Ukija uwanja wa Taifa ukiwa umevaa jezi ya Mamelodi Sundowns lazima utuoneshe passport ya Afrika Kusini na ukiwa na jezi ya Al Ahly utuoneshe passport ya Misri, nje na hapo Polisi watakuchukua ukapumzike” Damas Ndumbaro, Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo.

Yapi maoni yako?
Timu zinataka mapato Waziri aache mambo ya ajabu. Kwani makundi mbona zilipita? Hao waliokuwa wanavaa jezi za timu pinzani hawakuwepo? Uzalendo haujengwi Kwa nguvu, wao tu umewashinda.
 
Sasa kama mimi ni raia wa Tanzania lakini makazi yangu kwa muda mrefu yamekuwa huko Misri mtanikataza kushangilia timu nayoikubali?
Hakuan sheria inayosema ukiwa mtanzania basi ni lazima u-support Yanga au Simba. Huyo aliyesema hilo ni mpumbavu wa mwisho. Hivyo ni vilabu vya mpira na vina wachezaji kutoka nchi mbalimbali. Wamefikia kwenye udiktekta mpaka wanaamuru watu washangile timu ipi? Watanzania tungukuwa watu tunaojitambua, tungesusia kabisa kwenda mpirani siku hiyo ili liwe somo.
 
Ukija uwanja wa Taifa ukiwa umevaa jezi ya Mamelodi Sundowns lazima utuoneshe passport ya Afrika Kusini na ukiwa na jezi ya Al Ahly utuoneshe passport ya Misri, nje na hapo Polisi watakuchukua ukapumzike” Damas Ndumbaro, Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo.

Yapi maoni yako?
HII NI KAULI YA DICTATORSHIP NA UJUHA USIO NA AKILI TENA PREMATURE KABISA HII NI DALILI YA FAILURE NDUGU YANGU KUMCHUKIA ADUI HAIONDOI UHALISIA WA UBORA WA WENZETU MM NAONA TUNGEWEKEZA KWENYE KUASIDIA MAENDELEO YA SOKA LETU KWANZA UPUUZI KAMA HUU LEO HII USINGETOKEA HAO HAO WAGENI MNAOWAKATAANDIO MNAWAKUMBATIA KWENYE LIGI YENU NA NDIO WAMEPANDISHA LIGI YENU HALAFU LEO HII MNAKUJA KUPENGA NY***K****NY******NY***KOH AISEE NCHI HII INAENDESHWA NA AKILI KISODA MNO
 
Kila nchi ina utaratibu wake. Na utaratibu wa Tanzania ndiyo huo, so ni lazima kuufuata.

Ova
B... Mi hili suala naunga mkono 100% tena tumechelewa sana. Tumekuwa kama wendawazimu kushangilia wageni.
Sawa, utani upo tutaniane (kama mimi ile siku ya Wydad japo najutaga sana) ila sio katika kiwango tulichofikia cha kuujaza uwanja kushangilia wageni.

Watakaokiuka wageuzwe mfano, na iwe serious maana nchi yetu hii utekelezaji sifuri.
 
Hakuan sheria inayosema ukiwa mtanzania basi ni lazima u-support Yanga au Simba. Huyo aliyesema hilo ni mpumbavu wa mwisho. Hivyo ni vilabu vya mpira na vina wachezaji kutoka nchi mbalimbali. Wamefikia kwenye udiktekta mpaka wanaamuru watu washangile timu ipi? Watanzania tungukuwa watu tunaojitambua, tungesusia kabisa kwenda mpirani siku hiyo ili liwe somo.
Tungekuwa tunajitambua baada ya kauli hii, kesho tu angeshinikizwa ajiuzulu.

Ila mimi naona hii ni fursa. Fikiria una ushahidi usio na shaka wa kiongozi kama huyu kuchochea uvunjifu wa amani na ukiukwaji wa sheria za nchi. Unavaa zako jezi ya Mamelodi, lolote litakalokukuta siku hiyo uwanjani mbona watakulipa tu vizuri. Utaanzia mahakama zetu hadi huko CAF na FIFA hadi kieleweke.
 
Amefanya ujinga wa hali ya juu. Utanyimaje mtu kuingia uwanjani kwa sababu amevaa jezi ya timu pinzani? Hili linatakiwa kufikishwa CAF na FIFA ili uwanja ufungiwe?
 
Wangeelimisha watu kwa njia za kawaida, mbona watu ni waelewa sana ila kutishana ndiyo kutaongeza ukaidi. Lakini jambo la msingi ni kauli yake linajenga picha ya uhasama sehemu ya burudani. Halafu huyu si alikuwa kwenye Wizara ya Sheria na baadae Utalii? Kauli zake inaonyesha ha fit kote huko wala huku kwenye michezo.

Hao waarabu tunaodhani tunawaiga hizi figisu si ndiyo hao wanaporomoka sasa hivi?
 
Hizi siasa wapelekeeni familia zenu huko msituletee chokochoko kabisa. Tulipokuwa tunahangaikia hii league yetu mlikuwa huko matakomeni mnakunywa kahawa. SASA mpira wetu umekua mnaleta visheria vyenu vya kisiasa hapa.
Kwenye mpira wakusema ni mmoja Tu...mmiliki WA Azam TV. He knows how far he has brought this game.

Wengine kakojoe mlale na jezi tutazivaaaaa.....
Uzalendo kwani hizi timu ni taifa stars? Mmmmm
 
B... Mi hili suala naunga mkono 100% tena tumechelewa sana. Tumekuwa kama wendawazimu kushangilia wageni.
Sawa, utani upo tutaniane (kama mimi ile siku ya Wydad japo najutaga sana) ila sio katika kiwango tulichofikia cha kuujaza uwanja kushangilia wageni.

Watakaokiuka wageuzwe mfano, na iwe serious maana nchi yetu hii utekelezaji sifuri.
Haya yatawekeza kama ukiweza kuirudisha dunia nyuma kwa miaka 100. Dunia ya sasa watu wamestaarabika na michezo ni buruduni na siyo udikteta. Kila mtu yuko huru kushangilia timu yake anayoamua. Kwanza habari za kipumbavu kama hizi zikifika kwenye mashirikisho ya mpira kama CAF au FIFA viwanja vinaweza kufungiwa. Katika kandanda hakuna upande unaoheshimiwa kama mashabiki. Bila mashabaki hakuna kandanda.
 
Ukija uwanja wa Taifa ukiwa umevaa jezi ya Mamelodi Sundowns lazima utuoneshe passport ya Afrika Kusini na ukiwa na jezi ya Al Ahly utuoneshe passport ya Misri, nje na hapo Polisi watakuchukua ukapumzike” Damas Ndumbaro, Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo.

Yapi maoni yako?

View attachment 2939197
Huyo waziri hana Akili timamu.
Hivi hajui kuwa Yanga na Simba nazo zitakwenda kucheza ugenini, na huko pia zina mashabiki wa kutosha ambao watatamani waingie uwanjani kuzishangilia, nini watafanyiwa?
 
Back
Top Bottom