Did Nyerere admit he was a "failure"? Some say "Yes he did"...

Did Nyerere admit he was a "failure"? Some say "Yes he did"...

Umeshushuka shuu! Siku zingine msijidai ku "challenge" just kwa ubishi tu. Unanini babuwee? Unachekeshaa.
Uraisi ni taasisi sio mali ya mtu wala kikundi fulani....baada ya miaka kumi kumi tutapata muda wa kufanya assessment ya kila mtu amefanya nini. Kiukweli, penye ukweli uongo hujitenga....kwangu mimi, Nyerere was the best.....na tuliyenaye is the worse though ana muda pia wa kubadilisha mambo....sio ushabiki wala nini, nchi sasa uswahili umezidi...wizi wa mali ya umma umezidi na hakuna hatua yoyote inayochukuliwa...ufisadi nao ndio kitoweo cha watu wanaoneemeka na utaratibu huu.
 
Mkuu wangu katika swala la kuanguka kiuchumi nadhani hatuna sababu ya kulinganisha na nchi nyinginezo kwa sababu itakuwa utnaukimbia ukweli. Sisi tuli fail, so are many nations kama vile leo Greece wanavyolia haina maana Ureno na nchi nyingine za Ulaya ziko salama. Kifupi leo hii uchumi umeshuka kila mahala lakini, picha kubwa ipo Ugiriki na inabidi tuseme rais wao au wagiriki wame fail, ingawaje Taifa halitakufa kesho .

Na labda niseme Nyerere failed sio kwa sababu ya Ujamaa bali ni sawa na nyumba ziliyojengwa kwa drywall na mbao zikapigwa na dhoruba ya kimbunga (Tornado), sasa ziole zilizokuwepo katikati ya dhoruba zitaathirika zaidi ya zile za pembeni na pia hatuwezi kusema zile zilizoweza kupona zimejengwa imara zaidi ya zile zilizoharibiwa. Factors za ku detarmine uimara wa nyumba haupimwi baada ya madhara bali wakati wa ujenzi...

Na ndipo napomsifu Nyerere kwamba yeye aliwekeza sana ktk miundombinu na viwanda ambayo ilimchukua zaidi ya miaka 15 ya utawala wake kuijenga (toka 1967 to 1982) lakini wazalendo hawakuweza kuona faida yake kwa sababu ujenzi wa miundombinu na viwanda hivyo ulitufiksha kula Bulga na maziwa ya msaada kwani walichotegemea ni ujenzi wenye kuzaa kama dhahabu. Wanahesabu madeni ya kujenga miundombinu hiyo kama hasara wakati ni miundombinu hiyo na viwanda ambavyo leo vinatumika kuendesha uchumi wa serikali hizi toka Mwinyi hadi Mkapa.

Yote haya yamesaulika na kuitwa FAILURE simply because kimbunga cha 1982 na leo tumesahahu kwamba ni wakati nchi kubwa zinazotoa mafuta duniani zilikuwa ktk hekaheka ya vita (Iran vs Iraq) dunia nzima iliyumba kiuchumi leo Taifa ambalo fedha yake yote limewekeza ktk miundombinu na viwanda lingeweza vipi kuhimili vishindo tena baada ya vita ya Uganda.

Pamoja na yote yale na sababu zote zilizokuwepo lakini bado tukubali kwamba tulishindwa! we failed kama mzee wa Kariakoo aliyejenga nyumba ya vyumba sita ataonekana hakuwa na akili kuliko huyu mtoto wake aliyewtumia nyumba ile ile kuipangisha au kuivunja na kujenga ghorofa ambalo limewapa watoto hawa maisha bora zaidi ya yale waliyokulia chini ya himaya ya mzee baba yao.

Na hakika hawatakumbuka nguvu ya mzee kuijenga nyumba ile ambayo pengine ili cost only Tsh 5,000 lakini kwa mshahara wa Tsh 50 kwa mwezi (a thousand times) lakini sisi wenyewe kizazi kipya na mshahara wa Tsh 500,000 tunashindwa hata kununua kiwanja.
Imagine our elderly sacrifice, lakini waulize hao MasharoUharo wa Kariakoo utasikia makosa yote ya dingi, he failed us! angenizaa mimi ktk tajiri - NINGEKUWA bl;aa! blaa! blaaa!

Kwa hiyo mawazo mengi against Nyerere ni ya hawa Masharouharo ambao walitaka watengewe kila kitu mezani wao waje kujichana kama vile hakuna najsi!..Miafrika ndivyo Tulivyo!

Nyumba za kariakoo za hao wazee hazikujengwa wakati wa nyerere, thubutu wakati wa nyerere ujenge, si unaenda kujieleza pesa umetowa wapi.
 
Kwa sababu 1. Hiyo interview ya CNN niliiona. na 2. Kama Ukristo ulishindwa mbona bado twaenda makanisani? That is the point he was trying to impress upon the interviewer, kufananisha kushindwa kwa ujamaa na kushindwa kwa Ukristo.
Hayo maswali wenzako walimuuliza, ila sina uhakika kama aliyajibu.
 
Yaani siamini kwamba pamoja na shida zote alizoacha nyerere
kuna watu hawataki kusikia kabisa kuwa nyerere kuna mengi yalimshinda

its funny,
sisi tunaosema nyerere alishindwa,
hatupingi mengine kuwa alikuwa na ushawaishi afrika,au kuwa alikuwa labda na nia njema

but the bottom line
alishindwa..
 
Kataa tukuletee mabandiko mengine, wacha kutetea kisicho teteeka. He was a failure all the way.
huwaga siamini kama akili yako haikuwahi athirika utotoni. Either ulitolewa kwa vacum au ulivuta..... Na hata ulikulia katika mazingira tofauti. Kumuandama huyu mzee ni utovu wa nidhamu. Kama unamuogopa hata kidogo Allah wallah usingefanya hayo. Na hata hivyo mtafail na hiyo mipango yenu isiyo na kichwa wala miguu.
 
Hivi wewe hujawahi kukaa foleni ya sukari wakati wa nyerere? au ulikuwa haupo?

Masuala haya inabidi kuyaangalia kulingana na nyakati, tusiwe tunahamisha mambo ya wakati fulani na kuyapachika ktk wakati mwingine. Yawezekana kweli kupanga mstari kwa ajili ya sukari nk, kulikuwa na tija na manufaa ktk jamii. Lakini ukiyatazama mambo ya zamani(analog era) kwa darubini ya leo (digital era) lazima yatakuwa incompatible na lazima utayaona ni illogical.

Angalia leo watu wanaona wanafunzi kuvaa uniform za shule ni logical lakini itafika siku ambapo watu wa wakati huo watashangaa, ala sasa hawa wajima walikuwa wanavaa uniform za nini.

Kule kijijini pamoja na umri wangu kiduchu, lakini leo hua nashangaa kama kile nilichokuwa nakishudia wakati huo si ndoto, lakini wakati huo ilikuwa sawa sawa kwangu. Yani ni hawa sungusungu ama walugaluga kwa jina la isike na mirambo.
 
Hivi nyerere angekuwa haja "fail" tungekuwa tunapewa sukari kwa foleni wiki kilo moja kwa kaya moja? Hivi nyerere agekuwa haja "fail" si ageachia ngazi na huku nchi kidogo iko kwenye ahueni? kaiacha hata benki kuu kaichoa moto. Loooh, corruption mtindo mmoja, sisi tuliobahatika kuikimbia nchi wakati wake, tukija kutembea hapa, Wallahi zawadi kubwa ni dawa za meno (colgate) na sabuni za kuogea.

Nakumbuka airport maaskari walivyokuwa wajinga walikuwa wanashangalia saa ya "digital", Kama wameona kitu cha ajaaabu. He was simply a total failure.

wemesahau aliwanyima watanganyika hata television ya taifa... leo hii wanataka kumfanya mtakatifi ... kuna vijitu vinajifanya vina elimu hapa , elimu ya mlimani, videgree mbuzi... bado wanakumbatia u-DIKTETA... NO WONDER THIS COUNTRY WILL ALWAYS BE POOR...
 
Bora umekuwa Muungwana umesema gazeti hujalipata na siku ukilipata tuwekee hapa na sisi tuone, au; kwa sababu umesema wenyewe walinukuu mazungumzo ya kwenye CNN ambayo nadhani itakuwa ni television kwa nini usitafute hiyo video utuletee.

Mimi niliiyona hiyo program ...alihojiwa na Riz Khan wakati bado alikua anatangazia kupitia CNN... sasa unaweza kutafuta au kuwaandikia CNN kama kweli unahitaji kujua...Mimi sikuweka kumbukumbu sikujua kama kuna watu watakua wanamuabudu yule mzee.
 
Wanaekataa nyerere hakukubali kushindwa watuambie ni nini maana ya kung'atuka, wazanaki waseme!
 
Hivi wewe hujawahi kukaa foleni ya sukari wakati wa nyerere? au ulikuwa haupo?

Mbona hata miezi michache iliyopita sukari ilikuwa adimu? au hilo nalo lilisababishwa na Mwalimu?
 
Mwanakijiji, unapodai kuwa Nyerere alileta umoja, hivi alikuta hii nchi haitawaliki, watu hawasikilizani, kulikuwa na mapigano ya kikabila akayakomesha, alikuta Watanganyika wametawanyika akawaweka pamoja au...!?

Fafanua tafadhali, ina maana hata kwenye kupiga kampeni zake alikwenda na wakalimani au alitumia Kishwahili bila ya wakalimani?
Hata Kenyatta alikuta Kenya inatawalika. Tena katika harakati za uhuru makabila yote yalichangia wakiwemo Wajaluo, ambao walimwachia Kenyatta kiti cha urais wa chama na nchi, waluhya, Wakikuyu, Wakalenjin, etc.etc. Lakini baada ya uhuru Kenyatta alianzisha sera makusudi za kuwapendelea Wakikuyu. Walipewa mikopo ya biashara, walipewa ardhi ya kilimo na walipendelewa katika nafasi za kazi. Ikafikia hatua Kenyatta akaanza kuwatukana Wajaluo kuwa hawakutahiriwa. Tena kwenye mkutano wa hadhara. Nchini Kenya lugha iliyokuwa inatumika katika ofisi za serikali zilikuwa Kiingereza na Kikikuyu. Linganisha hayo na yale aliyoyafanya Nyerere Tanzania utaelewa anachosema Mwanakjj.
 
Mara nyingi huwa najiuliza, hivi yale maamuzi mabovu yote yaliyopeleka kuwatesa raia wa Tanzania yalikuwa ya Nyerere kweli?

Kinachonifanya nijiulize, hivi ni kweli M'Tanzania unaweza kuona raia zako wanateseka na wewe bado umo tu, kuwaswaga maporini wakaanzishe vijiji vya ujamaa?

Hivi unaona watu wako wanadhoofika kwa kukosa milo ya kutosha (sufficient nutrients), halafu wewe M Tanzania mwenzao bado tu unag'ang'ania uzi uleule wa usosholisti?

Hivi unaiona nchi yako inateketea, mabarabara hayapitiki kwa mashimo, hospitali zinaanza kuwa ni mahali pa kupokea misiba na misongamano ya wagonjwa, lakini wewe kama M'Tanzania bado upo tu, unapeleka fedha zako kwengine? "natengeza kwa wenzangu na kwangu kwa poromoka"

Nani amjuaye Joan Wicken?
 
haya mambo ya kufikiriaka sana,. lakini hii ya rais muislamu kuuwa raia wa nchi yake ili wazungu na waarabu wakombe madini yetu na wanyama wetu kwenye hifadhi zetu ni hatari sana huyu mkoloni mweusi.
 
mwache baba wa Taifa apumzike kwa amani.

RIP MWALIMU NYERERE!
 
haya mambo ya kufikiriaka sana,. lakini hii ya rais muislamu kuuwa raia wa nchi yake ili wazungu na waarabu wakombe madini yetu na wanyama wetu kwenye hifadhi zetu ni hatari sana huyu mkoloni mweusi.

Wakishikwa pazuri wanaanza, utawajuwa tu.
 
Joan Wicken ndiyo nani tena?

Nashangaa unamjuwa Nyerere lakini Joan Wicken humjui! ama kweli dunia hadaa na ulimwengu shujaa. Ngoja tuone wanaomjuwa ni nani wajibu hoja yangu. Au hawatoipenda hii na wataanza kama juu hao walioanza kuififirisha!
 
Mara nyingi huwa najiuliza, hivi yale maamuzi mabovu yote yaliyopeleka kuwatesa raia wa Tanzania yalikuwa ya Nyerere kweli?

Kinachonifanya nijiulize, hivi ni kweli M'Tanzania unaweza kuona raia zako wanateseka na wewe bado umo tu, kuwaswaga maporini wakaanzishe vijiji vya ujamaa?

Hivi unaona watu wako wanadhoofika kwa kukosa milo ya kutosha (sufficient nutrients), halafu wewe M Tanzania mwenzao bado tu unag'ang'ania uzi uleule wa usosholisti?

Hivi unaiona nchi yako inateketea, mabarabara hayapitiki kwa mashimo, hospitali zinaanza kuwa ni mahali pa kupokea misiba na misongamano ya wagonjwa, lakini wewe kama M'Tanzania bado upo tu, unapeleka fedha zako kwengine? "natengeza kwa wenzangu na kwangu kwa poromoka"

Nani amjuaye Joan Wicken?

I wish ungezaliwa Uganda na ungejua Idd Amin ni nani, na ungepata akili ya kujua kwa nini Waganda wanamuona Nyerere ni Mtakatifu..

Msikilize hapa:

Last edited by a moderator:
Mara nyingi huwa najiuliza, hivi yale maamuzi mabovu yote yaliyopeleka kuwatesa raia wa Tanzania yalikuwa ya Nyerere kweli?

Kinachonifanya nijiulize, hivi ni kweli M'Tanzania unaweza kuona raia zako wanateseka na wewe bado umo tu, kuwaswaga maporini wakaanzishe vijiji vya ujamaa?

Hivi unaona watu wako wanadhoofika kwa kukosa milo ya kutosha (sufficient nutrients), halafu wewe M Tanzania mwenzao bado tu unag'ang'ania uzi uleule wa usosholisti?

Hivi unaiona nchi yako inateketea, mabarabara hayapitiki kwa mashimo, hospitali zinaanza kuwa ni mahali pa kupokea misiba na misongamano ya wagonjwa, lakini wewe kama M'Tanzania bado upo tu, unapeleka fedha zako kwengine? "natengeza kwa wenzangu na kwangu kwa poromoka"

Nani amjuaye Joan Wicken?

Nani amjuaye Joan Wicken? Ans FaizaFoxy

Mwl Pumzika ndugu yetu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom