Mabwawa kwani unadhani huko kuna mito? Au una-assume kwamba kuna mito kila mahali Kenya. Kenya ni nchi kame sio kama huko kwenu nchi ya asali na maziwa. Mnapata mvua kila siku. Bwawa linaweza kujengwa tu mahali ambapo kuna mito ila asilimia kubwa ya kaskazini mwa Kenya hakuna mito kabisa na pia hakuna ziwa wala kiini chochote cha maji. Maji wanayotumia ni ya borehole pekee na pengine springs (yaani maeneo yenye mashimo madogo yenye maji machache). Boreholes na springs pia huwa yana matatizo yake ikiwemo kukauka. Boreholes na springs au oases huwa zinakauka baada ya muda fulani. Borehole pia inaweza kuwa na maji ya chumvi na maji hiyo haiwezi kutumika katika kupika chakula au kunywa maji kwa binadamu au mifugo. Kaskazini mwa Kenya ni mahali ambapo Mwenyezi Mungu pengine alisahau kabisa kuwapa vyanzo vya maji. Sio kwamba wao ni watu lazy, hawataki kufanya kazi. Unakuta mtu ana bidii ya mchwa na ni mfugaji hodari ana ng'ombe mia moja ila ukame ukija, anapoteza ng'ombe wake wote. Mtu kama huyu sio mtu wa kumcheka bali ni mtu wa kumhurumia. Hawana vyanzo vya maji kabisa. Kwa hivyo ukiona wanapata matatizo ya njaa na ukame ni kwa sababu mazingira hayo ni mabaya sana. Kuna joto na jua kali sana hata kama kungekuwa na mto, basi maji ya mto huo yangeyeyuka. The water in the river would have evaporated. Kwa hivyo tatizo hili la ukame na njaa ni tatizo la mazingira yaani climate ya huko sio nzuri kwa kutunza maji. Maji yanayeyuka. Kwa hivyo bwawa haliwezi kujengwa huko maana hakuna mito. Suluhisho ni kuchimba boreholes zaidi. Hakuna suluhisho nyingine. Hawa sio watu wa kuwacheka kama Wabongo mnavyopenda kufanya, hawa ni watu wanaostahili huruma na msaada. Tanzanians should have empathy on these people instead of laughing at them. Sio kupenda kwao kwamba walizaliwa maeneo hayo.
cc
ichoboy01
joto la jiwe