Haya mambo ya Magufuli hivi Magufuli vile tuachane nayo, ukweli utabaki palepale kwamba jamaa ametupa nguvu ya kutamba humu la sivyo Wakenya walikuwa wanatupiga asubuhi kweupeee, miaka nenda rudi walikuwa wanatutukana kwamba linchi kubwa na lina kila kitu lkn mazembe ya Tz yamekaa tuu, na huo ndio ulikuwa ukweli tukubali tukatatae.
Leo hii Wakenya tumewaacha mbali kwenye maendeleo, wamebaki na paper GDP ambayo nayo tunakwenda kuifutilia mbali. Magufuli alibadilisha maandishi kuwa uhalisia, Dodoma ilikuwa kwenye makaratasi, electrifitried SGR ilikuwa kwenye makaratasi, barabara nyingi mpk za mitaani zilikuwa kwenye makaratasi, masoko, ferries, terminals, flyovers karibu vyote vilibaki kwenye makaratasi jamaa akavibadili kuwa ukweli na ilibidi wapigaji wengi wamchukie ili leo tujivunie, tutoke kwenye matusi tuliyokuwa tunastahili kutukanwa.
So tumuache apumzike kwn tumefaidi kodi za wananchi zilizotumika kumsomesha, ila kama bado kuna watu wanaendelea kumtukana hii battle itachafuka mm nawaambia mana wengine sisi akitukanwa Magufuli tunaona kama tumetukaniwa wazazi wetu, me nasema patanuka humu ndani na hii battle itaharibika kabisa.