ACT Wazalendo: Bandari ni Hoja ya Kiuchumi, Tunaunga Mkono Uwekezaji

Sep 11, 2014
5
17
Leo Jumatatu tar. 4. 9.2023 Saa 5:00 asubhhi Chama cha @ACTwazalendo kitatoa Uchambuzi, msimamo na Mapendekezo yake kuhusu sakata la #Bandari kati ya Serikali ya Tanzania na @DPWorldUAE.

-----
Tangu Mwezi Juni mwaka huu kumekuwa na mijadalambalimbali kufuatia taarifa ya Azimio la Bunge kuhusumapendekezo ya kuridhia makubaliano (IGA) kati yaSerikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikaliya Emireti ya Dubai juu ya ushirikiano wa Kiuchumi naKijamii kwa ajili ya uendelezaji na uboreshaji wa utendajikazi wa Bandari za Tanzania. Azimio hilo liliridhiwa naBunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo Juni10, 2023.

Kufuatia mijadala hiyo, mnamo Julai 5, 2023 Kiongozi waChama cha ACT Wazalendo aliunda Kamati Maalum yaWataalam 22 iliyoongozwa na Wakili Emmanuel Mvula,Mjumbe wa Kamati Kuu ya ACT Wazalendo na Msemaji waKisekta wa Mipango, Uwekezaji na Hifadhi ya Jamiikufanyia kazi masuala yaliyoibuliwa na Jamii kuhusuMakubaliano hayo na kutoa mapendekezo kwa Uongozi waChama Taifa.

Kamati hii ya Wataalam iliyoundwa kwa ajili ya kukishaurichama juu jambo hili ambalo limeleta mjadala mkubwakwenye jamii iliwasilisha Taarifa yake kwa Kiongozi waChama na kujadiliwa na Kamati ya Uongozi ya ACTWazalendo. Kamati ya Uongozi ya Chama inatoa msimamohuu rasmi wa chama kwa niaba ya Kamati Kuu yaACT Wazalendo.


----
Zaidi soma kiambatanisho hapa chini
 

Attachments

  • Msimamo wa ACT 2.pdf
    3.7 MB · Views: 4
Tunataka majibu ya hoja....

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
Leo Jumatatu tar. 4. 9.2023 Saa 5:00 asubhhi Chama cha @ACTwazalendo kitatoa Uchambuzi, msimamo na Mapendekezo yake kuhusu sakata la #Bandari kati ya Serikali ya Tanzania na @DPWorldUAE.

View attachment 2738378
Msimamo gani tena zaidi ya ule wa Ayatola Kabwe kuwa Bandari haijauzwa?. Tena anaulizaga kama Bandari imeuzwa kwa DPw mbona hawajaondoka nayo?;
 
Back
Top Bottom