Msemaji Mkuu wa Serikali Mobhare Matinyi ametoa ufafanuzi kuhusu kauli ya Waziri wa Utamaduni, Sanaa na michezo Dkt Damas Ndumbaro

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
10,255
12,754
Msemaji Mkuu wa Serikali Mobhare Matinyi ametoa ufafanuzi kuhusu kauli ya Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Damas Ndumbaro kwamba Shabiki atakayekwenda uwanjani kutazama mechi za Kimataifa za Simba na Yanga anapaswa kuvaa jezi za Simba au Yanga kinyume na hapo atalazimika kuwa na passport ya Nchi ambayo klabu anayoishangilia inatokea au vinginevyo hatoruhusiwa kuingia uwanjani.

Msemaji Mkuu katika ufafanuzi wake leo amesema Waziri alikuwa anahamasisha tu uzalendo wa Timu na hakumaanisha kuwa kweli Watu watazuiliwa kisa pasport.

“Alichozungumza Mh. Waziri (Dkt.Ndumbaro) alikuwa anahamasisha uzalendo wa Timu zetu na katika lugha zetu za michezo Waandishi wa Michezo tunafahamu, Mimi niliwahi kuwa wakati fulani Mwandishi wa Michezo na niliwahi kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo (TASWA) sisi tukizungumza 80% ni utani, 20% tunazungumza vitu vimekaa vimenyooka”

“Ukizungumza habari zinazohusisha Simba na Yanga, ukang’ang’ana kuzungumza kitu kama kilivyoandikwa mahali fulani hivi inafika mahali unawachosha Watu, hizi ni Timu zinazopenda utani ni Timu zinazopokea ujumbe wakati mwingine kwa lugha rahisi, si kweli kwamba Mh. Waziri alimaanisha pale itakaguliwa pasport, anayejua pasport halali na isiyo halali ni Idara ya Uhamiaji, hakusema Idara ya Uhamiaji itaenda uwanjani pale”

“Kwahiyo katika ushabiki huohuo wa mpira Watu wamelifanya jambo hili la mzaha wamelikuza mpaka Mamelodi wamesikia wameingia uoga, na wameandikiwa na TFF lakini Mimi niwasihi Watanzania tuwe Wazalendo na tutarajie Mamelodi watafungwa na Al Ahly nao watafungwa magoli ya kutosha” ——— Matinyi.
 
Nimeshangazwa na maelezo hayo
Kwanini Waziri alete utani wa kijinga kwenye mambo makini

Utani gani ulio kinyume cha kanuni, sheria na katiba

Kukagua passport za mashabiki wanaoshanikia
Timu tofauti ya simba na yanga uwanja wa mkapa ni uhuni

Na fifa inaweza kutungia

Rais Samia mtengue waziri kilaza kwenye wizara ya michezo hana uelewa wowote amekuja kutugharimu tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dar Young Africans Tunaenda Kumpiga Goal Nyingi Sana Huyo Mamelod Tena Hao Watakao Kimbilia Uwanjani Na Jezi Zao Za Ubuntu Botho Watazivua Wenyewe Kipindi Cha Kwanza Tu
 
Msemaji Mkuu wa Serikali Mobhare Matinyi ametoa ufafanuzi kuhusu kauli ya Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Damas Ndumbaro kwamba Shabiki atakayekwenda uwanjani kutazama mechi za Kimataifa za Simba na Yanga anapaswa kuvaa jezi za Simba au Yanga kinyume na hapo atalazimika kuwa na passport ya Nchi ambayo klabu anayoishangilia inatokea au vinginevyo hatoruhusiwa kuingia uwanjani.

Msemaji Mkuu katika ufafanuzi wake leo amesema Waziri alikuwa anahamasisha tu uzalendo wa Timu na hakumaanisha kuwa kweli Watu watazuiliwa kisa pasport.

“Alichozungumza Mh. Waziri (Dkt.Ndumbaro) alikuwa anahamasisha uzalendo wa Timu zetu na katika lugha zetu za michezo Waandishi wa Michezo tunafahamu, Mimi niliwahi kuwa wakati fulani Mwandishi wa Michezo na niliwahi kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo (TASWA) sisi tukizungumza 80% ni utani, 20% tunazungumza vitu vimekaa vimenyooka”

“Ukizungumza habari zinazohusisha Simba na Yanga, ukang’ang’ana kuzungumza kitu kama kilivyoandikwa mahali fulani hivi inafika mahali unawachosha Watu, hizi ni Timu zinazopenda utani ni Timu zinazopokea ujumbe wakati mwingine kwa lugha rahisi, si kweli kwamba Mh. Waziri alimaanisha pale itakaguliwa pasport, anayejua pasport halali na isiyo halali ni Idara ya Uhamiaji, hakusema Idara ya Uhamiaji itaenda uwanjani pale”

“Kwahiyo katika ushabiki huohuo wa mpira Watu wamelifanya jambo hili la mzaha wamelikuza mpaka Mamelodi wamesikia wameingia uoga, na wameandikiwa na TFF lakini Mimi niwasihi Watanzania tuwe Wazalendo na tutarajie Mamelodi watafungwa na Al Ahly nao watafungwa magoli ya kutosha” ——— Matinyi.
Miungu watu isiyotaka kuonekana inakosea.

Waziri alisema HATANII, sasa inakuwaje tunaambiwa tena na Semaji kuwa Waziri alikuwa anatania?
 
huyu msemaji nae kamwagia petroli kwenye fukuto, katukana tasnia nzima ya habari za michezo

"Mimi niliwahi kuwa wakati fulani Mwandishi wa Michezo na niliwahi kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo (TASWA) sisi tukizungumza 80% ni
utani, 20% tunazungumza vitu vimekaa vimenyooka”

Eti waandishi wa habari za michezo wanaongea pumba 80% of the time. Suala la michezo, ambalo lina waziri,wizara, bajeti za mabilioni ya kujenga viwanja, ajira, tena ajira hii huko duniani ni ajira lucrative kuliko zozote duniani, kumbe kwetu ni suala la utani tu
 
Waziri Damas ndumbaro akiwapatanisha OKW BOBAN SUNZU pamoja na NALIA NGWENA

IMG-20240322-WA0002.jpg
 
Back
Top Bottom