Kote wawekezaji wapo na wanaendelea na heka heka za uwekezaji, kila nchi Kuna changamoto zake, kila muwekezaji anazo changamoto zake.
Kwamfano tukianza na Tanzania, ili kuchimba chuma kunahitajika umeme mwingi na uwe na Bei ndogo Sana, kwasasa Tanzania umeme wetu ni ghali, hivyo, Kuna wazo kwamba watumie makaa ya mawe yanayopatikana kusini mwa Tanzania, au gesi ya mtwara, Sasa hiyo ni miradi ndani ya mradi mkuu, lazima kujipanga upya, pia Kuna swala la kusafirisha hicho chuma baada ya kuzalishwa hadi bandarini, reli ni muhimu na huko Liganga hakuna reli kwa Sasa.
Upande wa Uganda, Mambo ni Kama hayo, wanafikiria kutumia Bomba litakalojengwa la kusafirisha mafuta Yao ili nao waweze kuunganisha na Bomba la gesi toka Tanzania kabla hawajaanza kuchimba chuma, Machimbo ya chuma yanahitaji umeme mwingi Sana.