Nimekuita mkenya kutokana na jinsi unavyojenga hoja zako. Ngoja nikuulize, hivi wewe ukianzisha duka au biashara yako ya kufuga kuku au hata ya kuchimba madini, lengo la biashara yako ni ipi Kama sio kusaidia familia yako?.
Kwahiyo hiyo biashara hata iwe kubwa kiasi gani, lengo kuu ni kusaidia ndugu na jamaa zako, lazima utawapa ajira ndugu zako, kitu kitakachokufanya uende kuajiri mtu mwengine ni uwezo wake na masharti ya vyombo vya fedha vinavyokupa mikopo, hakuna Sheria ya nchi inayokulazimisha utoe ajira, unaweza kuajiri mtanzania yeyote yule vile upendavyo.
Hiyo hufanyika duniani kote, nenda Japan ktk kampuni la Toyota, nenda Nigeria kwenye makampuni ya Dangotte, Nenda Marekani kwa Bill gate, zunguka duniani kote.
Ninachokiona ndani mwako ni chuki na wivu kwa baadhi ya jamii za watu hasa waliofanikiwa, kwanini usihoji mafanikio ya wachagga na wakinga ambao nao wanafanya vizuri Sana. Kwanini humtaji Reginald Mengi ambaye aliajiri watoto wake wawili na mdogo wake kuwa ndio wakurugenzi wa makampuni yake?
Wahindi ni wafanya biashara wazuri duniani kote na sio Tanzania au Africa pekee, wamesambaa duniani kote kutafuta maisha kwa zaidi ya Karne 4 Sasa, unataka kujilinganisha na wewe unayepiga Domo tupu?. Punguza wivu na chuki kwa watu waliofanikiwa, ongeza bidii ya kazi na nidhamu katika maisha.
Sent from my itel L5007 using
JamiiForums mobile app