi, mawakili wao wamedai kuwa wateja wao wamehojiwa kwa tuhuma za uhaini.

Kufuatia madai hayo, baadhi ya wanasheria nchini wamezungumzia hatua hiyo wakichambua maana na hatima ya mtu anayetuhumiwa kwa kosa hilo, endapo atapatikana na hatia.

Pia, wengine wamelitaka jeshi hilo kutenda haki ikiwemo kuwapa watuhumiwa kupata fursa kuonana na mawakili wao na kupelekwa mahakamani kwa wakati baada ya kujiridhisha na suala hilo, kwa kuwa si kosa dogo.

Hata hivyo, Jeshi la Polisi halijatoa taarifa mpya kuhusu tuhuma zinazowabili watu hao, zaidi ya zile za awali zilizohusu kauli za uchochezi.

Mwabukusi aliyekuwa akiongoza jopo la mawakili katika kesi ya kupinga mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kati ya Serikali ya Tanzania na ya Dubai (IGA) pamoja na Mdude walikamatwa Agosti 11 mkoani Morogoro, saa 8:30 usiku.

Wawili hao walikuwa pamoja na Katibu wa Chadema Kanda ya Kati, Emmanuel Masonga ambaye hata hivyo aliachiwa asubuhi Agosti 11.

Mwabukusi na Mdude walirejeshwe jijini Mbeya wanakoshikiliwa Kituo Kikuu cha Polisi mkoani humo huku Balozi Slaa aliyekamatwa nyumbani kwake Dar es Salaam, anashikiliwa katika Kituo cha Polisi Oysterbay (mpaka Agosti 14).

Agosti 11 mwaka huu, taarifa kwa umma iliyotolewa na msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime ilisema wanafuatilia watuhumiwa walioandaa na kutoa maneno ya kichochezi, akisema kati yao tayari wanashikilia Mwabukusi na Mdude kwa mahojiano.

Siku moja kabla ya Misime kueleza hayo, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Camillius Wambura alikutana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kutoa onyo kwa watu aliosema wamepanga maandano ya kuiangusha Serikali kabla ya mwaka 2025, akiwataka wasitingishe kiberiti.

IGP Wambura alidai kundi hilo linahusisha maandamano hayo na kushawishi Watanzania kuwaunga mkono na hoja zinazoendelea za bandari.

"Tuliamini hoja za bandari zinajibiwa kwa hoja, tukaamini baadhi ya watu walikwenda mahakamani basi wangeheshimu uamuzi wa mhimili huo, lakini badala yake wametoka na kutafuta ushawishi wa kuwachochea Watanzania kuwaunga mkono,” alisema.

"Mmoja amekwenda mbali zaidi na kusema watahakikisha wanaiangusha Selikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kabla ya mwaka 2025. Nimewaita hapa kuwaambia wakome kabisa na kusitisha matamshi yao ya kichochezi na tutawachukulia hatua za kisheria," alisisitiza IGP Wambura.

Wanatuhumiwa uhaini

Wakili Dickson Matata anayemtetea aliyewahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Dk Slaa alidai jana kuwa mteja wake amepewa kesi ya uhaini na kuwa mwanasiasa huyo hakuwa tayari kutoa maelezo polisi badala yake atakwenda kuyatolewa mahakamani.

“Bado Dk Slaa hajatoa maelezo yoyote bali atayatoa mahakamani maana kosa lenyewe halina dhamana, kesho (leo) ndiyo tutajua kama watampeleka mahakamani au la,” alisema Matata.

Mwananchi lilimtafuta Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro kujua kinachoendelea dhidi ya Balozi Slaa akasema, “unataka niseme nini wakati kila kitu mmeshaandika. Mmeandika Dk Slaa naye atiwa mbaroni, unataka kujua kama anashikiliwa au hashikiliwi? Nakushukuru asante.”

Kwa upande wake Wakili Philipo Mwakilima anayewatetea Mdude na Mwabukusi, alisema wateja wake walihojiwa juzi kwa tuhuma za uhaini na kuwa hivi sasa wanaipa muda Serikali kuandaa mchakato wa kuwapeleka mahakamani, baada ya kuchukua maelezo yao.

“Tumewapa nafasi Serikali kuandaa hati ya mashtaka, kwa sababu ukishamaliza kuchukua maelezo ya mtuhumiwa jadala linatakiwa kwenda katika ofisi ya mwendesha mashtaka,” alisema.

Wakati mawakili wakisema hayo, jana kwa nyakati tofauti gazeti hili liliwatafuta Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime, IGP Wambura kwa simu zao za kiganjani bila mafanikio huku Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Ramadhan Kingai alipokea simu yake lakini hakuwa tayari kulizungumzia suala hilo.

Ni jambo linalotisha

Baada ya taarifa za kesi ya uhaini kusambaa, Wakili Frank Chundu akizungumza na gazeti hili alisema hilo ni jambo linalotisha, akisema mtu akikutwa anashtakiwa na uhaini lazima upate shida, kwa sababu si kosa jepesi kama ambavyo watu wanafikiria.

Chundu alisema ni kosa ambalo lazima kuwepo na kitu kikubwa kinafikirika cha mtu kutenda uhaini.

“Sasa haya maneno kama nitaandamana au nitafanya… sidhani labda tuseme sheria ilikusudia kwamba mtu akiongea haya basi ashtakiwe na uhaini. Kesi ya uhaini maana tunazungumzia kitu hatari kwa mamlaka ya Serikali au kuiondoa madarakani.

Wakili huyo alishauri Serikali kuangalia namna bora ya kushughulikia changamoto zinazojitokeza pasipo kutumia nguvu kubwa kwa wanaodaiwa kwenda kinyume.

“Kwa sababu kuna uhuru wa kuongea tuwaache wazungumze, lakini kuna namna ya kushughulika nao... Watu wakitoa malalamiko Serikali iwaite na kuzungumza nao na kuwasikiliza hoja zao, kwa sababu wote wana nia moja ya kuijenga Tanzania,” alisema.

Wakati Chundu akieleza hayo, Wakili mwingine Jebra Kambole alisema uhaini si kosa dogo, akisema halina dhamana na adhabu yake ni kunyongwa. Pia, alisema kosa hilo linatendwa dhidi ya Serikali si mtu binafsi au raia.

Kambole alisema uhaini ni kosa kubwa akitoa tahadhari kwa Serikali kuwa kabla ya haijachukua hatua dhidi ya watu wengine, ihakikishe inatenda haki kwa wanaowashikilia, ikiwemo kuwapa huduma zinazostahili.

“Kosa la uhaini kwa namna linavyoonekana kwa sasa wanalipotosha au wanalifanya lionekane la kawaida. Kosa ambalo ni ‘serious’ (kubwa) wanalifanya lionekane la kawaida kwa sababu wameshalizoea kulisikia,” alisema.

Akijadili zaidi kosa hilo, Profesa wa sheria, Abdallah Safari alisema kwa mujibu wa Sheria ya Kanuni ya Adhabu kifungu cha (39), chenye vifungu vidogo kuanzia vya moja hadi nne, mtu yeyote raia wa Tanzania akiwa na nia ya kumuua au kumjeruhi Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania anatenda uhaini.

Alisema vifungu hivyo pia vinazungumzia mtu akitaka kuipindua Serikali au kuchochea mambo kama hayo yafanyike, vyote vinahusisha na masuala ya makosa ya uhaini.

“Kwa tafsiri ya sheria ya kanuni ya adhabu (yote hayo) ni uhaini na adhabu yake ni mbaya sana yaani kunyongwa. Hili ni shtaka la juu kabisa katika makosa ya jinai,” alisema Profesa Safari.

Tafsiri ya Profesa Safari inaungwa mkono na Wakili Edson Kilatu akisema uhaini ni kosa pekee ambalo linatajwa kwenye Katiba moja kwa moja kuwa ndiyo kosa kubwa kuliko mengine na adhabu yake ni kifo na kwa mujibu wa kifungu cha 148 (5) cha Sheria ya Mwenendo wa Jinai Sura ya 20 halina dhamana.

“Kwa mujibu wa kifungu cha 39 cha Kanuni ya Adhabu uhaini umeainisha vitu vingi kwanza njama yoyote ya kutaka kumuua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na pili njama yoyote yakutaka kupindua Serikali.

“Jambo lingine linaloweza kuwa uhaini ni kitendo cha kuzuia majeshi kufanya majukumu yake ya kuilinda mipaka ya nchi kwa kusudio la kutaka Serikali ianguke na kushindwa kufanya majukumu yake,” alisema.

Kesi nyinginezo

Endapo kesi hii itafunguliwa itakuwa kwenye orodha ya nyingine kadhaa zilizowahi kuendeshwa kwa nyakati tofauti nchini.

Kati ya mwaka 1989 hadi 1991, aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad (marehemu) aliwekwa kizuizini kwa kosa la uhaini, lakini baadaye aliachiwa.

Kesi nyingine ni ya Khamis Ali Machano na wengine 17, wafuasi wa CUF walioshtakiwa kwa tuhuma za kutaka kupindua Serikali ya Mapinduzi Zanzibar chini ya Rais Salmin Amour.

Tuhuma hizo zilisababisha kufunguliwa kesi ya uhaini na kukaa gerezani miaka miwili na nusu.

Hata hivyo, mwaka 2000 Mahakama ya Rufaa Tanzania ilitamka kupitia hukumu yake kuwa uhaini usingeweza kutendekea Zanzibar kwa kuwa si dola bali ipo chini ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Vilevile, mwaka 1985 Watanzania 19 wakiwamo wanajeshi 14 walifikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya kula njama za kumpindua Rais wa Kwanza wa Tanzania, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

Baadhi yao waliachiwa huru na wengine kuhukumiwa kifungo cha maisha. Hata hivyo, mwaka 1995 waliachiwa huru na Rais Ali Hassan Mwinyi.

MWANANCHI

Habari zaidi, soma:
  1. Sakata la DP WORLD: Rais Samia asema Serikali itatafuta mbia wa kuiendesha bandari ya Dar, sasa kuchangia robo tatu ya bajeti ya nchi
 
Ajabu sana, mpaka leo siku ya tatu watuhumiwa bado hawajafikishwa mahakamani, sijui kitu gani kinachowachelewesha wale ambao tayari wameshatuonesha ushahidi wao wakutengeneza studio.
 
Kufuatia madai hayo, baadhi ya wanasheria nchini wamezungumzia hatua hiyo wakichambua maana na hatima ya mtu anayetuhumiwa kwa kosa hilo, endapo atapatikana na hatia.
Hizo ni mbinu tu za kuzima huu mjadala wa bandari, hakuna kesi ya maana hapo.

Vyombo vya dola hutumika kisiasa pale watawala wanapojaribu kuzima ukosoaji.
 
Ajabu sana, mpaka leo siku ya tatu watuhumiwa bado hawajafikishwa mahakamani, sijui kitu gani kinachowachelewesha wale ambao tayari wameshatuonesha ushahidi wao wakutengeneza studio.
Watu wenyewe sio wepesi, wajipange haswa, kama wanasheria wao ndio hao kazi wanayo
 
Sasa sijui kwanini hawawapandishi kizimbani wakati wwmeshawapa case ya uhaini?
 
Waangalie hiki kitu,
Wengine hapo wanatumia dawa za bp au za sukari pia.

Hivi Bwana akiamua yake huko huko kifungoni mtasema nini?
yaani watu wawe wanahurumiwa waseme watakavyoi kisa wanatumia dawa? ikitokea wametuacha itakuwa zimefika zao na hakuna mtu atalaumiwa maana hawatakuwa wameondoka kwa risasi wala kipigo
 
Watu wenyewe sio wepesi, wajipange haswa, kama wanasheria wao ndio hao kazi wanayo
hao ni wepesi sana tu tena hawana ujanja wowote sasa mdude naye anajifanya anajuwa sheria halafu anaropoka huyo mwambukusi sheria anajuwa halafu anasema wafanye mikutano na kuchopma vituo vya polisi balozi ndiyo mhaini kabisa maana yeye kasema serikali ipinduliwe mnawahurumia wanini sasa?
 
Kwani unadhani haiwezekani
Kupinduliwa ama kuchoma hivo vituo?
 
View attachment 2718692
Wakati Jeshi la Polisi likiendelea kuwashilia wanasiasa Dk Willibrod Slaa na Mpaluka Nyangali maarufu ‘Mdude’ na mwanasheria Boniface Mwabukusi, mawakili wao wamedai kuwa wateja wao wamehojiwa kwa tuhuma za uhaini.

Kufuatia madai hayo, baadhi ya wanasheria nchini wamezungumzia hatua hiyo wakichambua maana na hatima ya mtu anayetuhumiwa kwa kosa hilo, endapo atapatikana na hatia.

Pia, wengine wamelitaka jeshi hilo kutenda haki ikiwemo kuwapa watuhumiwa kupata fursa kuonana na mawakili wao na kupelekwa mahakamani kwa wakati baada ya kujiridhisha na suala hilo, kwa kuwa si kosa dogo.

Hata hivyo, Jeshi la Polisi halijatoa taarifa mpya kuhusu tuhuma zinazowabili watu hao, zaidi ya zile za awali zilizohusu kauli za uchochezi.

Mwabukusi aliyekuwa akiongoza jopo la mawakili katika kesi ya kupinga mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kati ya Serikali ya Tanzania na ya Dubai (IGA) pamoja na Mdude walikamatwa Agosti 11 mkoani Morogoro, saa 8:30 usiku.

Wawili hao walikuwa pamoja na Katibu wa Chadema Kanda ya Kati, Emmanuel Masonga ambaye hata hivyo aliachiwa asubuhi Agosti 11.

Mwabukusi na Mdude walirejeshwe jijini Mbeya wanakoshikiliwa Kituo Kikuu cha Polisi mkoani humo huku Balozi Slaa aliyekamatwa nyumbani kwake Dar es Salaam, anashikiliwa katika Kituo cha Polisi Oysterbay (mpaka Agosti 14).

Agosti 11 mwaka huu, taarifa kwa umma iliyotolewa na msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime ilisema wanafuatilia watuhumiwa walioandaa na kutoa maneno ya kichochezi, akisema kati yao tayari wanashikilia Mwabukusi na Mdude kwa mahojiano.

Siku moja kabla ya Misime kueleza hayo, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Camillius Wambura alikutana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kutoa onyo kwa watu aliosema wamepanga maandano ya kuiangusha Serikali kabla ya mwaka 2025, akiwataka wasitingishe kiberiti.

IGP Wambura alidai kundi hilo linahusisha maandamano hayo na kushawishi Watanzania kuwaunga mkono na hoja zinazoendelea za bandari.

"Tuliamini hoja za bandari zinajibiwa kwa hoja, tukaamini baadhi ya watu walikwenda mahakamani basi wangeheshimu uamuzi wa mhimili huo, lakini badala yake wametoka na kutafuta ushawishi wa kuwachochea Watanzania kuwaunga mkono,” alisema.

"Mmoja amekwenda mbali zaidi na kusema watahakikisha wanaiangusha Selikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kabla ya mwaka 2025. Nimewaita hapa kuwaambia wakome kabisa na kusitisha matamshi yao ya kichochezi na tutawachukulia hatua za kisheria," alisisitiza IGP Wambura.

Wanatuhumiwa uhaini

Wakili Dickson Matata anayemtetea aliyewahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Dk Slaa alidai jana kuwa mteja wake amepewa kesi ya uhaini na kuwa mwanasiasa huyo hakuwa tayari kutoa maelezo polisi badala yake atakwenda kuyatolewa mahakamani.

“Bado Dk Slaa hajatoa maelezo yoyote bali atayatoa mahakamani maana kosa lenyewe halina dhamana, kesho (leo) ndiyo tutajua kama watampeleka mahakamani au la,” alisema Matata.

Mwananchi lilimtafuta Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro kujua kinachoendelea dhidi ya Balozi Slaa akasema, “unataka niseme nini wakati kila kitu mmeshaandika. Mmeandika Dk Slaa naye atiwa mbaroni, unataka kujua kama anashikiliwa au hashikiliwi? Nakushukuru asante.”

Kwa upande wake Wakili Philipo Mwakilima anayewatetea Mdude na Mwabukusi, alisema wateja wake walihojiwa juzi kwa tuhuma za uhaini na kuwa hivi sasa wanaipa muda Serikali kuandaa mchakato wa kuwapeleka mahakamani, baada ya kuchukua maelezo yao.

“Tumewapa nafasi Serikali kuandaa hati ya mashtaka, kwa sababu ukishamaliza kuchukua maelezo ya mtuhumiwa jadala linatakiwa kwenda katika ofisi ya mwendesha mashtaka,” alisema.

Wakati mawakili wakisema hayo, jana kwa nyakati tofauti gazeti hili liliwatafuta Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime, IGP Wambura kwa simu zao za kiganjani bila mafanikio huku Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Ramadhan Kingai alipokea simu yake lakini hakuwa tayari kulizungumzia suala hilo.

Ni jambo linalotisha

Baada ya taarifa za kesi ya uhaini kusambaa, Wakili Frank Chundu akizungumza na gazeti hili alisema hilo ni jambo linalotisha, akisema mtu akikutwa anashtakiwa na uhaini lazima upate shida, kwa sababu si kosa jepesi kama ambavyo watu wanafikiria.

Chundu alisema ni kosa ambalo lazima kuwepo na kitu kikubwa kinafikirika cha mtu kutenda uhaini.

“Sasa haya maneno kama nitaandamana au nitafanya… sidhani labda tuseme sheria ilikusudia kwamba mtu akiongea haya basi ashtakiwe na uhaini. Kesi ya uhaini maana tunazungumzia kitu hatari kwa mamlaka ya Serikali au kuiondoa madarakani.

Wakili huyo alishauri Serikali kuangalia namna bora ya kushughulikia changamoto zinazojitokeza pasipo kutumia nguvu kubwa kwa wanaodaiwa kwenda kinyume.

“Kwa sababu kuna uhuru wa kuongea tuwaache wazungumze, lakini kuna namna ya kushughulika nao... Watu wakitoa malalamiko Serikali iwaite na kuzungumza nao na kuwasikiliza hoja zao, kwa sababu wote wana nia moja ya kuijenga Tanzania,” alisema.

Wakati Chundu akieleza hayo, Wakili mwingine Jebra Kambole alisema uhaini si kosa dogo, akisema halina dhamana na adhabu yake ni kunyongwa. Pia, alisema kosa hilo linatendwa dhidi ya Serikali si mtu binafsi au raia.

Kambole alisema uhaini ni kosa kubwa akitoa tahadhari kwa Serikali kuwa kabla ya haijachukua hatua dhidi ya watu wengine, ihakikishe inatenda haki kwa wanaowashikilia, ikiwemo kuwapa huduma zinazostahili.

“Kosa la uhaini kwa namna linavyoonekana kwa sasa wanalipotosha au wanalifanya lionekane la kawaida. Kosa ambalo ni ‘serious’ (kubwa) wanalifanya lionekane la kawaida kwa sababu wameshalizoea kulisikia,” alisema.

Akijadili zaidi kosa hilo, Profesa wa sheria, Abdallah Safari alisema kwa mujibu wa Sheria ya Kanuni ya Adhabu kifungu cha (39), chenye vifungu vidogo kuanzia vya moja hadi nne, mtu yeyote raia wa Tanzania akiwa na nia ya kumuua au kumjeruhi Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania anatenda uhaini.

Alisema vifungu hivyo pia vinazungumzia mtu akitaka kuipindua Serikali au kuchochea mambo kama hayo yafanyike, vyote vinahusisha na masuala ya makosa ya uhaini.

“Kwa tafsiri ya sheria ya kanuni ya adhabu (yote hayo) ni uhaini na adhabu yake ni mbaya sana yaani kunyongwa. Hili ni shtaka la juu kabisa katika makosa ya jinai,” alisema Profesa Safari.

Tafsiri ya Profesa Safari inaungwa mkono na Wakili Edson Kilatu akisema uhaini ni kosa pekee ambalo linatajwa kwenye Katiba moja kwa moja kuwa ndiyo kosa kubwa kuliko mengine na adhabu yake ni kifo na kwa mujibu wa kifungu cha 148 (5) cha Sheria ya Mwenendo wa Jinai Sura ya 20 halina dhamana.

“Kwa mujibu wa kifungu cha 39 cha Kanuni ya Adhabu uhaini umeainisha vitu vingi kwanza njama yoyote ya kutaka kumuua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na pili njama yoyote yakutaka kupindua Serikali.

“Jambo lingine linaloweza kuwa uhaini ni kitendo cha kuzuia majeshi kufanya majukumu yake ya kuilinda mipaka ya nchi kwa kusudio la kutaka Serikali ianguke na kushindwa kufanya majukumu yake,” alisema.

Kesi nyinginezo

Endapo kesi hii itafunguliwa itakuwa kwenye orodha ya nyingine kadhaa zilizowahi kuendeshwa kwa nyakati tofauti nchini.

Kati ya mwaka 1989 hadi 1991, aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad (marehemu) aliwekwa kizuizini kwa kosa la uhaini, lakini baadaye aliachiwa.

Kesi nyingine ni ya Khamis Ali Machano na wengine 17, wafuasi wa CUF walioshtakiwa kwa tuhuma za kutaka kupindua Serikali ya Mapinduzi Zanzibar chini ya Rais Salmin Amour.

Tuhuma hizo zilisababisha kufunguliwa kesi ya uhaini na kukaa gerezani miaka miwili na nusu.

Hata hivyo, mwaka 2000 Mahakama ya Rufaa Tanzania ilitamka kupitia hukumu yake kuwa uhaini usingeweza kutendekea Zanzibar kwa kuwa si dola bali ipo chini ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Vilevile, mwaka 1985 Watanzania 19 wakiwamo wanajeshi 14 walifikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya kula njama za kumpindua Rais wa Kwanza wa Tanzania, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

Baadhi yao waliachiwa huru na wengine kuhukumiwa kifungo cha maisha. Hata hivyo, mwaka 1995 waliachiwa huru na Rais Ali Hassan Mwinyi.

MWANANCHI
Umemwacha Thomas Zangira = 197-- naye alifunguliwa kesi ya Uhaini
 
2025 imekuwa ngumu kiasi wahusika wanaanza kutumia virungu kuua nzi
 
Hapo hakuna kesi , Hiyo ni michezo michafu ya wanasiasa , wanakama wakubwa kiuongo uongo na kuwapa kesi mbaya zaidi ili wadogo( sisi wananchi) tuongope ukiangalia na hali zetu za kiuchumi upesi kesi ya uhaini si utaua familia kwa presha, hivo hiyo ni danganya toto tu kuzima suala la bandari , mbinu za kimedani hizo , IMEISHA HIYO.
 
Back
Top Bottom