Tatizo scope pekee ya mapungufu ya demokrasia unayoangalia ni Utekelezaji wa mipango ya nchi. Kwamba, kama angeruhusu opinions za watu wengine basi asingeweza kukamilisha mipango yake. Lakini Unadhani kuwa kila mpango wa Magufuli una tija na feasibility? Mfano ni issue ya Chato. Sehemu ambayo hata kwenye map haionekani Kwa urahisi Mara ghafla anataka kujenga international airport, a major district hospital, a stadium etc.. Lakini uwekezaji wote huo ni hasara Tupu! Kama demokrasia ingekuwepo na maswala haya yakafanyiwa majadiliano bungeni na upinzani ukatoa hoja zao, basi hasara hiyo isingetokea. Lakini kwasababu alikuwa Dikteta, lolote alilopenda Moyoni mwake alilifanya.
Na pia mapungufu ya demokrasia kwenye uongozi wake yalionea watu wote waliompinga. Hata humu mtu yoyote aliyeongea hata sentensi moja ya kumkosoa Magufuli alikuwa bullied (absolute psychopathy). Uhuru wa kujieleza ulishuka, uhuru wa vyombo vya habari Ndio hata usiseme. Kiufupi, everything was a mess. Lakini majority ya watanzania, say, 84% walikuwa bega Kwa bega na udiketa wake. Why? Mass manipulation.