Battle: Dar es Salaam vs Nairobi

Battle: Dar es Salaam vs Nairobi

TANAPA YATANGAZA UTALII ULAYA KASKAZINI - “MY TANZANIA ROADSHOW 2024”
1714835055871.png

1714835091026.png

1714835115388.png


Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limeshiriki katika msafara wa kutangaza utalii nchi za Ulaya Kaskazini ambazo ni Berlin-Germany, Copenhagen -Denmark, Oslo-Norway na Stockholm-Sweden yaliyoanza tarehe 29.4. hadi 3.5.2024. Msafara huu wa utalii unaojulikana kama "My Tanzania Roadshow" umeratibiwa na kampuni ya KILIFAIR kutoka Tanzania.

Aidha katika msafara huu jumla ya makampuni ya utalii 20 kutoka Tanzania yameshiriki wakiwemo mawakala wa usafirishaji, huduma za malazi pamoja na waendesha utalii wa puto.

"My Tanzania Roadshow 2024" imetoa fursa kwa ujumbe kutoka Tanzania kukutana na “Travel Agencies” zaidi ya 120 kutoka Germany, Denmark, Norway na Sweden.

Huu ni muendelezo wa kutangaza utalii na kuvutia uwekezaji katika masoko mapya yalioonesha ukuaji wa kasi katika kipindi kifupi pamoja na kuendelea kuhamasisha kwenye masoko ya zamani ili kufikia malengo ya kitaifa Tanzania kufikisha wageni milioni tano na mapato ya dola za kimarekani bilioni sita ifikapo mwaka 2025.
 
Hospitali za JKCI na Mloganzila ni awamu ya Kikwete si Magufuli!
Najua mkuu,ila yeye kasema Tanzania Samia ndio rais pekee aliyefanya transformation,na mimi nikamtolea mfano jumuishi baina ya Samia na watangulizi wake(Nyerere,Mwinyi,Mkapa,Kikwete,Magufuli) nani aliwekeza mambo muhimu katika afya?
Yani hapo ni watangulizi wote vise Samia.
 
Jamaa wapumbavu hawa, hivi wako serious kweli, phase II ishakamnilika ila watu wasubiri mwaka mzima ili kuanza kutumia! Ndo akili gani hii??
Kama hawawezi si watoe miundombinu kwa watu binafsi!

Hawa jamaa wajinga kweli!!
Mabasi yamefika?
 
Hao watu baada ya kujenga Mwendokasi mbagala low quality na vibanda vya kuku kama bus stop. Naona ni kampuni la ovyo bila kusahau Kulipa wafanyakazi wake 18000 kwa siku.
Ni kweli BRT Phase 2 imesuasua sana hata ujenzi wake ulikuwa ni wakijua kali sana! kuanzia kwenye mobilatizion ya equipments, vituo kama zahanati au wodi ya wazazi, Sijui kwa nini Hayati hakuwatia nyundo mapema mapema alikuwa anawazoom tu
Ila cha kushangaza hawa hawa ndo wanaojenga BRT phase 3, wamekuja kitofauti kbs, equipments zakutosha na kazi inaonekana imenyooka.
Imani yangu kubwa kwny BRT Phase 3 imekuwa zaidi kwa consultant ambaye ni SMEC International (Pty) Ltd huyu ndo aliyekuwa consultant pia kwenye BRT Phase 1, ni kampuni ya Australia iko fit https://www.smec.com/tz/
Ni ukweli usiopingika Consultant ana-play part kubwa sana katika kumshape Mkandarasi Site, kuanzia masuala ya safety, equipments, material, ubora na kadhalika. Wachina wakija Africa wanakuwa na ubabaishaji mwingi sana.
 
Back
Top Bottom