Kwa hiyo, hiyo ni conclusion ya moja ya muandishi aliyemnukuu nyerere kusema failure? Kama ndio hivyo kuna tatizo lipi hapo?
He simply failed. No one with his right mind can argue with this. Muwandanganye wale ambao hawakuwepo wakayi wake.
Nyerere kaiacha nchi njaa, kiza, hakuna hata mafuta ya taa, foleni ma petrol station, foleni hata sukari, ashaakum si matusi hata pamba zetu za kujistiri tulikuwa hatupati mpaka tuzinunue za magendo, sijui kama wanaume wanalijuwa hilo? ukipita njiani umebeba hata kikapu, kinapekuliwa na mgambo. Vizuizi vimewekwa Tanzania nzima eti vya kuzuia kipindupindu! jamani? mlikuwepo au mnabisha tuu?
Hivi mkiambiwa ukweli wa nyerere kwanini hamuupendi? nyerere alikuwa "orater" mzuri sana. Lakini mama yangu, ikifika kwenye maamuzi ya utendaji, yote bogus, hakuna kilicho fanikiwa.Viwanda vya umma, viko wapi? majumba aliyotaifisha, yako wapi? mabenki aliyotaifisha. yako wapi, shule alizotaifisha, ziko wapi? mashamba aliyotaifisha, yako wapi? vijiji vya ujamaa alivyolazimisha watu wahamie, viko wapi? mashirika umma aliyoanzisha, yako wapi? Hivyo vyote vimeanza kufa kabla yeye haja ng'atuka. Kaondoka benki kuu haina senti tano ya kigeni na ikachowa moto kuficha madudu yake, wizara ya mambo ya ndani ikachomwa moto kuficha madudu yake. Na ndio maana tukasikia mpaka kaburi lake liliwaka moto kwa dhulma alizofanya, siku aliyozikwa mpaka ardhi ikatetemeka kwa dhambi alizonazo.
Hao wanaojidai, oooh kaondoa udini. Ni waongo, kabla ya nyerere kulikuwa hakuna tatizo la udini Tanzania. Kungekuwa kuna tatizo la udini hata yeye asingepokelewa na kufadhiliwa na waIslaam wa Kariakoo. Oooh eti ukabila, ni nani aliyenyanyaswa kwa kabila yake Tanzania kabla ya nyerere? baada ya kuja nyerere ndio tukaona udini unaanza kwa kuwafunga mashekhe wote wwakubwa Tanzania, kuwahamisha makazi yao, kuwakejeli. Ukabila ukaanza alipoanzisha mashirika ya umma.
He was simply a failed dictator.