joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,111
- 46,621
Mkuu, wapo wabobezi katika Hilo eneo unalozungumza duniani na hata katika nchi mojamoja, je unao ushahidi wa kisayansi unaotokana na tafiti za kisayansi kuthibitisha Hilo unalolisema?.
Mkuu Kama tutaendelea kupiga bila kutumia ushahidi wa kisayansi tutaendelea kubaki nyuma Sana.
Ni ukweli usiopingika kwamba, nchi zilizoendelea wanajali Sana Afya zao kuliko sisi, Kuna vyombo vingi vinavyodhibiti ubora wa vyakula kuliko huku kwetu, raia wenyewe wapo "knowledgeable and very sensitive" na Afya zao kuliko sisi. Kuna makampuni ya bima za Afya na wanasheria wengi ambao wanafuatilia Sana makosa Kama hayo ili kuyashitaki hayo makampuni yenye kuuza na kutengeneza bidhaa zenye ukakasi Kama huo.
Ninakuhakikishia, Kama kungekuwepo na madhara katika GMO food Kama unavyofikiria, tayari mtiti ungeanzia huko huko na hizo bidhaa usingeziona huko Supermarkets.
Jambo Moja ninaloligundua kwako ni kwamba ni mtu unayeishi kwa kusikiliza Sana maneno na hupendi kufuata matokeo ya Sayansi, juzi Kati ulipingana na WHO, Leo unaanzisha sakasaka na FAO & WFP, sijui kesho utapingana na nani tena[emoji23][emoji23]
Chamoto
Sent from my itel L5007 using JamiiForums mobile app