Nilisema mwanzo, ambitious za watutsi kutaka kuitawala eastern Congo zinatumika kama nyenzo na wazungu kuendeleza ukoloni mamboleo Congo.
Migogoro ipo ila inakuzwa na nje ya Afrika. Jamaa zako kwa fitna si mchezo, wanahusika moja kwa moja kuchochea migogoro mingi Afrika kwa kutumia machawa wao wanao rubuniwa na vipesa vichache. Nimekupa mfano hai wa misukosuko aliyoipata Magufuli kule Kibiti na kwenye bwawa la Nyerere ila naona kwa bahati mbaya au makusudi umekuwa unaupotezea.
Nitakupa mfano mwingine wa nje ya Afrika...
China miaka ya 1500s ndiyo ilikuwa nchi yenye uchumi mkubwa duniani. Miaka ya 1700s Waingereza wakawaletea wachina madawa ya kulevya (opium), walipokataa wakawapiga na navy yao iliyokuwa unmatched kipindi kile.
Wachina wakanyang'anywa Hong Kong na Waingereza wakaifanya kuwa kitovu cha kuendesha biashara ya madawa ya kulevya. The Hong Kong and Shanghai banking corporation (HSBC) ilianzishwa ili kuendesha biashara ya opium. Leo hii ndiyo benki kubwa Ulaya, imeichukua China miaka 200 hivi kurudi kwenye status yake ya uchumi mkubwa duniani, sisi Afrika hata hatujafikisha miaka 100 toka kupata uhuru.