Battle: Dar es Salaam vs Nairobi

Battle: Dar es Salaam vs Nairobi

Hapana hii ni ideology ya watu wa kitaambo. Saiv ukijinga majengo marefu kwa mji caliber ya Arusha unaifanya ipendeze zaidi. Ngoja nikupe mfano. Hii apo vancouver city. View attachment 3571454

Ni kweli inapendeza ila unakuwa umeondoa sifa kuu ya utaliii arusha. Wageni wengi wanaokuja hasa kutoka mataifa ya ulaya wanataka Ile natural beauty, ndo maana arusha kuna mpaka mashamba ya kiutalii ambapo unakuta wazungu wanataka wakanywe zile mbege na sio bia.
Maghorofa ni mentality yetu sisi kuwa ndo itavutia wageni ukienda karatu ukiwa umetokea mto wa mbu kuna watu wamejenga nyumba za kilocal sana kwa ajili ya watalii na wanapiga kwa chumba Cha nyumba ya udongo zaidi ya yule mwenye ghorofa.
Ili tufanikiwe tukibaki kuitumia asili yetu kutunufaisha.
Kama ni miziki au makazi tuyaboreshe kwa kuendana na asili yetu badala ya kuiga za kigeni.
Leo kuna kuna madj wanalipwa madolari ya kufa mtu ulaya kwa ajili ya kupiga disco vumbi huko ulaya . Sio Kila nyumba nzuri lazima iwe ghorofa
 
Back
Top Bottom