Did Nyerere admit he was a "failure"? Some say "Yes he did"...

Did Nyerere admit he was a "failure"? Some say "Yes he did"...

Yote. Wa Dar wakipelekwa gezaulole.
Napata kichefuchefu kila ninaposoma posts au threads za wewe Faiza (mbaguzi) hasa zinazomshambulia marehemu Baba wa Taifa. Hujaolewa wewe? Hebu nenda kapike huko tuondelee uchuro eboo!
 
Swali: Nani amjuaye Joan Wicken?
She was Mwalimu's mentor and wrote his speeches.Inasemekana she brainwashed Mwalimu into 'Ujamaa (socialism)' idealogy ambao ungekuwa tofauti kabisa na ukomunist wa China au USSR wakati ule.
 
Kumbe humu wengi ni watoto yaani Bi Joan Wicken hakuna amjuaye alikuwa na kazi gani hapa Tanzania? Muhulizeni Mwanakijiji si ndio mjanja wenu
 
Yote. Wa Dar wakipelekwa gezaulole.
Kumbe waTZ walikuwa mijini tu. Jaribu kukatiza Ngorongoro na Serengeti utaona watanzania wa ukweli tunaishi bila hofu ya hao simba mnaoimba kila siku! Au walikuwa 'simba' wa sumbawanga?!
 
Mara nyingi huwa najiuliza, hivi yale maamuzi mabovu yote yaliyopeleka kuwatesa raia wa Tanzania yalikuwa ya Nyerere kweli?

Kinachonifanya nijiulize, hivi ni kweli M'Tanzania unaweza kuona raia zako wanateseka na wewe bado umo tu, kuwaswaga maporini wakaanzishe vijiji vya ujamaa?

Hivi unaona watu wako wanadhoofika kwa kukosa milo ya kutosha (sufficient nutrients), halafu wewe M Tanzania mwenzao bado tu unag'ang'ania uzi uleule wa usosholisti?

Hivi unaiona nchi yako inateketea, mabarabara hayapitiki kwa mashimo, hospitali zinaanza kuwa ni mahali pa kupokea misiba na misongamano ya wagonjwa, lakini wewe kama M'Tanzania bado upo tu, unapeleka fedha zako kwengine? "natengeza kwa wenzangu na kwangu kwa poromoka"

Nani amjuaye Joan Wicken?

Angalia aheri waliokufa kwa Njaa kama walikuwapo sababu ardhi ipo; kuliko wale walionyang'anywa zana zote za kuishi NYUMBA, ARDHI na USALAMA

Nyerere succeeded in keeping us Free no bloodbaths like all of our neighbours... Au Ungependa kuishi na Idd Amin Dada huko Uganda?
 
Napata kichefuchefu kila ninaposoma posts au threads za wewe Faiza (mbaguzi) hasa zinazomshambulia marehemu Baba wa Taifa. Hujaolewa wewe? Hebu nenda kapike huko tuondelee uchuro eboo!

U Baba kwako, baba yangu ni mmoja tu aliyenizaa. Hata mungu wangu si baba.
 
Mwalimu alishawahi kutamka mwenyewe kwamba un mazuri mengi wamefanya na kuna mabaya wamefanya kwa ajiri ya kiazi hiki,,alitusii tufuate mazuri tu kama kutetea rasilimali za taifa kw amanufaa ya watanzania na kuwa filisi wote wahujumu uchumi,muulize maalimu amefanya yapi mema mpaka sasa???
 
Mmeona Forums za Wakenya? a So Called Capitalist Nation? Hawaongelei Ardhi anymore, Wanaongelea Mafanikio ya Nairobi sababu ya Wakikuyu, Wanaongelea Rais lazima awe Mkikuyu kuliko Mkamba, au Mjaluo hawajui Waislamu ila wanasema kiswahili chao kizuri huko Mombasa... yeah wataweke Mahakama ya Kadhi only in Mombasa.

Is that fair? kuna Usawa hapo? Sisi kila mtu ana haki sawa sababu ya nani? Tuache Chuki, Chuki zitatupeleka kwa Matatizo Majirani wetu wanayo
Please Please Chuki iishe...
 
Tazama vizuri hii picha halafu itolee maelezo:

joan2.jpg

Hata Kenyatta alikuta Kenya inatawalika. Tena katika harakati za uhuru makabila yote yalichangia wakiwemo Wajaluo, ambao walimwachia Kenyatta kiti cha urais wa chama na nchi, waluhya, Wakikuyu, Wakalenjin, etc.etc. Lakini baada ya uhuru Kenyatta alianzisha sera makusudi za kuwapendelea Wakikuyu. Walipewa mikopo ya biashara, walipewa ardhi ya kilimo na walipendelewa katika nafasi za kazi. Ikafikia hatua Kenyatta akaanza kuwatukana Wajaluo kuwa hawakutahiriwa. Tena kwenye mkutano wa hadhara. Nchini Kenya lugha iliyokuwa inatumika katika ofisi za serikali zilikuwa Kiingereza na Kikikuyu. Linganisha hayo na yale aliyoyafanya Nyerere Tanzania utaelewa anachosema Mwanakjj.
Ndio unataka kusemaje, angependelea Kizanaki!?
 
You have missed my point entirely. Soma tena nilichoandika.
Nimekusoma na kukuelewa, vile nilivyo elewa...! Kufananisha Kenya na Tanzania (Tanganyika) yenye makabila 123, unakosea kabisa. Kiufupi Nyerere aliendeleza kile alichowakuta nacho Watanzania.
 
Nimekusoma na kukuelewa, vile nilivyo elewa...! Kufananisha Kenya na Tanzania (Tanganyika) yenye makabila 123, unakosea kabisa. Kiufupi Nyerere aliendeleza kile alichowakuta nacho Watanzania.
Hujanielewa kaka.
Sisi tuna makabila 123. Kenya wana makabila mangapi? Nadhani ni zaidi ya 20 na kitu. Sasa ukinipa makabila 20 na wewe uwe na makabila 123 nani atakuwa na kazi ngumu ya kuyaunganisha makabila hayo? Ninachosema ni kwamba wakati Tanganyika inapata uhuru na Kenya inapata uhuru, kulikuwa na equal level field, kote Tz na Kenya, ya kuleta umoja wa kitaifa kwa sababu misingi ya KANU na TANU ilikuwa inafanana. Hata wimbo wa KANU waliiga kutoka TANU---Tanu yajenga nchi, Kanu yajenga nchi. Lakini tulianza kutofautiana pale Nyerere alipochukua msimamo wa kitaifa na Kenyatta akafuata msimamo wa kikabila baada ya nchi zetu kuwa huru. Sasa la kutoelewa hapo ni lipi? Na kusema kuwa Nyerere alitukuta Watanzania na umoja ama ni kupotosha au kutojua ukweli. Ngoja nikupe mfano wa kule kwetu. Tuna makabila 23. Ilikuwa vigumu kabla ya TANU kwa Mzanaki kuona Mjita au Mkurya kuoa Msukuma. Lakini kilichotuunganisha pamoja ni mwamko wa uzalendo, wakati huo tunaitana wananchi, ulioletwa na TANU. Nakumbuka mwalimu wangu wa primary alipata mchumba wa Kinyamwezi alipokuwa masomoni Tabora. Mama yake alikuja kulalamika kwa baba yangu ambaye alikuwa mzee wa kanisa, kuwa mwanae anamletea mkwe wa Kinyamwezi, wataelewanaje? Ilikuwa sokomoko kweli kweli. Ilibidi baba afanye kazi ya ziada kumshawishi yule mama kuwa sisi sote ni Watanganyika na huko ndiko tunakoelekea. Hatukuwa na umoja. Mwingereza alitumia mfumo wa divide and rule. Ni TANU na Nyerere ndio waliofanya kazi ya ziada kuleta umoja wetu na hilo huwezi kubisha.
 
Habari yako imeongeza chumvi, uko Musoma nina historia nako, babu yake na mama yangu mimi alikuwa cheaf na alikimbia baada ya nduguze kutaka kumuwa kwa sumu ya mamba, baada ya kusikia kuwa amesilimu na amebadilisha jina, alikimbia na baadhi ya wasaidizi wake wa karibu, akakimbilia Puma uko Singida na akajenga mji wake na akaoa Wake mmoja alikuwa ni mtoto wa Cheaf Mkwawa na mwingine Bibi yake na mama yangu ambaye ametokea Zaire (Wakiitwa Wamanyema). Na uko Singida alipokelewa vema tu na wenyeji wa uko. Bibi yangu mzaa mama aliolewa na babu yangu ambaye baba yake ni kutoka Malawi. Huo ni upande wa Mama yangu, na hata upande wa baba yangu walichanganyika na kuoana Tangia enzi na enzi na kulikuwa hakuna hayo unayoyasema...!

Kulikuwa na baadhi ya watu kweli walikuwa na ukabila, lakini si kwa kiwango cha kukataa umoja, na ndio maana Mtemi Mtyela Kasanda wa Tabora aliyejulikana kwa jina la Kifo au maiti (Mtemi Mirambo), aliweza kukusanya jeshi lenye askari wa kutoka makabila tofauti tofauti na kulipa jina la Warugaruga. Bila kusahau vita vya Majimaji ambavyo navyo vilikusanya watu wa makabila ya kusini mwa Tanganyika.

Nyerere alipokuja Dar es Salaam, alikuta TAA ina watu walikwisha changanyika tayari, na yeye alikaribishwa vema tu na wenyeji na wala hawakumbagua.

Alichofanya Nyerere ni kuweka Askari jeshi na polisi wengi kutoka Mkoa wa Mara, kiasi cha wenyeji wa mkoa huo kuhisi kila kazi ni Jeshi tu.

Wakati mwingine tulikuwa tukiwatania kwa kuwaiga "... Chacha amepata rikazi ra jeshi la Posta au Nyasanje amepata ri kazi la jeshi la sekretari au ra supamaketi" n.k.

Kwa ufupi ni kuwa nchi yenye makabila machache ni rahisi sana kuwa na ukabila, ukilinganisha na nchi kama Tanganyika yenye makabila 123, kwa hakuna kabila kubwa kiasi ya kuweza kupata kura za kuwawezesha kutawala nchi, tofauti na nchi kama Kenya, Uganda, Rwanda au Burundi.
 
Nimekusoma na kukuelewa, vile nilivyo elewa...! Kufananisha Kenya na Tanzania (Tanganyika) yenye makabila 123, unakosea kabisa. Kiufupi Nyerere aliendeleza kile alichowakuta nacho Watanzania.
Mkuu wangu labda mimi nikueleze kinagaubaga upate kuelewa matatizo ya kuchukua nchi iliyokuwa imetawaliwa kwa mabavu ama Ukoloni.

Pengine hufahamu kwamba Kabla ya Uhuru kulikuwepo na makundi ya kikabila na baina yetu hatukukubaliana kiutawala zaidi ya kuwa chini ya mkoloni. Waasisi wa chama chetu TANU iwe toka AbdulWakil au Nyerere swala kubwa lililowatatizo zaidi iulikuwa kuunganisha nguvu ya kupata kudai uhuru wetu ambao ulikuwa na masharti na moja kubwa lilikuwa kupata kura toka majimbo yote na kazi hii ilianza baada ya Nyerere kuwa mwenyekiti wa chama.

XPASTER, kabla ya Uhuru sisi tulozaliwa bara hatukuzungumza kiswahili kama lugha ya kwanza na wala haikuwa lugha ya biashara..Na nakumbuka vizuri sana ingawa nilizaliwa na wazazi wanazungumza kiswahili ilikuwa taabu sana ku communicate na wengine hadi nilipokuwa fluent kwa Kijita na Kikerewe.

Sisi tulokuwa tukizungumza kiswahili tuliitwa waswahili na Waislaam na hakika ni Waislaam na waswahili ndio walizungumza kiswahili hata kiwe cha kuokoteza, tena basi huwezi kuamini Biblia ya kwanza niliyoiona mimi ilikuwa kwa Kikererewe na hata nyimbo za kanisani zilikuwa za kikerewe.

Labda kwa kifupi nikwambie kwamba sisi tumepitia muda wa mabadiliko na tunayozungumza sii historia iliyoandikwa mahala popote isipokuwa watu wengi wanafikiria maisha ya Dar ama Pwani yalikuwa vile vile huko bara.. hapana mkuu wangu.

Na kumbuka tu kitu cha kwanza ktk kujenga utamaduni wa watu ni lugha, siku Nyerere alipotangaza kiswahili kuwa lugha ya taifa kulipita malalamishi mengi tena huwezi kuamini. Na ilichukua kazi kubwa sana Nyerere kubadiulisha masopmo yote kuwa kwa kiswahili jambo ambalo hadi leo wasomi na wataalam wanamlalamikia kwa sababu Kiswahili kiliharibu upana wa elimu lakini wakati huo huo ukijenga Umoja wa Utaifa letu.

Nakuhakikishia kama Kiswahili kisingekuwa lugha ya Taifa na tukaendelea na lugha za makabila huku Kiingereza kikitumika kama lugha ya kufundishia ingekuwa kazi kubwa sana hata kuelemisha wananchi kwa mwalimu kutoka Lindi aje fundisha Ukerewe, lakini maadam ku learn lugha haichukui muda kama elimu watu wengi walishindwa kuelewa kwa nini kiswahili kiwe lugha ya kufundishia ikiwa wananchi wengi (asilimia kubwa) hawazungumzi kiswahili, lakini leo hii wanakubali kiingereza kiwe lugha ya kufundishia hata kama ni asilimia ndogo sana wanazungumza lugha hiyo, tena basi pasipo kujali kama lengo ni kukifanya kiswahili kiwe lugha ya mawasiliano isipokuwa lugha ya kibiashara...

Hivyo ukitazama malengo ya lugha ya biashara kinachotakiwa ni wananchi kufundishwa lugha kuizungumza basi, lakini unapoifanya lugha kuwa ya kufundishia siku zote unaua lugha zingine ktk mawasiliano kwa sababu huyo msomi hataweza kujieleza ktk lugha yeyote isipokuwa ile aofundishiwa hhivyo kuzoea kutumia lugha hiyo ktk mawasiliano yake..

Na ukitazama sasa hivi TZ kiswahili kinapotea taratibu, vijana wengi wanashindwa kunyoosha kiswahili pasipo kuweka maneno ya kiingereza na sii kwamba wanadengua laa hasha! hawajui maana ya maneno hayo kwa kiswahili ingawaje yapo.. Hii ni mpoja ya mwanzo wa kututenganisha.. Lugha ni kiungo na lugha inaweza kuwasambaratisha ndio maana unaona nchi zote za magharibi wanaprotect lugha zao na mara zote hujifunza lugha ya kigeni kama lugha ya kibiashara (somo) na sii ya kufundishia..

Na kwa bahati leo hii mimi na wewe na wengine wote hapa JF tunajumuika ktk mijadala mbalimbali kutokana na maamuzi ya utawala wa JKN laa sivyo tungekuwa kama Mataifa mengine yaliyoshindwa kutumia lugha moja kuwa ya mawasiliano na hakika lugha ina picha pana sana ktk Ubaguzi wa makabila kama tunavyozungumzia Udini kutokana na majina ya watu na ubaguzi mwingineo..
 
Habari yako imeongeza chumvi, uko Musoma nina historia nako, babu yake na mama yangu mimi alikuwa cheaf na alikimbia baada ya nduguze kutaka kumuwa kwa sumu ya mamba, baada ya kusikia kuwa amesilimu na amebadilisha jina, alikimbia na baadhi ya wasaidizi wake wa karibu, akakimbilia Puma uko Singida na akajenga mji wake na akaoa Wake mmoja alikuwa ni mtoto wa Cheaf Mkwawa na mwingine Bibi yake na mama yangu ambaye ametokea Zaire (Wakiitwa Wamanyema). Na uko Singida alipokelewa vema tu na wenyeji wa uko. Bibi yangu mzaa mama aliolewa na babu yangu ambaye baba yake ni kutoka Malawi. Huo ni upande wa Mama yangu, na hata upande wa baba yangu walichanganyika na kuoana Tangia enzi na enzi na kulikuwa hakuna hayo unayoyasema...!

Kulikuwa na baadhi ya watu kweli walikuwa na ukabila, lakini si kwa kiwango cha kukataa umoja, na ndio maana Mtemi Mtyela Kasanda wa Tabora aliyejulikana kwa jina la Kifo au maiti (Mtemi Mirambo), aliweza kukusanya jeshi lenye askari wa kutoka makabila tofauti tofauti na kulipa jina la Warugaruga. Bila kusahau vita vya Majimaji ambavyo navyo vilikusanya watu wa makabila ya kusini mwa Tanganyika.

Nyerere alipokuja Dar es Salaam, alikuta TAA ina watu walikwisha changanyika tayari, na yeye alikaribishwa vema tu na wenyeji na wala hawakumbagua.

Alichofanya Nyerere ni kuweka Askari jeshi na polisi wengi kutoka Mkoa wa Mara, kiasi cha wenyeji wa mkoa huo kuhisi kila kazi ni Jeshi tu.

Wakati mwingine tulikuwa tukiwatania kwa kuwaiga "... Chacha amepata rikazi ra jeshi la Posta au Nyasanje amepata ri kazi la jeshi la sekretari au ra supamaketi" n.k.

Kwa ufupi ni kuwa nchi yenye makabila machache ni rahisi sana kuwa na ukabila, ukilinganisha na nchi kama Tanganyika yenye makabila 123, kwa hakuna kabila kubwa kiasi ya kuweza kupata kura za kuwawezesha kutawala nchi, tofauti na nchi kama Kenya, Uganda, Rwanda au Burundi.
X-Paster,
Kwa information yako mimi ni mzaliwa wa Musoma. Nimekulia pale mpaka nilipoingia sekondari. Kwa hiyo uzoefu wangu, kutofatiana na wako, si wa kusimuliwa. Nimesoma na Wakiroba, Waisenye, Wangoreme, Wakurya, Wasimbiti, Wakwaya, Waruri, bila kutaja makabila makubwa kama Wakerewe, Wasukuma na Wajita. I speak from experience. Na kumalizia tu, si Nyerere aliyeandikisha Wakurya jeshini, naona hiyo dhana potofu inaenezwa na wale wanaotaka kumwonyesha Nyerere kuwa mkabila. It was the damn British colonialists. Growing up nilikuta kazi nyingi za ulinzi, polisi zikifanywa na Wakurya, si Musoma tu bali hata Mwanza. Na melini wapishi na walinzi walikuwa Wajaluo. Nyerere alirithi jeshi la kikoloni na alijitahidi kuajiri makabila mengine kama vile Wachaga, etc.
 
Huyu jamaa kila time hoja zake ni Nyerere tosha basi mwache arest in peace tu hoja zimemuishia za kuchangia maendeleo kutwa Dikteta blah blah
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom