Kuna neno linatumika vibaya na kwa dhamira isiyosahihi 'Failure'. Kwa def kutoka katika dictionary, failure; be unsuccessful, be or judged below standard in a test, dissappointing or to be useless (to someone), be unable to do something. Neno hilo linalisitizwa ili kufunika hata kile kizuri kilichofanyika, na hapa ndipo hoja ilipo, je mistakes zilizofanyika zinaondoa success zilizopatikana?
Nyerere alichukua nchi ikiwa na changamoto nyingi sana. Hakuwahi kuwa waziri au mkuu wa mkoa kama viongozi waliomfuata, lakini hii sio excuse!
Nchi ilikuwa haikuwa na wasomi, wananchi kuwa na matarajio makubwa na uchumi hafifu. Kazi haikuwa kujenga uchumi tu bali kuliunganisha taifa lielewe kujitawala maana yake ni nini. Vurugu (sio jaribio la mapinduzi) kambi ya Colito(Lugalo 1964) ni mfano mzuri wa matarajio ya wananchi baada ya uhuru.
Nchi ilipita katika wakati mgumu, 1974 njaa kali kutokana na ukame(sio ujamaa), 1977 kuvunjika kwa EA, 1978 vita ya Kagera, 1980 vita ya Iran na Iraq, 1980.. vita baridi. Kuvunjika kwa EA kuliifanya serikali ya Tz ibaki tupu. Nchi ikaanza upya kwa kila kitu, kila shirika na kila taasisi.
Licha ya changamoto hizo tulikuwa na maendeleo ya ujenzi wa vituo vya afya, elimu na vyuo vya kada ya kati kuliko wakati wowote ule.
Nyerere aliwekeza katika reli,usafiri majini,Anga na kujenga viwanda.
Infrastructures na Industries ndivyo vilitegemewa kulikuza taifa hili kiuchumi (foundation)
Akiondoka madarakani vitu vyote hivyo vilikuwa vinaonekana na vinafanya kazi.
Marekani inatumia infrastructure zilitojengwa wakati wa industrial revolution na great depression. Uingereza inatumia infrastructure kama reli na bandari hadi leo , vyote vikiwa mwendelezo wa misingi iliyojengwa na watangulizi.
Kama hatuwezi kuweka mabehewa au kuendesha ATC ni failure ya nani?
Tuna acha mahindi yaoze mbeya tumeshindwa kuendesha Tazara, ni failure ya nani?
tunageuza vyuo alivyojenga Nyerere ( mfano, IFM, Mzumbe kuwa vyuo vikuu) ,hatuwezi kujenga mabwawa ya umeme, tunaagiza jenereta hewa ni failure ya nani?
Hatuwekezi katika shule na vyuo tunawekeza katika VX na posho,tumeua kibo match tunaagiza kutoka pakistan ni failure ya nani?
Tumeua Moproco tunaagiza kutoka malaysia, tumeua magunia tunaagiza rambo india, tumeua general tyre tunaagiza mitumba ni failure ya nani?
Tumeua Tanganyika packers tunaagiza kutoka brazil,tumeua STAMICO mchanga unabebwa usiku, failure ya nani?
Tumeua mgololo tunauziana plot,tunaacha twiga wanabebwa usiku, tunasema mwl kafeli!!
Hospitali gani kiwango cha rufaa imejengwa baada ya mwalimu kuondoka!! nani ka fail hapo!
PM Churchil anaheshima sana uingereza, baada tu ya vita alivyoshinda aliondolewa madarakani, je Sir Churchil anapewa heshima ya failure au success? Hakuna kiongozi duniani aliyewahi kukamilisha ndoto zake 100%, je nao ni failure!!!
Ni ukweli kuwa failure inapimwa kwa viwango kama vile chuo au shule inapoweka pass mark, swali ni je Nyerere anapewa pass mark kiasi gani hadi tuseme 'failure'? kwa definition inaonekana anapewa 0 au 5%, fair enough! Ili tupate pass mark ya haki ya Nyerere basi uzuri na uovu viwekwe katika mizani, si kusema 'mbaya' au failure bali ielezwe ni kwa vipi kama ilivyo kwa wanaosema pass wakionyesha ABCD.
Swali litakuja 'investment katika intellectual' inapimwa vipi, maana viongozi wote wazuri na wabaya ni zao la mwalimu wakiwemo maprofesa, JK,BWM n.k. Kama E.Lowassa ni 'failure' ya Nyerere, Salim A Salim ni success ya mwl, tunapata wapi ushajaa wa ku generalize kila kitu cha Nyerere kama 'failure' endapo hatuangalii pande zote.