Tetesi: Ndumbaro kutumbuliwa: FiFa huenda ikaifungia Tanzania

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
14,047
20,411
Kauli ya Waziri wa Michezo Ndugu Ndumbaro kuagiza wananchi watakao-vaa jezi ya Mamelodi au ya Al ahly wakamatwe na kupelekwa polisi ama waingie kwa Passport imeleta sintofahamu.

Chama cha Soka CAF kimepenyezewa habari hii na huenda kama kawaida wananchi watakao ingia na jezi hizo watakamatwa basi huenda tukafungiwa mashindano ya CHAN 2027 na pia kuondoshwa uanachama kwa muda.

Kauli hii ni kuwapangia mashabiki furaha na huzuni. Shabiki wa Simba anapata furaha Yanga ikifungwa na Yanga anapata furaha Simba ikifungwa kitu ambaco kimeifanya kuwa kati ya Dabi kubwa kabisa Afrika na hata duniani Simba na Yanga ni dab ya 15 kwa umaarufu.

Tanzania tuna ubalozi wa South Afrika, tuna Ubalozi wa Misri na wamesikia na wameripoti nchini mwao, hii ni aibu na mpaka usiku huu Mtoa tamko yupo kwenye utumishi wa Umma.

Dkt Samia ameweka mtu ambaye amefeli kwenye Wizara zaidi ya 2 na hapa hajui impact ya agizo lakeambalo limeishusha CCM pakubwa, anaingilia michezo na kudhibiti washangiliaji na wazomeaji.

Serikali inaingilia michezo.
Itashangaza sana kama bado atachwa kwenye michezo.
 
Wamtumbue tu au la si hivyo atengue kauli yake.

Why watupangie timu za kushabikia na viingilio ni vyetu.

Yeye akaweke sheria hizo kwa wanae.

La si hivyo bongo tunafungiwa soka

Mimi nashauri wachalazwe na viboko. Hatuwezi kuishi na binadamu ambao hawana tofauti na nyumbu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
KUcharazwa viboko haisaidii, Atenguliwe tu, huenda hatoshei uwaziri.
 
Mie nishanunua jezi yangu ya Al ahly toka juzi siku ikifika naitinga zangu naingia uwanjani alafu dogo namkabidhi simu awe ananirekodi live anayeweza aje anikamate
 
Back
Top Bottom