Binafsi sina tatizo na rais mstaafu kupewa zawadi ya gari itakayoendana na hatua ya maisha aliyofikia (ya chini chini). Tatizo langu ni thamani ya gari na timing yake.
Katika nyakati ambazo kuna makundi ambayo unayaambia seeikali yako haina uwezo wa kuyakirimu kwa kiwango tarajiwa (watumishi, wazee, nk), unapotoa zawadi kwa niaba ya serikali na taifa yenye thamani hiyo ni kama unaleta utani vile.
Ishu ya nyumba kwa rais mstaafu ni kweli usemavyo. JPM hakuanzisha utaratibu huo bali ni sheria ambayo ilikuwepo ila haikuwa ikitekelezwa. Yeye alirejesha utekelezaji tu.
Rais alivyotaja zawadi ya 'gari ya chinichini' haraka nikadhani kuwa angepewa moja ya zile state cars (benz) zilizonunuliwa pindi ile ya SADC summit. Ndiyo, zawadi si lazima iwe mpya hasa katika nyakati ambazo "uchumi umeshuka hadi asilimia 4".
Kuhusiana na pesa alizokuwa akigawa Magu ziarani binafsi huwa sipendi kujiuliza maana huenda zilikuwa za kwake binafsi! Sasa kama za kwake binafsi hakuwa na sababu ya kueleza zimetoka wapi.
Sent using
Jamii Forums mobile app