Mkuu, japo hii list inamuweka Diamond na kiasi hicho Cha pesa, huo sio ukweli, hizi ni habari za kuhisi tu.
Mwanamziki tajiri kuzidi wote hapa EA ni Diamond, lakini hafikii hiyo pesa hapo, Kama amezidi Sana atakuwa anakaribi $7M, lakini hata hiyo Nina wasiwasi naye.
Bobi Wine hawezi kufika hata $3M, kwa mziki upi?, Labda Kama amepata kwenye siasa, zaidi ya miaka 6 hivi Sasa hafanyi muziki Yuko Bungeni.
Kuhusu Prof.J, huyo ndio kichekesho kabisa, juzi hapa mke na ndugu zake walijitokeza kwenye vyombo vya habari kuomba mchango Ili kulipia gharama za matibabu, vipi mtu mwenye mamilioni ya dollar aombe msaada wa matibabu?.
Kenya hakuna mwanamziki hata mmoja ambaye alishawahi kuvuka $1M mark, kwa muziki upi, kwa shows zipi, kwa mauzo yapi?
Sent from my itel L5007 using
JamiiForums mobile app