Bunge lakaribisha maoni, kuhusu mapendekezo ya kuridhia makubaliano mkataba kati ya Tanzania na kampuni ya Saudia kuendesha bandari Dar es Salaam

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Kamati ya Pamoja (Joint Committee) ya Bunge ya Mindombinu na ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) inawaalika wadau kutoa maoni kuhusu Azimio la Bunge kuhusu Mapendekezo ya Kuridhia Makubaliano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai kuhusu Ushirikiano wa Kluchumi na Klamil kwa ajili ya Uendelezaji na Uboreshaji wa Utendaji Kazi wa Bandari Tanzania la Mwaka 2023 /(Intergovemmental Agreement - IGA, between the United Republic of Tanzania and the Emirate of Dubai concerning Economic and Social Partnership for the Development and Improving Performance of Ports in Tanzania).

Mkutano wa kupokea na kusikiliza mani ya wadau (Public Hearing) utafanyika siku ya Jumanne tarehe 06, Juni saa 7:30 mchana katika Ukumbi wa Msekwa "D', Ofisi ya Bunge, Jijini Dodoma.

Kamati inawaalika watu wote wenye maoni kuhusu Azimio hilo kufika kuwasilisha mani yo kabla haujapelekwa katika hatua nyingine. na Vilevile Kamati itapokea maoni kwa njia ya Posta au Barua pepe kwa anuani
ifuatayo:-

Katibu wa Bunge, Ofisi ya Bunge,
10 Barbara ya Morogoro
S.L.P. 941.
40490 Tambukareli

Habari zaidi, soma:
  1. Sakata la DP WORLD: Rais Samia asema Serikali itatafuta mbia wa kuiendesha bandari ya Dar, sasa kuchangia robo tatu ya bajeti ya nchi

Bunge.jpeg
 
Kamati ya Pamoja (Joint Committee) ya Bunge ya Mindombinu na ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) inawaalika wadau kutoa maoni kuhusu.
Kamati ya bunge isiweke mtego eti kupokea maoni. Ni jambo liko wazi kabisa. Hatupaswi kukabidhi nchi yoyote kuendesha bandari zetu.

Watatuhukumu sio vizazi vijavyo ila raia wanaoshuhudia huu uhuni unataka kwenda kutekelezwa. Nchi ina uwezo kabisa kuendesha bandari zake kwa ubora ila hakuna utashi kwa lengo la kujinufaisha vigogo.

Hakuna utaalam hatuna au hatuwezi kujipatia ila kinachohitajika ni uamuzi tu kufanya kazi kwa uadilifu na weledi.
 
Kamati ianzishe uzihapa JF watu watoe maoni yao. Swali la utangulizi kwa nini miaka 10 na si chini ya hapo kwa kuanzia?

Vipengele vya mkataba vinatoa unyumbufu kiasi gani ili serikali kufanya tathmini wakati mkataba ukiendelea kutekelezwa?

Serikali itakuwa na jicho lililowezeshwa kiasi gani na huo mkataba ili kuona nini kinapita hapo bandarini na idadi yake kwa usahihi?

Mimi si mmoja wa wale wanao dhani kukodisha ni uamuzi sahihi, lakini kwa vile walisha amua iwe hivyo basi angalau mkataba uwe ni wa hali shinda shinda kwa kila upande.
 
Barua ya kuomba mapendekezo ya kukodisha bandari kwa miaka 100, Tangazo la kualika wadau limetolewa tarehe 5 alafu siku ya kutoa maoni ni tarehe 6. Hii haijakaa sawa kabisa. Ni nini mnakwepa, mna maana gani ofisi ya bunge?.
Bandari ni yetu sote. Suala la kutoa maoni lilipaswa liwe la wadau wote.
 
Kwanini nchi inauza mali zetu.
Kama tumeshindwa kuiendesha bandari ifungwe,

Aliposema yule spika nchi inauzwa na kazi ikapotea.

Mheshimiwa, angalia maamuzi mengine yasije kukulalamikia hadi ukiwa ahera.
 
Maoni na Ushauri wa Wataalam wa Bunge ulikuwa ni huu - Je ulizingatiwa? Ndio ni kweli Bandari yetu ina shida kubwa hasa ya uzembe, kuendeshwa kwa hasara na upigaji - Je swala la kubinafsisha ni lini ilifanyika Mjadala wa Kitaifa watu watoe maoni- Uwekezaji ni mzuri ila ni hatari sana usipopelekwa kwa umakini na uzalendo. Kwanini miaka 100.

Wataalam a wa bunge wanasemaje? Kutokana na uchambuzi tuliofanya hapo juu, ni maoni na ushauri wetu kuwa, Bunge lipate ufafanuzi kutoka Serikalini katika maeneo machache yafuatayo:-

19 a. Ibara ya 25 (1) inaeleza kuwa kuna shughuli za awali za mradi (Early Project Activities) zitaanza kufanyika mapema baada ya kusainiwa Mkataba. Shughuli za awali za mradi zitafanyika kabla ya Bunge kuridhia Mkataba na kabla ya Mkataba kuanza kutumika rasmi kwa mabadilishano ya Hati za Uridhiaji kati ya Serikali zote mbili.

Shughuli za awali za mradi zimetafsiriwa katika Ibara ya 1 kuwa ni kufanya upembuzi yakinifu pamoja na kufanya tathmini ya kimazingira na kijamii ya mradi huu (environmental and social due diligence), kujenga barabara za muda kuwezesha kufika eneo la mradi, n.k.

Tunashauri Serikali itoe ufafanuzi katika eneo hili, ambapo shughuli za Mradi zinaanza kabla ya Mkataba kuridhiwa na Bunge.

b. Ibara ya 20 kuhusu usuluhishi wa migogoro kufanyika Afrika Kusini na kwa kutumia Sheria za Usuluhishi za Kamisheni ya Umoja wa Mataifa juu ya Sheria zinazohusika na Biashara za Kimataifa (UNICITRAL Arbitration Rules), ni kinyume na maelekezo ya kifungu cha 11 cha Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa Rasilimali na Maliasili ya Mwaka 2017 (The Natural Wealth and Resources [Permanent Sovereignty] Act, 2017).
Sheria tajwa inaelekeza kuwa mgogoro wowote unaotokana na matumizi ya rasilimali na maliasili za nchi hautatatuliwa katika mahakama na mabaraza ya nchi za nje, bali utatatuliwa na vyombo vya sheria vya Tanzania na kwa kutumia sheria za Tanzania.

c. Ibara ya 23 (4) kuhusu kusitisha Mkataba, inaeleza bayana kuwa Serikali husika katika Mkataba hazitakuwa na haki ya kuvunja Mkataba (denounce), kujitoa (withdraw from), kuahirisha (suspend) au kusitisha (terminate) Mkataba katika mazingira yoyote, ikiwa ni pamoja na mazingira ya uvunjaji mkubwa wa masharti ya Mkataba huu (material breach), mabadiliko ya msingi katika mazingira ya utekelezaji Mkataba (fundamental change of circumstances), mgogoro mkubwa wa kidiplomasia (severance of diplomatic or consular relations), au sabau zozote zile zinazotambulika katika sheria za kimataifa.
Masharti ya Ibara hii yanatakiwa kufafanuliwa na Serikali.

d. Muda wa utekelezaji Mkataba huu haujawekwa bayana, bali Ibara ya 23 1) inasema kuwa ukomo wa Mkataba huu ni mpaka hapo shughuli za mradi huu zitakapokuwa zimekamilika. Serikali iombwe kutoa ufafanuzi kuhusu jambo hili la ukomo wa Mkataba.

e. Ibara ya 27 inaweka masharti kwamba, pale ambapo Mkataba huu utaanza kutumika rasmi, Serikali yeyote katika Mkataba huu haitaingia au kuwa sehemu ya makubaliano ya ndani ya nchi au ya kimataifa wakati wa utekelezaji wa Mkataba.

Serikali iombwe kutoa ufafanuzi wa Ibara hii. Mkataba huu haujaweka muda wa ukomo, hivyo Serikali haitakuwa na nafasi ya kuingia makubaliano mengine kuhusu kuendeleza au kuboresha na kuendesha bandari zake.

f. Ibara ya 30 inaweka masharti ya kuwa na uthabiti, uimara na uhakika wa kutoyumbisha Mkataba huu (Stabilization). Eneo hili lipate ufafanuzi wa Serikali. Kwa kuzingatia kuwa Mkataba huu hauna muda wa ukomo. Hivyo, kuna mazingira sheria zitahitaji kufanyiwa mabadiliko kulingana na wakati, ambapo mabadiliko hayo yanaweza kuathiri masharti ya Mkataba huu na kuchukuliwa kuwa ni kuyumbisha Mkataba huu.

g. Kwa upande wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mamlaka ya kusaini mMkataba huu yametolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hata hivyo, kwa upande wa Serikali ya Dubai haijawekwa wazi. Tunashauri Serikali itoe ufafanuzi kuhusu mamlaka ya kusaini Mkataba huu kwa upande wa Serikali ya Dubai
Imeandaliwa na Sekretariati ya Bunge

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanini nchi inauza mali zetu.
Kama tumeshindwa kuiendesha bandari ifungwe,

Aliposema yule spika nchi inauzwa na kazi ikapotea.

Mheshimiwa, angalia maamuzi mengine yasije kukulalamikia hadi ukiwa ahera.
Mzee Malecela ashukuriwe lasivyo “niguse ninuke” tungekuwa tulishamsahau. Ila mi huwa sielewi hii nchi inaendeshwa na nani? Yaani Dkt Magufuli alionesha nia kabisa ya kuachana na hizi biashara za kuuza nchi ila eti leo akina Msukuma darasa la saba wanapelekwa kujifunza kuuza bandari
 
Mzee Malecela ashukuriwe lasivyo “niguse ninuke” tungekuwa tulishamsahau. Ila mi huwa sielewi huu nchi inaendeshwa na nani? Yaani Dkt Magufuli alionesha nia kabisa ya kuachana na hizi biashara za kuuza nchi ila eti leo akina Msukuma darasa la saba wanapelekwa kujifunza kuuza bandari
Msukuma akapewa tu kifunga mdomo.

Anayeendesha nchi anafahamika,
 
Kamati ya bunge isiweke mtego eti kupokea maoni. Ni jambo liko wazi kabisa. Hatupaswi kukabidhi nchi yoyote kuendesha bandari zetu. Watatuhukumu sio vizazi vijavyo ila raia wanaoshuhudia huu uhuni unataka kwenda kutekelezwa. Nchi ina uwezo kabisa kuendesha bandari zake kwa ubora ila hakuna utashi kwa lengo la kujinufaisha vigogo. Hakuna utaalam hatuna au hatuwezi kujipatia ila kinachohitajika ni uamuzi tu kufanya kazi kwa uadilifu na weledi.
Hatutaki hata maoni Huo Ni uwizi..Mama Samia unafanya Nini????
 
Najaribu kuwaza tu kwa nni marais wa kanda ya pwani wanapenda kubinafsisha Mali za uma je uwezo wao wa kufikkli ni mdgo ?
 
Kamati ya bunge isiweke mtego eti kupokea maoni. Ni jambo liko wazi kabisa. Hatupaswi kukabidhi nchi yoyote kuendesha bandari zetu. Watatuhukumu sio vizazi vijavyo ila raia wanaoshuhudia huu uhuni unataka kwenda kutekelezwa. Nchi ina uwezo kabisa kuendesha bandari zake kwa ubora ila hakuna utashi kwa lengo la kujinufaisha vigogo. Hakuna utaalam hatuna au hatuwezi kujipatia ila kinachohitajika ni uamuzi tu kufanya kazi kwa uadilifu na weledi.
tuliwabinafsishia wazawa ticts, Tanzania kama nchi tulipata nini? tuliambulia kukimbiwa na majirani waliokuwa wanaitumia bandari yetu na kuilipa serikali kodi. wafanyabiashara wengi hata wakitanzania wakakimbilia bandari za nchi jirani. Tulishuhudia wafanyakazi wa bandari hata wahudumu wa ofisini wakimiliki mali zisizoendana na kipato chao.
 
Uzi Dubai kichwa cha uzi Saudi au mimi sijaelewa ?
Dubai na Saudi ni kitu kimoja. Ukisema Dubai sawa na Arusha ndani ya Tz. Ila Dubai imefahamika zaidi kama nchi ksbb ya utawala wa majimbo na ni mji mkubwa wa kibiashara. Dubai ni sehemu ya Saudi Arabia.
 
Back
Top Bottom