Mkuu, kuhusu chakula, Urusi imetoa shutuma kwamba chakula kilipelekwa nchi za Ulaya, lakini Ukraine ikakanusha, vipi umeamua kuamini upande mmoja bila hata kupata ushahidi?.
Majuzi tuu Ukraine na vyombo vyote vya magharibi vilisema Urusi imedondosha kombora Poland. Hata Biden aliposema hakuna ushahidi kuwa kombora limetoka Urusi, Ukraine bado waliendela kudanganya. Picha zilizopigwa na mkulima wa Poland zilionesha mabaki ya kombora hilo ni la Ukraine, lakini bado Zelensky aliendelea kuudanganya ulimwengu. Utawaamini vipi watu kama hawa?
Kuna mengi sana ya uongo yanasemwa na Ukraine, mfano wao kupiga kituo cha umeme cha Zaporozhia na kusingizia warusi, wakati warusi wamekuwa wakikimiliki toka machi 2022. Sasa unajiuliza kuna sababu gani ya warusi kushambulia kituo wanachokimiliki ?
Kuhusu hili swala la Wazungu kutumia njia za janjajanja, hapo umechanganya na haya maelezo uliyoweka haya uhusiano na tunalozungumza.
Hapo sijakuelewa, unaongelea nini?
Tunachozungumza ni kuhusu nchi za Ulaya kutumia mgogo wa nchi za Africa kupata chakula toka Ukraine, nimekuambia hiyo sio kweli, kwasababu Europe wanategemea gesi ya Urusi kwa 45%, lakini kwa kipindi chote tangu vita kuanza, wamekuwa wakisema na kupanga mikakati ya kuachana na gesi ya Urusi, hivi Sasa wanakaribia kabisa kuacha kutegemea hiyo gesi, vipi washindwe kuagiza chakula toka mataifa mengine wakati nchi nyingi duniani zinalima na kuzalisha hizo chakula badala yake eti watumie ujanja?
Ulaya wanakaribia kuacha kutegemea gesi ya Urusi? Aisee, sidhani hata unauelewa mzuri wa kinachoendelea.
Kwa taarifa yako Ulaya bado inanunua mafuta na gesi ya Urusi (LNG) kupitia mataifa mengine kwa gharama kubwa zaidi. China, India na Turkey wanafanya arbitrage, wananunua gesi ya Urusi na kuiuza kama LNG Ulaya kwa gharama kubwa. Gharama zinapanda kutokana na kuongezeka kwa hatua za kuchakata, kuhifadhi na kusafirisha liquified natural gas.
Ulaya sasa hivi viwanda vingi vinafungwa kwa kukosa gesi nafuu ya Urusi, unaweza kusearch "deindustrialization of Europe" ili ujiellmishe kidogo.
Ulaya imekuwa ikilalamika kuuziwa LNG na Marekani mara nne ya bei halisi, gharama zote hizi unafikiri nani atazilipa? Makampuni ya Ulaya yataweza vipi kumudu gharama kubwa za uzalishaji huku wakishindana na China? Ufahamu wako wa uchumi unaowaburuza wakenya kila siku hapa umeuweka mfukoni?