Dah! Vijana wenye vigari mjini wanatamba sana

Dah! Vijana wenye vigari mjini wanatamba sana

Hivyo vigari ni kwa ajili ya kulia mademu wajinga tuu lakini heshima iko kwenye nyumba japo haipendezi una nyumba afu huna usafiri japo pikipiki
 
Maisha ni mipango/kupanga na kupanga ni kuchagua. Tusipangiane cha kufanya na cha kutokufanya ila ni vizuri KUSHAURIANA. Na ushauri haulazimshwi. Mtu anaamua mwenyewe kuukubali au kuukataa ushauri anaopewa.
 
Tatizo huwezi kutofautisha gari ya mkopo na ya kununua cash........tunaomba vyombo husika vipendekeze alama maalum kwa magari ya mkopo ili tuheshimiane BAR
Kwamba gari ilionunuliwa kwa mkopo sio gari hio enh?
 
Nawe tembea na nyumba yako... hujakatazwa
Yaani siku hizi watembea kwa miguu na wenye baiskeli tunanyanyasika Sana na Hawa vijana wenye magari ya mkopo huku Kitaa

Yani kijana akishakopa milioni 10 akanunua gari basi anataka atambe nalo kila bar na kutembea kwa kujitanua huku akining'iniza funguo ili kila mtu amuone anamiliki gari

Wadada nao ndo wanashoboka wakiona kijana kaingia na gari bar yani wanamwona bonge la digala kutembea na Ist

Vijana wenye magari wakiingia bar wanataka kujifanya wao kina MO wanakunywa Pombe laini tu yani serengeti lite, castle lite, Henekien, Windhoek au savannah hawataki masuala ya Safari au serengeti lager wala Balimi extra lager

Ni ushamba na uboya kutamba na gari lako mtaani wakati unaishi nyumba ya kupanga chumba kimoja self na sebule.
 
Kumbuka kila mwenye gari aina yoyote ana uwezo wa kujenga lakini sio kila mwenye nyumba ana uwezo wa kununua na kutunza gari?... halafu watu wanafikiri kujenga nyumba ni kuwa na akili ya maisha!, halafu kuwa na nyumba mbona ni suala la kawaida sana, mbona kijijini kwetu kila mwanamme ana nyumba... heshima gari
-Ni ujinga kununua gari wakati hujajenga
-Gari kwa nature yake ni liability i.e unajaza mafuta,service, fine za barabarani unless uwe na vyanzo vingine vya mapato
-unakopea mshahara, ukitoa makato kinachobaki hicho hicho ule,ulipe kodi,ujaze petrol,unywee bia,uhonge
 
Kumbuka kila mwenye gari aina yoyote ana uwezo wa kujenga lkn sio kila mwenye nyumba ana uwezo wa kununua na kutunza gari?...halafu watu wanafikiri kujenga nyumba ni kuwa na akiri ya maisha!, halafu kuwa na nyumba mbona ni suala la kawaida sana,mbona kijijini kwetu kila mwanamme ana nyumba...heshima gari
  • Sio kweli,
  • Bei ya gari hadi milioni5, 6, 7 unapata, bei ya kujenga nyumba ya kawaida tu inaweza kufika hadi 30M+
  • Kujenga ndiyo moja ya indicator ya kwamba una akili ya maisha kwa sababu nyumba ni Mali inayopanda thamani compared to gari ambalo linashuka thamani
    [*]Nyumba unaweza kukopea mkopo mkubwa ukaweka rehani wakati Vitz,ist unaweza kukopea hela kidogo sana
    [*]Heshima ni gari kwa wasiotambua umuhimu wa realestate

Sasa kila mmoja mwenye pesa zake si ananunua gari kulingana na mahitaji yake!! Kama huna, tumia usafiri wa umma tu. Gari halimfanyi mtu ashindwe kujenga, bali ni mipango ya mtu. Mimi nilianza na gari, na sasa ninajenga.
  • Tutaamini vipi kwamba unajenga?
  • Gari linaweza kukufanya usijenge hususan wale wenye vipato vidogo waliojiingiza kwenye mikopo ya magari.
 
-tutaamini vipi kwamba unajenga?
-Gari linaweza kukufanya usijenge hususan wale wenye vipato vidogo waliojiingiza kwenye mikopo ya magari.
Sihitaji kukuthibitishia hilo. Ila experience yangu ni kwamba nilianza na gari, na si la mkopo na sasa ni ujenzi, na sichukui mkopo. Either way, kama gari litamfanya mtu asijenge, basi hilo gari halifai na huyo mtu bado hana uwezo wa kumiliki gari. Kumiliki gari ambalo linagharimu laki na nusu au mbili kwa mwezi, likimfanya mtu ashindwe kujenga, basi aliuze tu maana halina tija.
 
-Ni ujinga kununua gari wakati hujajenga
-Gari kwa nature yake ni liability i.e unajaza mafuta,service, fine za barabarani unless uwe na vyanzo vingine vya mapato
-unakopea mshahara, ukitoa makato kinachobaki hicho hicho ule,ulipe kodi,ujaze petrol,unywee bia,uhonge
Acha hizo wewe ujenge? Utakufa bila kuendesha gari yako hayaaa weeee!
Kama uko hivyo huna akili wewe ni division zero au hukuna kabisa drs. Ngoja nikusaidie
Kwanza huna hobbie na gari. Japo unajulikana Nyumba wataijua majirani tu.

Ukiwa na akili gari utajenga faster kwanza. Unaaminiwa.
Utakodiwa hata na jirani wenye shida.
Jirani rafiki asiye na gari watakutafuta uwawaishe ubungo.
Unasanya jioni na asubuhi.
Ukitoka kazini
Wakitaka lift unasema kirahisi tu hela ya mafuta.
Foleni zoote hizo ukose hela si utakuwa. Mburula wa kutupa. Hata shwewitani hakutamani.

Mtu gani usiyependwa hata na shetani muovu. Shtani anaandaliwa kuwa kuni.sasa wewe utakuwa majani ya kukolezea moto wa kumuangamiza shweitani. UkiziPata kula maisha tembelea matako.
tatizo baba zenu hawakuwa nayo mukaona na kuijua raha yake hata mushipa wa gari huna. Wenzako licha ya nyumba huko mbali.
Hata Wala mashuka hana kitanda mambo yote down kwa down tu lkn gari lazima.

Lakini gari lazima piga ua garagaza. Hawakaribishagi watu makwao hao halafu inakuzuia kuwa malaya utampeleka wapi na gheto huna.

Wewe unataka umalaya na sifa. Sana utaishia kijinyonga tu siku kakigongwa na ni rahisi kugongwa maana huna limit. Zaidi ya kufanya show off!. Mara wende nako kanisani.
Mara ukanunue matikiti chalinze heeee!
Huyu asiye na nyumba anawaza kuipata ataitumia gari yake kwa adabu.
 
acha hizo wewe ujenge? Utakufa bila kuendesha gari yako hayaaa weeee!
Kama uko hivo huna akili wewe ni division zero au hukuna kabisa drs. ngoja nikusaidie
Kwanza huna hobbie na gari. Japo unajulikana Nyumba wataijua majirani tu.

ukiwa na akili gari utajenga faster kwanza. unaaminiwa.
Utakodiwa hata na jirani wenye shida.
Jirani rafiki asiye na gari watakutafuta uwawaishe ubungo.
Unasanya jioni na asubuhi.
Ukitoka kazini
Wakitaka lift unasema kirahisi tu hela ya mafuta.
Foleni zoote hizo ukose hela si utakuwa. Mburula wa kutupa. Hata shwewitani hakutamani.

Mtu gani usiyependwa hata na shetani muovu. Shtani anaandaliwa kuwa kuni.sasa wewe utakuwa majani ya kukolezea moto wa kumuangamiza shweitani. UkiziPata kula maisha tembelea matako.
tatizo baba zenu hawakuwa nayo mukaona na kuijua raha yake hata mushipa wa gari huna. Wenzako licha ya nyumba huko mbali.
Hata Wala mashuka hana kitanda mambo yote down kwa down tu lkn gari lazima.

lkn gari lazima piga ua garagaZa. Hawakaribishagi watu.makwao hao halafu inakuzuia kuwa malaya utampeleka wapi na gheto huna.

Wewe unataka umalaya na sifa. Sana utaishia kijinyonga tu siku kakigongwa na ni rahisi kugongwa maana huna limit. Zaidi ya kufanya show off!. Mara wende nako kanisani.
Mara ukanunue matikiti chalinze heeee!
Huyu asiye na nyumba anawaza kuipata ataitumia gari yake kwa adabu.
-Mbona umepanik?
-Hujajibu hoja zangu hata moja
-Mambo uliyoyasema ni Hypothetical yote hujajibu hoja zangu
-Jipange
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Hata nyumba ya kuishi ni liability! Haiingizi pesa na inahitaji ukarabati.
Nyumba kwa TZ si liability labda mbele, ni mtazamo wangu tu.
Ila gari ni muhimu kwa Wachizi kuzivua chupi
 
Gharama ya kukarabati nyumba ni sawa na gharama ya kuendesha gari?

Amini usiamini ni kubwa zaidi

Gari linasaidia kwenye kuingiza kipato ila nyumba haina huo mchango.

Utatumia 35Mil kujenga pesa ambayo huwezi irudisha mapema. Ila gari la 12Mil ndani ya miaka miwili linarudisha hela yote uliyonunulia.

Ukiwa na 35Mil nunua gari la 10Mil na shamba la cha 10Mil Bagamoyo ufuge huko huku town kapangishe kwa 200K ili uweze fanya michongo town
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom