Vijana wanaoenda mijini na kudandia mtumbwi wa vibwengo

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,891
VIJANA WANAOENDA MIJINI NA KUDANDIA MTUMBWI WA VIBWENGO

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Kwenye Wadada 10 basi 8 wanaovaa uchi, wauza nyapu, na wanaofanya mambo ya hovyo basi ni Watu wakuja. Yaani wamekuja mjini wakiwa tayari ni Watu wazima. Wadada 2 ndio wamezaliwa mjini
Halikadhalika na vijana, vijana wengi wanaofanya mambo ya hovyo kwenye majiji makubwa hapa Tanzania. Ukifuatilia kwa umakini utagundua wengi wao ni Watu wakuja, yaani wamekuja mjini wakiwa Watu wazima.

Unaweza ukaanzia na Watu mashuhuri unaowajua kuanzia kwenye media, burudani, siasa, n.k

Kuna wazazi wapo mkoani au vijijini wakihadithiwa mambo ya watoto wao wanayoyafanya huko mijini wanaweza kukukatalia na siku wakishuhudia wengi huishia kupata Stroke na magonjwa yasiyo na mdhamini.

Nenda Bar chunguza wanaoleta fuja au wenye tabia za ajabuajabu utaniambia ukweli wa mambo ninayokuambia.

Taikon kama Mtaalamu wa mahusiano, saikolojia, sosholojia, na Falsafa. Ni rahisi kwa ndoa ya Watu waliozaliwa na kukulia mjini kudumu kuliko ndoa mchanganyiko.

Au ni rahisi ndoa ya waliozaliwa na kukulia kijijini na mpaka sasa maisha watayafanyia kijijini kudumu tofauti na mchanganyiko.

Wengi wakifika mjini hupata mabadiliko hasi yenye madhara.

Kijana alipokuwa kijijini hakuzoea kuona wanawake maelfu kwa maelfu warembo, sasa kafika mjini kakutana na Pisikali zinazojua kuoga na kunukia muda wote. Misambwanda na sura za kimalaika hakuwahi kuziona kwa wingi huko kijijini. Matokeo yake anapiga dole gumba Chini anapiga mzinga.

Demu katoka kijijini hajawahi kukutana na wanaume mabishoo kama kina Taikon, hajawahi kukutana na wanaume wenye swagga na maneno matamu, hajawahi kukutana na wanaume wenye magari na majumba ya kifahari. Yote hayo hajawahi. Huko kijijini alipotoka alizoea kuwasikia vijana wa huku wakizungumza kwa lafudhi nzito ya kilugha cha kabila lako.

Leo kakutana na Taikon Master mwenye mchanganyiko wa lafudhi na mwenye uwezo wa kuiperemba lafudhi kwa sauti ya kizungu au kispanyola, mtoto anabaki kuchekacheka akiwa amepagawa, anajiona kama yupo kwenye filamu za Telenovela.

Kwa nini asikuache, kwa nini asibadilike.

Kule kijijini amezoea kijana mwenye kazi yake hana hata Friji au Flat TV. Anakuja mjini anakuta kijana hana kazi yoyote ya kueleweka lakini anamiliki vitu vya kimaajabu. Nusu ya ukuta wa chumba cha msela wa mjini imezibwa na TV kubwa. Unafikiri hata badilika?

Huko kijijini hakuna msusi wa maana, wala kinyozi wa maana. Binti wa Watu hakuwahi kujiona kapendeza, hata akisuka anazuga tuu. Kafika mjini kakuta sio tuu wasusi ila mpaka mafundi kucha.

Binti kafika mjini kajiona kituko sio tuu kwa namna ya uvaaji wake bali hata muonekano na uongeaji wake. Hapo kajikalia kimya kutimiza unabii wa wahenga kubwa jogoo la shamba haliwiki mjini. Haya kasuka mtoto huyo!

Huyo! Sura imeitikia kama kiitikio cha Uefa Champion. Fundi kucha kafanya yake, mguu unang'aa ungedhani mtoto kazaliwa pre-mature kabla ya siku zake. Magaga na makarara yametolewa. Hataki kuamini kama zile ni kucha zake jinsi zilivyopendeza. Nani hapendi hayo.

Binti gani hapendi kupita mitaani macho ya vijana na wababa na wazee wa busara na wale wa hovyo yakimkodolea kwa hamu isiyokuwa na nidhamu.

Yule aliyekuwa haitwi leo aitwa. Yule aliyekuwa haangalii leo yuaangaliwa.

Insight yake mitongozo imeongezeka maradufu.

Maringo na kiburi vilivyokuwa haijulikani kwake vinaanza kumea.

Sasa siku hizi hasalimii. Mwezi unapita.

Lakini anakuja kugundua kuwa lile wigi na kucha aliloviweka kumbe vinachakaa. Pesa hana. Mwenyeji wake alitaka tuu kumuonjesha kama mwalimu wa Sigara. Fegi ya kufundishiwa utapewa bure lakini ya kutumia ukishajua utajua pakuipata.

Wigi lachukiza
Kucha zinababuka,
Mafuta ya kupaka yameisha.

Wapi atapata pesa na kazi hana. Kazi sio kwamba hazipo lakini elimu yake ya kuungaunga. Aaanh! Taikon wapo waliosoma, kweli wapo waliosoma, elimu unayo kazi hauna kwa sababu hakuna anayekujua.

Hapo ndipo mtu anapoamua kupanda mtumbwi wa vibwengo. Unajua mtumbwi wa vibwengo bhana siku moja nilienda pale bandarini kuutazama ili kujua ni mtumbwi wa aina gani. Sijui niseme maana nishaanza kutoka nje ya mada. Anyway ni kawaida yangu kurukia rukia mambo.

Nilipofika bandarini niliona Mitumbwi mingi sana. Huu iliyapa macho yangu ubize wa kuona ni wapi ilipoegeshwa Mtumbwi wa vibwengo. Lakini sikuuona. Kumbe mtumbwi wa vibwengo hatiagi nanga kama ilivyomitumbwi mingine.
Wenyewe ili upande sharti upige mbuzi kuufuata na wakati wa kushuka halikadhalika lazima upige mbizi kwenda Ufukweni ukitoka mtumbwini.

Hayo ningeyajulia wapi kama sio huko bandarini kwa wataalamu. Unaambiwa kuwa kama hujui kuogelea kupanda mtumbwi wa vibwengo ni jaribio la kujiua. Kupona hapo ni Bahati tuu.

Basi ndio hivyo bhana. Binti kuogelea sijui kama alikuwa anajua. Lakini huyo karukia majini kuufuata mtumbwi wa vibwengo. Tapatapatapa! Kutapatapa mtoto wa kike kujitetea huko majini anakutana na vijana wakiume nao wanayapigania maisha yao. Kumeza mafumba ya maji na mikojo ya vibwengo.
Ndio hapo mabinti kuwa Masanga, Malaya, kuuza madawa ya kulevya, wengine wengi vijana kuwa mashoga, ving'asti, makuwadi, mapunda na kashkash zingine na mtumbwi wa vibwengo.

Unajua Taikon niliwahi kuandikaga barua ya kuomba kazi ya unahodha wa mtumbwi wa vibwengo. Mpaka leo bado sijajibiwa. Lengo langu ni kuwasaidia hawa vijana wenzangu. Yaani siku nikipewa kazi ya kuendesha mtumbwi wa vibwengo vijana wote mliojitupa majini mmepata mwokozi.

Vijana msiyapapatikie maji ya bahari
Kuogelea yahitaji taji na umahiri.
Mafunzo ya vijiji mlonayo ni utajiri
Msiendekeze Ushkaji mtakufa kikafiri.

Nikakumbuka habari za mjusi Kafiri, sitaki kukumbuka yule Demu aliyekuwa akimfuga yule mjusi. Hii stori inasikitisha sana. Sijui nini kimetokea kwenye akili yangu mpaka neno kafiri likawa kama batani ya kufungulia filamu ya mjusi kafiri na Mrembo wa jiji katika fikra zangu.
Acha nipumzike nitasimulia stori hii siku nyingine. Akili yangu inabembea kama bembea ya Makaburini ambayo juu yake imekaa maiti anayembembeshwa huku na huku. Hiyo nayo ni simulizi nyingine.
Hapa nilikuwa nataka kuwaaga lakini nashindwa namna ya kuwaaga.

Babu yangu alikuwa akiimbaga wimbo huu wakati akiaga;
"Goodbye my dear friend I am going Faraway,
We shall meet for another time,
When God wishes"

Ahsante! Asante! Asante Sana!

Nawatakia maandalizi mema ya Sabato.
Jioni nikiamka nitawasalimu tena.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
🤣🤣🤣🤣 vijana wanapoingia mijini kutoka huko maporini wanataka kujua kila kitu kuliko sisi ma born town at C, mwisho wa siku wanageuka mashoga, wauza nyapu, machawa na ujinga wote, me huwa na nawazoom...
 
Hayo yote yanatokana na msemo kwenye wengi kuna mengi basi siyo zaidi ya hapo

Uwepo wa mchanganyiko mkubwa wa watu unaleta vurugu nyingi siyo kwamba wazawa ni wajanja sana kuliko wengine hapana

Mafikizolo tunaijua bara na pwani vyedi
Huwezi kuijua pwani tu ukajiita mjanja kuliko sisi
8 kwa 2 kama ulivyosema hapo juu ukiitafsiri vizuri kutokana na idadi ya watu iliyopo hapa mjini hii 2 ni kubwa sana tena sana kuliko hiyo nane
Maana yake hawa uliyowapa 2 wamepotea sana
 
I think you are right.yea you are always right taikon.mabandiko yako yamekua muongozo mzuri Sana kwangu.keep it up
 
VIJANA WANAOENDA MIJINI NA KUDANDIA MTUMBWI WA VIBWENGO

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Kwenye Wadada 10 basi 8 wanaovaa uchi, wauza nyapu, na wanaofanya mambo ya hovyo basi ni Watu wakuja. Yaani wamekuja mjini wakiwa tayari ni Watu wazima. Wadada 2 ndio wamezaliwa mjini
Halikadhalika na vijana, vijana wengi wanaofanya mambo ya hovyo kwenye majiji makubwa hapa Tanzania. Ukifuatilia kwa umakini utagundua wengi wao ni Watu wakuja, yaani wamekuja mjini wakiwa Watu wazima.

Unaweza ukaanzia na Watu mashuhuri unaowajua kuanzia kwenye media, burudani, siasa, n.k

Kuna wazazi wapo mkoani au vijijini wakihadithiwa mambo ya watoto wao wanayoyafanya huko mijini wanaweza kukukatalia na siku wakishuhudia wengi huishia kupata Stroke na magonjwa yasiyo na mdhamini.

Nenda Bar chunguza wanaoleta fuja au wenye tabia za ajabuajabu utaniambia ukweli wa mambo ninayokuambia.

Taikon kama Mtaalamu wa mahusiano, saikolojia, sosholojia, na Falsafa. Ni rahisi kwa ndoa ya Watu waliozaliwa na kukulia mjini kudumu kuliko ndoa mchanganyiko.

Au ni rahisi ndoa ya waliozaliwa na kukulia kijijini na mpaka sasa maisha watayafanyia kijijini kudumu tofauti na mchanganyiko.

Wengi wakifika mjini hupata mabadiliko hasi yenye madhara.

Kijana alipokuwa kijijini hakuzoea kuona wanawake maelfu kwa maelfu warembo, sasa kafika mjini kakutana na Pisikali zinazojua kuoga na kunukia muda wote. Misambwanda na sura za kimalaika hakuwahi kuziona kwa wingi huko kijijini. Matokeo yake anapiga dole gumba Chini anapiga mzinga.

Demu katoka kijijini hajawahi kukutana na wanaume mabishoo kama kina Taikon, hajawahi kukutana na wanaume wenye swagga na maneno matamu, hajawahi kukutana na wanaume wenye magari na majumba ya kifahari. Yote hayo hajawahi. Huko kijijini alipotoka alizoea kuwasikia vijana wa huku wakizungumza kwa lafudhi nzito ya kilugha cha kabila lako.

Leo kakutana na Taikon Master mwenye mchanganyiko wa lafudhi na mwenye uwezo wa kuiperemba lafudhi kwa sauti ya kizungu au kispanyola, mtoto anabaki kuchekacheka akiwa amepagawa, anajiona kama yupo kwenye filamu za Telenovela.

Kwa nini asikuache, kwa nini asibadilike.

Kule kijijini amezoea kijana mwenye kazi yake hana hata Friji au Flat TV. Anakuja mjini anakuta kijana hana kazi yoyote ya kueleweka lakini anamiliki vitu vya kimaajabu. Nusu ya ukuta wa chumba cha msela wa mjini imezibwa na TV kubwa. Unafikiri hata badilika?

Huko kijijini hakuna msusi wa maana, wala kinyozi wa maana. Binti wa Watu hakuwahi kujiona kapendeza, hata akisuka anazuga tuu. Kafika mjini kakuta sio tuu wasusi ila mpaka mafundi kucha.

Binti kafika mjini kajiona kituko sio tuu kwa namna ya uvaaji wake bali hata muonekano na uongeaji wake. Hapo kajikalia kimya kutimiza unabii wa wahenga kubwa jogoo la shamba haliwiki mjini. Haya kasuka mtoto huyo!

Huyo! Sura imeitikia kama kiitikio cha Uefa Champion. Fundi kucha kafanya yake, mguu unang'aa ungedhani mtoto kazaliwa pre-mature kabla ya siku zake. Magaga na makarara yametolewa. Hataki kuamini kama zile ni kucha zake jinsi zilivyopendeza. Nani hapendi hayo.

Binti gani hapendi kupita mitaani macho ya vijana na wababa na wazee wa busara na wale wa hovyo yakimkodolea kwa hamu isiyokuwa na nidhamu.

Yule aliyekuwa haitwi leo aitwa. Yule aliyekuwa haangalii leo yuaangaliwa.

Insight yake mitongozo imeongezeka maradufu.

Maringo na kiburi vilivyokuwa haijulikani kwake vinaanza kumea.

Sasa siku hizi hasalimii. Mwezi unapita.

Lakini anakuja kugundua kuwa lile wigi na kucha aliloviweka kumbe vinachakaa. Pesa hana. Mwenyeji wake alitaka tuu kumuonjesha kama mwalimu wa Sigara. Fegi ya kufundishiwa utapewa bure lakini ya kutumia ukishajua utajua pakuipata.

Wigi lachukiza
Kucha zinababuka,
Mafuta ya kupaka yameisha.

Wapi atapata pesa na kazi hana. Kazi sio kwamba hazipo lakini elimu yake ya kuungaunga. Aaanh! Taikon wapo waliosoma, kweli wapo waliosoma, elimu unayo kazi hauna kwa sababu hakuna anayekujua.

Hapo ndipo mtu anapoamua kupanda mtumbwi wa vibwengo. Unajua mtumbwi wa vibwengo bhana siku moja nilienda pale bandarini kuutazama ili kujua ni mtumbwi wa aina gani. Sijui niseme maana nishaanza kutoka nje ya mada. Anyway ni kawaida yangu kurukia rukia mambo.

Nilipofika bandarini niliona Mitumbwi mingi sana. Huu iliyapa macho yangu ubize wa kuona ni wapi ilipoegeshwa Mtumbwi wa vibwengo. Lakini sikuuona. Kumbe mtumbwi wa vibwengo hatiagi nanga kama ilivyomitumbwi mingine.
Wenyewe ili upande sharti upige mbuzi kuufuata na wakati wa kushuka halikadhalika lazima upige mbizi kwenda Ufukweni ukitoka mtumbwini.

Hayo ningeyajulia wapi kama sio huko bandarini kwa wataalamu. Unaambiwa kuwa kama hujui kuogelea kupanda mtumbwi wa vibwengo ni jaribio la kujiua. Kupona hapo ni Bahati tuu.

Basi ndio hivyo bhana. Binti kuogelea sijui kama alikuwa anajua. Lakini huyo karukia majini kuufuata mtumbwi wa vibwengo. Tapatapatapa! Kutapatapa mtoto wa kike kujitetea huko majini anakutana na vijana wakiume nao wanayapigania maisha yao. Kumeza mafumba ya maji na mikojo ya vibwengo.
Ndio hapo mabinti kuwa Masanga, Malaya, kuuza madawa ya kulevya, wengine wengi vijana kuwa mashoga, ving'asti, makuwadi, mapunda na kashkash zingine na mtumbwi wa vibwengo.

Unajua Taikon niliwahi kuandikaga barua ya kuomba kazi ya unahodha wa mtumbwi wa vibwengo. Mpaka leo bado sijajibiwa. Lengo langu ni kuwasaidia hawa vijana wenzangu. Yaani siku nikipewa kazi ya kuendesha mtumbwi wa vibwengo vijana wote mliojitupa majini mmepata mwokozi.

Vijana msiyapapatikie maji ya bahari
Kuogelea yahitaji taji na umahiri.
Mafunzo ya vijiji mlonayo ni utajiri
Msiendekeze Ushkaji mtakufa kikafiri.

Nikakumbuka habari za mjusi Kafiri, sitaki kukumbuka yule Demu aliyekuwa akimfuga yule mjusi. Hii stori inasikitisha sana. Sijui nini kimetokea kwenye akili yangu mpaka neno kafiri likawa kama batani ya kufungulia filamu ya mjusi kafiri na Mrembo wa jiji katika fikra zangu.
Acha nipumzike nitasimulia stori hii siku nyingine. Akili yangu inabembea kama bembea ya Makaburini ambayo juu yake imekaa maiti anayembembeshwa huku na huku. Hiyo nayo ni simulizi nyingine.
Hapa nilikuwa nataka kuwaaga lakini nashindwa namna ya kuwaaga.

Babu yangu alikuwa akiimbaga wimbo huu wakati akiaga;
"Goodbye my dear friend I am going Faraway,
We shall meet for another time,
When God wishes"

Ahsante! Asante! Asante Sana!

Nawatakia maandalizi mema ya Sabato.
Jioni nikiamka nitawasalimu tena.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Ushawahi kujiiza matatizo ya mjini kama hayo ya street children, homeless na prostitute kwa nn yanaroot na watu kutoka rural areas na background ya mvurugano wa familia na umaskini?
 
Siyo kweli hata hapa mjini watoto kibao wanakata ringi na kuingia mitaani kuanza maisha mapya ya uchokoraa
Sawa tu na huko mikoani kuja huku

Sijui kama umenielewa hapo juu?

Dar es salaam ni mkoa mmoja Tanzania inayo mikoa zaidi ya 20

Ukitaka kuelewa ninachosema
Chukua idadi ya hao wanaofanya huo uchafu ugawanye kwa mikoa yote uangalie kila mkoa una idadi gani lazima uikute dar es salaam ina idadi kubwa kwa sababu ya huu ugeni uliowaletea vurugu wenyeji
 
Daah! Kama ndo nazi,umiikuna kwlkwl!!!!....🤮😁
 
Back
Top Bottom