Ninashangaa kuna mtu anasema kama yapo mazuri mbona hayaonekani? ah! sasa kama ameacha viwanda 400 mkauza mtaviona wapi,
Nguruvi!!
Swali lako ni jepesi, rahisi, na lisilo na maneno mengi lakini limebeba ukubwa mkubwa sana na kina.
Tulikuwa na viwanda vya nguo - Mwatex, Mutex, Urafiki n.k - wameviua kwa kuleta mitumba leo wanaenda kuchapsha kanga za kampeni China! - wataona wapi mazuri ya Nyerere?
Tulikuwa na viwanda vya zana za kilimo (I hope bado ila Plau iko juu pale) -
Tulikuwa na kiwanda cha baskeli za Swala (kwa wasiojua ilikwua na alama ya mnyama swala, zilitengenezwa Bongo - nakumbuka tulikuwa tunazikodi pale Tanga enzi hizoooo!)
Tulikuwa na viwanda vya viatu tunaita Bora - tulivivaa wengine kwa fahari
Tulikuwa na kampuni ya Maziwa - na maziwa yake kwenye makatoni yale ya kijani na nyeupe..!!
Tulikuwa na Kiwanda cha Chai!
Tulikuwa na kampuni ya Radio (siyo kuuza, kutengeneza) iliitwa National pamoja na ya betri ya National! ya kijani na nyeupe!
Tulikuwa na kampuni ya ndege iliyokuwa inaruka hadi Uingereza huko kwa fahari (unaangalia ubavuni kama unapanda "Serengeti" chini ya kina Marehemu Kapt. Mazula!)
Tulikuwa na treni ya kisasa na huduma nzuri ya Tazara (ukikaa first class kwenye ile express hadi unajisahau!) hata reli ya kati yakaingizwa mabehewa mapya!
Dar-es-Salaam kulikuwepo na kampuni ya mass transportaion yanaitwa UDA (maikarusi na haya yale mafupi);
Meli ya Mv. Bukoba, MV. Victoria zote zilikuja wakati wa Nyerere kurahisisha usafiri, bandari ya Dar, Mtwara na Tanga zikapanuliwa,
Wakoloni walituachia madaktari 2 na wahandishi 12 tu wazalendo, Nyerere akaweka sera ya elimu ya bure kusomesha mamia ya vijana ndani ya miaka michache tu tukaanza kupata wasomi wa kada mbalimbali, vyuo vya ualimu vikajengwa, mahospitali yakajengwa (Mbeya, Sekou Toure Mwanza) n.k Sijazungumzia Vyuo vya Ufundi (Tanga Tech, Arusha Tech, Mbeya Tech) kuchukua vijana ambao wangeweza kuwa katika kada ya ufundi (watoto wa kike na wa kiume wakachukuliwa)
Ukimaliza sekondari kidato cha nne unajaza uchaguzi wa wapi unataka kwenda kutegemeana na academic perfomance yako - tena kwa vipaumbele, walioenda ualimu walienda, walioenda A level walienda n.k hakukuwa na mashaka kama ukifaulu kitafanyika nini? Hadi jeshi na polisi iliwezekana kuapply moja kwa moja toka shuleni.
Naweza kuendelea kuhusu huyu dikteta Nyerere alivyoiacha nchi yake tupu!
Hakuwahi kuonesha ubaguzi wowote wa rangi au wa dini - kiongozi pekee ambaye toka mwanzo hakuwa na tatizo na kuwa na multi -race government. Jaji Georges, Gen. Walden, Afande Singh, Al Noor Kassum na wengine waliweza kuitumikia nchi yao pasipo tatizo lolote. Leo hii nafasi zote kubwa zimeshikiliwa na watu weusi kana kwamba ni wao pekee wana urithi wa Tanzania. Hata Unaibu Katibu hakuna minority represented lakini hawa hawa wakaona fahari kweli kwa Obama kushinda Urais au Powell alipokuwa mkuu wa Majeshi kule USA! Utaona hata upinzani wa leo haurecruit from the minority groups ya Tanzania! Serikali ndio kabisa... !
Sijazungumzia mbuga na maliasili zetu jinsi ambavyo zililindwa wakati wa Nyerere na sijagusia madini n.k
Wanasema Nyerere aliacha nchi ina shambles.. vyote hivyo hapo juu vimetoweka au vinakaribia kutoweka! urithi wetu unaporwa na historia yetu inafutwa halafu wanadiriki kusimama kutuuliza "alivyoviacha viko wapi"?
Well.. wanataka kuivunja hadi Tanzania ili waweze kusema "Tanzania ipi?"!