Battle: Dar es Salaam vs Nairobi

Battle: Dar es Salaam vs Nairobi

And that's why dodoma your "capital city" looks like a battle field!!!!how can a responsible government compete with a private sector?. Eti majengo marefu!jengo refu pekeyake Tanzania ni Mt kilimanjaro...
Hujajibu swali mzee wangu, me sijaulizia kuhusu private sector kuwekeza majengo marefu lahasha, swali kilikua hiv kuna jengo refu hata moja hapo kenya ambalo linamilikiwa na wakenya, kama ambavyo tz majengo yote marefu ni mali ya Tanzania.? Ili kusudi tujue nani Kati yetu anajiweza without external investments, sio mnapiga mbamba mingi humu kumbe hamjiwezi ni kelele tu.. alafu kuhusu Dom mzee, mji mzima unajengwa high rise buildings ni kama zote it's just a matter of time utanionea, you just wait and see
 
Courtesy of bus world and Tanzania regional bus 🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿
tanzania_regional_buses-post-2021_10_02_20_35-1.jpg
tanzania_regional_buses-post-2021_10_02_20_35.jpg
 
Ujenzi wa njia nne kutoka Dodoma hadi Morogoro wazidi kunoga
Muungwana Blog 3 Nov 20, 2019
View attachment 1960352

Waziri wa Fedha na mipango Dkt. Philip Mpango amefanya mazungumzo na Benki ya maendeleo ya Afrika (AfDB) ili iweze kuipatia Tanzania mkopo nafuu kwa ajili ya kujenga barabara ya njia nne toka mkoani Morogoro hadi Jijini Dodoma kwa lengo la kuboresha usafirishaji wa abiria na mizigo.

Ametoa ombi hilo Jijini Dodoma wakati alipokutana na Mkurugenzi mtendaji wa bodi ya wakurugenzi ya benki hiyo Amos Cheptoo anayewakilisha nchi nane za ukanda wa Afrika Mashariki.

Amesema ombi lake kwa Mkurugenzi huyo wa AfDB ni kuona namna gani wanaweza kuanza kuliweka jambo hilo kwenye miradi ambayo benki hiyo imekuwa ikiigharamia ili kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo ya njia nne itakayo kuwa na uwezo wa kupitisha magari mawili kwa njia ya kwenda na ya kurudi.

“Baada ya Dodoma kuwa Makao Makuu ya nchi tunahitaji usafirishaji kwa njia ya barabara uwe bora na haraka zaidi lakini pia tuweze kupunguza ajali maana kuna ajali nyingi kwa sababu magari yanayokwenda Dar es Salaam na yanayokuja Dodoma au kwenda Mwanza yanapishana kwenye njia moja,” amefafanua Dkt. Mpango.

Akijibu ombi la Waziri Dkt. Mpango Mkurugenzi mtendaji huyo wa Bodi ya wakurugenzi ya benki ya AfDB Amos Cheptoo amesema watahakikisha Tanzania inapata mikopo ya miradi yake ya kimkakati na ya kipaumbele ukiwemo wa ombi hilo la ujenzi wa barabara ya Morogoro hadi Dodoma kwa kiwango kinachokusudiwa.

Kuhusu uwezeshwaji kwa taasisi nyingine nchini Cheptoo amezitaka sekta binafsi kuchangamkia fursa za mikopo nafuu zilizopo katika benki hiyo kutokana na kuwa na nafasi nzuri ya upatikanaji wake ili ziweze kujikwamua kiuchumi na kutokomeza umasikini barani Afrika.

“Sekta binafsi za Tanzania hazijatumia vizuri dirisha la mikopo ya AfDB ikilinganishwa na chi nyingine za ukanda huu wa Afrika ninakuomba Waziri wa fedha uwahamasishe wakope fedha hizo ili kukuza mitaji yao na kuongeza ajira,” amedisitiza Cheptoo.

Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imefadhili miradi 23 nchini ikiwemo 21 ya umma na miwili ya sekta binafsi ikiwa na thamani ya dola za kimarekani bilioni 2.1 katika nyanja za nishati, miundombinu ya barabara, usafiri, kilimo, maji na usafi wa mazingira.


Yah ila kipande cha Dar morogoro ndio cha muhimu zaidi kwaiyo hawewezi kujenga moro -dom kabla ya Dar moro kwanza
 
Back
Top Bottom