Dah! Vijana wenye vigari mjini wanatamba sana

Dah! Vijana wenye vigari mjini wanatamba sana

Mimi bwana sio mpenz wa magari ila gari ni kitu cha lazima sana na kwakwel nimekua namuonea huruma sana wife na madogo adha za kukimbizana kwenye daladala.Mwaka huu gari lazimaaa.Piga ua
Hahahah gari inasaidia sana mkuu
 
Ugumu wa maisha huu [emoji41][emoji41][emoji41]
 
Mimi huwa nashangaa hivi funguo za gari zikiwekwa mfukoni kama funguo za nyumba au ofisi inakuwaje? Unakuta zimeshikwa mkononi muda wote hata akitaka kuelekeza kitu anaelekeza kwa kunyoosha funguo kulikoni???
 
Yaani siku hizi watembea kwa miguu na wenye baiskeli tunanyanyasika Sana na Hawa vijana wenye magari ya mkopo huku Kitaa

Yani kijana akishakopa milioni 10 akanunua gari basi anataka atambe nalo kila bar na kutembea kwa kujitanua huku akining'iniza funguo ili kila mtu amuone anamiliki gari

Wadada nao ndo wanashoboka wakiona kijana kaingia na gari bar yani wanamwona bonge la digala kutembea na Ist

Vijana wenye magari wakiingia bar wanataka kujifanya wao kina MO wanakunywa Pombe laini tu yani serengeti lite, castle lite, Henekien, Windhoek au savannah hawataki masuala ya Safari au serengeti lager wala Balimi extra lager

Ni ushamba na uboya kutamba na gari lako mtaani wakati unaishi nyumba ya kupanga chumba kimoja self na sebule.
Sigara kali unateseka ukiwa wapi ndugu
 
Mi huwa nashangaa hivi funguo za gari zikiwekwa mfukoni kama funguo za nyumba au ofisi inakuwaje?Unakuta zimeshikwa mkononi muda wote hata akitaka kuelekeza kitu anaelekeza kwa kunyoosha funguo kulikoni???
Hahahaha kwa hiyo Mkuu unakereka sana sio????
 
Mi huwa nashangaa hivi funguo za gari zikiwekwa mfukoni kama funguo za nyumba au ofisi inakuwaje?Unakuta zimeshikwa mkononi muda wote hata akitaka kuelekeza kitu anaelekeza kwa kunyoosha funguo kulikoni???
Nadhani sababu ni ile kuziunganisha na vifunguo vingine na hivyo kukunyima comfortability vikiwa mfukoni. Sababu ya kuunganisha na funguo zingine ni kupunguza chance ya kuzipoteza na pia urahisi wa kuziona zikipotea. Ndio maana wengi hupenda kuzishika mkononi.
Hiyo ndiyo sababu ninayohisi mimi.

Najaribu kuwa +ve.
 
Mtoa mada kaongea jambo ambalo wengi wenu ndilo mnaloliwaza mioyoni.

Kiufupi kaziwakilisha chuki na husda zenu kwa ufasaha sana.

Lakini wengi wanamponda hapa kinafiki huku viroho vyao vinasema "yes yes".

Jamani tuwe wawazi. Wivu ni hisia ya asili ya binadamu.

Kuwa na wivu ni jambo la kawaida tu. Sio swala la aibu wala kuficha ficha.

Kama wivu umekukaba kooni we jimwage tu utoe makavu yako hadharani.
 
Mna Nyumba Au Vibanda, Uwe na Nyumba Hasa ya Maana, Ushindwe kuwa Na Usafiri?
Baelezee Baba mkuru wana kijiji mkuu shiida hawajui.eti yale mabanda km ya kipawa yasiyo kuwa kwenye ramani wanaita nyumba.

Hawana maji ya bomba barabara hazipiti.yaani kujenga hovyo hovyo.juu ya bomba la mafuta.duu!!

Nyumba.Masaki huko.Sinza.Kamunyonge Biafra .Mbezi Beach nk ni
Huguswi mpaka unakufa vizazi na vizazi.
 
Yaani siku hizi watembea kwa miguu na wenye baiskeli tunanyanyasika Sana na Hawa vijana wenye magari ya mkopo huku Kitaa

Yani kijana akishakopa milioni 10 akanunua gari basi anataka atambe nalo kila bar na kutembea kwa kujitanua huku akining'iniza funguo ili kila mtu amuone anamiliki gari

Wadada nao ndo wanashoboka wakiona kijana kaingia na gari bar yani wanamwona bonge la digala kutembea na Ist

Vijana wenye magari wakiingia bar wanataka kujifanya wao kina MO wanakunywa Pombe laini tu yani serengeti lite, castle lite, Henekien, Windhoek au savannah hawataki masuala ya Safari au serengeti lager wala Balimi extra lager

Ni ushamba na uboya kutamba na gari lako mtaani wakati unaishi nyumba ya kupanga chumba kimoja self na sebule.
Jamaa Ana chuki Sana.hawa ndio wanaomchukia mtu akiwa nacho. Nilianza kuwaona nikiwa shule yaani ukifaulu ukamzidi anaumia Sana.
Una demons kwako.ninakuona ukimkuta kijana mdogo amepata ajali Tena umemzidi umri hautomsaidia.
Kumchuki hautomsaidia wewe kuimiliki mkuu.yaani unateseka kwa kuzidiwa pia una egoistic Sana Mana unakiona kuwa wewe ndiye uliyestahili kuimiliki na kushobokewa na wadada. Kakope Sasa na wewe so unajua kuwa wamekopa kakope mkuu.
Yaani bana sijui binadamu wakoje.
Ndo Mana mtu akishapata hela inabidi uwakimbie masikini wenzako Mana wanaumia wewe kula sato samaki huku wao wakila matobolwa utadhani Kama umewanyang'anya hizo samaki na jogoo mkubwa.
Yaani bana hii nchi nikipata hela ya kununua apartment nje nahama fasta Sana.
Na hii ndo sababu huwa sipendi kuishi sehemu ambapo Kuna watu wananifahamu.
Yaani bana mtu anaumia anakuona unaishi nyumba nzuri kuzidi ya kwake.
 
mkuuuu acha roho mbaya mkuuu kama ipo ipo tu pambana ww mwanaume
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom