Mkuu, lengo kubwa la GMO ni kuwa na mimea inayohimili magonjwa na yenye kutoa mazao mengi zaidi na kwa muda mfupi.
Hivi Sasa hali ya rutuba imepungua Sana, wadudu wanaoshambulia mazao wamekua wengi na wamejenga usugu kwa dawa nyingi zinazotumika za kuulia wadudu mashambani, na ukame pia umeongezeka Sana.
Mimea hii ya asili inashindwa kuhimili mabadiliko haya ya kimazingira yanayobadilika kwa Kasi Sana, ni muhimu na lazima hiyo mimea na wanyama kubadilika ili kueandana na mabadiliko hayo.
Genetic Engineering inajaribu kuweka au kuondoa sehemu ya Genetic materials ambayo inaonekana kuwepo kwake au kukosekana kwake ndio kunasababisha huo mmea au mnyama kushindwa kupambana na mabadiliko hayo.
Mfano mzuri katika maisha ya binadamu ni Ugonjwa wa "sickle cell", huu Ugonjwa unatokana na kuwepo na "protein" Moja kwenye DNA za watu wenye tatizo la Ugonjwa huo. Hivi Sasa Kuna majaribio yanafanyika kwa kutumia "Genetic Engineering" ili kuiondoa hiyo "protein" na kuweka protein sahihi ili huu Ugonjwa upotee kabisa duniani. Au ugonjwa wa "Albinism" ambao unatokana na kukosekana kwa "gene ya melanin" tafiti zinafanyika ili kupandikiza gene ya melanin ili miaka ijayo, kusiwepo na Albino duniani, hapo tatizo la GMO lipo wapi Kama tutapata binadamu wazima bila magonjwa ya kurithi?.
Kwa kifupi, GMO ni kupata viumbe Bora zaidi kwa kubadilishia "weak genes na kuweka "strong genes" kwa kutumia Elimu ya "Genetic Engineering"
Sent from my itel L5007 using
JamiiForums mobile app